Yoyote yule anayebeza juhudi za Dr Magufuli toka ameingia madarakani 2015 basi ni lazima mtu huyo atakuwa na tatizo la akili.
Dr Magufuli amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania wanafanyakazi kwa juhudi zote, wala rushwa wanashughulikiwa, mafisadi wanasumbuliwa, pesa ya umma unatumika kama ilivyopangwa, miradi yote inamalizima kwa wakati.
Kwasababu hatupendi kufanya kazi na tumezoea mteremko basi tunamuona Dr Magufuli ni mwiba mkali.
Dr Magufuli ana malengo makubwa na Tanzania wengi haoni kwa sasa.
Akili za Lumumba ni sawa na verifications za Twaweza,,Onyesha aliyoyafanya Magufuli,yaorodheshe tuone si kusema sema bila evidences zozote,
Mambo aliyofeli Magufuli mpaka muda huu ni haya yafuatayo
1,Ahadi ya kuwashughulikia mafisadi kwenye mahakama ya mafisadi,mpaka muda huu hakuna mtu hata mmoja aliyeshitakiwa kwenye mahakama ya mafisadi,pia licha ya kutumia mahakama ya hakimu mkazi kisutu kupambana na mafisadi mpaka sasa hivi hakuna mtu yeyote aliyetiwa hatiani,awali waliwakamata watu kwa mbwembwe ohhoo Masamaki amekutwa na mafurushi ya hela ndani yamefukiwa,ohhho masamaki ana nyumba 70 Mara 80 lakini siku ya siku masamaki hana kesi,(Watanzania tunayaona na kuyahifadhi kwenye gallery)
Tofauti na Masamaki kuna vigogo wengine wengi tu wameachwa hakuna kilichofanyika,au vigogo wengine wameisababishia serikali karibia billion 4 lakni hukumu inatoka eti wanahukumiwa kwenda jela miaka miwili au kulipa faini million 30, jamani hii ni haki kweli,mtu amesababishia hasara serikali billion kadhaa then alipe million ambazo ni hela ya kutoka na mchepuko weekend mlimani city(Watanzania tunaweka Gallery)
Magufuli amefeli vibaya kwenye sekta ya kilimo,Watanzania 75 % ni wakulima, serkali makini inatakiwa asilimia kubwa ya bajeti yake iweke kwenye kilimo,ili kutoa mazao mengi ya kula na biashara kupunguza baa la njaa na kupeleka mazao viwandani,(serikali ya viwanda ) mpaka sasa sekta hii ndo ya mwisho hapa Tanzania licha ya kula na watu wengi, serikali yenyewe haina mipango mikakati ya kuinua mkulima halafu ukisimama jukwani unasema Tanzania ya viwanda,jamani hebu tujikumbushe tuliosoma history ya ulaya na China,mfano uingereza hadi kufikia kwenye viwanda,mapinduzi yaliyofanyika na kuelekea kwenye uchumi wa viwanda ulikuwa mapinduzi ya kilimo kwanza(agro-revolutuion) awali walichukua maeneo wakawapa matajiri ili wazalishe"enclosure system) na matajiri (bourgeoisie) wakazalisha wakapelekea mapinduzi ya viwanda(industrial revolution) lakni Tanzania badala ya kuwatengenezea matajiri mifumo na kuwaencourage wawekeze kwenye kilimo badala yake serikali inapambana nao ili wawe masikini,utadhani sasa Tanzania ndo inaingia kwenye kipindi rasimi cha ujamaa( socialism)
Kufikia jana mauzo ya nje Tanzania imeshuka sana,(Watanzania tunatunza kwenye Gallery)
Ukweli na uwazi,licha ya serikali hii kujipambanua kuwa ni serikali ya wanyonge na masikini ina maana wanyonge wawe na haki kupata taarifa za serikali kwa kile kinachofanyika lakini hakuna na hakuna kipindi kigumu cha kupata taarifa za serikali kwa uwazi kama kipindi hiki,yaanni serikali ya sasa inaficha vitu sana,na kwa nini inaficha vitu ambavyo mtanzania inapaswa avipate ili ajue mfano masuala ya kiuchumi,B.O.T wamezilalia sijui ni kwa nini,pia suala bombadia kukamatwa huko Canada na serikali kuja na majibu mepesi kuwa kuna wanasiasa wamesababisha,ni kitu ambacho serikali hii imechemsha,wanaccm na serikali yao wakae wakijua Watanzania waliokuwepo miaka 30 iliyopita siyo wa sasa hivi,unapokuja na hoja nyepesi unajikaanga mwenyewe,hiki kizazi kinachambua pumba na mchele,fanya tu utafiti Mdogo ,chukua vijana 10 wa mtaani kwako waliozaliwa kati ya 1980 -1995,waulize kitu chochote kuhusu bombadia watakupa majibu ndo utajua things are changed
Elimu,nchi yoyote duniani ambayo imepiga hatua katika uchumi wao na teknolojia cha kwanza waliwekeza kwenye elimu,
Elimu ya juu,licha ya serikali hii kujipambanua kuwa wanakusanya mapato million 200 kwa siku,watoto wa maskini wameshindwa kujiunga na elimu ya juu, hakuna kipindi kigumu kwa watoto wa maskini kupata elimu ya juu kama kipindi hiki,yaani ni huzuni ,angalau serikali ya kikwete licha ya kuwemo wapiga dili wengi lakini wanafunzi wa kipindi hicho walinufaika,wengi kwa kweli walipata mikopo lakini awamu hii,watoto wa maskini ndo wanahali ngumu haijawahi kutokea, waombaji elfu 70,wanapata elfu 20,ni swali la kujiuliza kwa hiyo Watanzania sasa hivi ndo matajiri wameongezeka au la,maana ukianagalia ingawa si takwimu rasmi ila ni usambamba wa takwimu hizo,watoto elf 50 wanatoka kwenye familia za matajiri,
Mambo mengi sana magufuli amefeli,madeni ya serikali lukuki si nje wala ndani,kibao,elimu bure mpaka sasa hivi kuna shule hazifanyi mitihani ya ndani
Hospitals hakuna madawa,swali alijitutumua kupambana na maduka yaliyopo karibu na hospili za serikali baadae amaeshindwa ,sasa hivi ndo maduka yameongezeka na sasa hivi ndo wagonjwa wananunua dawa kwa kasi,bila mfumo thabiti serikali hii itachemka sana