Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Dk Magufuli haitaji kupiga kampeni katika uchaguzi ujao, ili uweze kupata kura yangu na watanzania kwa ujumla, yale uliyofanya Kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani yananilazimisha kumpa kura yangu, na kutokufanya hivyo nitakuwa nimefanya dhambi isiyosameheka.

Nangojea pia kwa shauku kukamilika kwa stigler George ili tuepukane na adha ya gharama kubwa za umeme pamoja na kuanza kazi Standard gauge Railway Mwanza to Dar ndani ya masaa kadhaa.
 
2020 Magufuli atakaa zake TBC na kupiga kampeni five words will kill the giant(just a guess)
 
Watu wawe fair kwake (Rais Magufuli kwa namna anavyochapa kazi) Wampe credit.. Reformation ya nchi masikini kama Tanzania ambayo ina vitu vyote.. then tu, ilikuwa inakaliwa na watu wachache wanatuvuruga tu.. wanagonganisha vichwa wanatuvuruga tu.. kwa sababu tu, hawataki kuwa na dhamira njema; Yeye (Rais Magufuli) anaingia ndani ya miaka mitatu.

Watu wanaanza kuona results hata kama hutaki basi nyamaza!!”(kukubali na kusema kuwa Mhe. Rais na serikali inafanya mambo ya maendeleo na kujenga Tanzania mpya

Wanaochezelea kodi watumbuliwe bila kujali wanatoka Kolomije au wanatoka Same kwa Mama Anna Kilango. Haki itendeke sawa.

Piga kazi rais Magufuli
 
Hapo mwisho labda nimekuelewa
 
Naona sasa kilichobaki ni kulazimisha pongezi kipropaganda.

Sent using Mikoyan MiG-29
 
Ulivyoanza nilidhani ni bandiko la kusifu, kumbe unapiga chapuo mtu atumbuliwe!.
Mtangoja sana!, Au Mtasubiri sana!.

Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!. - JamiiForums
P.
unasifia uharibifu tu kwasababu mhusika ni Msukuma kama wewe au sio?
we kweli mzigo.
Rais kaeleza wazi kuwa Makonda anaweza kuwa Mbadhilifu . na mfano akatoa kuwa huenda akaingiza Container 10 kisha akapeleka 2 mashuleni na Zingine Akauza pembeni.
RAIS wa nchi akifikia kutamka maneno kama hayo kwa MTU aliyemchagua yeye maana yake HANA IMANI NAE TENA.
AU nyie wasukuma mtu mpk auwe ndio mnashtuka?
 
Kwani mkuu kilo ya sukari kwa sasa huko kwenu bei gani? hapo kwa mangi cement anauzaje?
 
TATIZO LENU UVCCM MNASHINDWA KUTOFAUTISHA KATI YA KUSHAURI NA KUPINGA. MTU AKIKUAMBIA KUWA BADALA YA KUNUNUA NDEGE NUNUA KWANZA MADAWA NI TOFAUTI NA ANAYEKUAMBIA HATUHITAJI NDEGE. TATIZO LA SERIIKALI YA AWAMU YA TANO HAIJUI VIPAUMBELE (PRIORITIES) VYAKE NI VIPI
 
Mimi sina chama, lakini naunga mkono maendeleo. Kweli anachapa kazi
 
Mikoa iliyobaki ni Kigoma na Katavi. Mipango ya kuiunganisha mikoa hii ipo ila utekelezaji wake haueleweki. Mikoa hii ni muhimu iunganishwe ili kuinasua kwenye wimbi la umasikini. Nitoe muono wangu. Mkoa wa Kigoma ukiunganishwa kwa lami utaendelea kuliko matarajio. Hii ina maana utakuwa umeunganishwa na Tanzania nzima, Burundi na DRC.Mkoa huu unafanya biashara na Tanzania nzima, Burundi na Congo. Kwa hiyo ina maana miundo mbinu ikiboreshwa maendeleo yatapatikana kwa urahisi. Siyo kwamba nasisitiza barabara za lami kwa vile mambo mengine sijayaweka maanani. Hapana. Ya kufanyika ni mengi ila barabara za lami ziwe kipaumbele cha kwanza. Baada ya hapo kuna mengine kwa mfano bandari ya Kigoma, meli za abiria na mizigo katika ziwa Tanganyika. Yaani kama Raisi anavyofanya kule Mwanza ingekuwa vizuri na Kigoma pia. Siwezi kuzungumzia SGR maana imeshatupiga chenga. Lakini kwa maoni yangu SGR ilibidi ielekezwe Kigoma na siyo Rwanda. Hapa tunalenga uchumi wa Eastern Congo na Burundi vs Rwanda. Unajua Wa Jeremani ingawa na wao ni wakoloni mipango yao ilikuwa makini sana. Kujenga reli Dar to Kigoma haikuwa ajali. Mpaka sasa tukiacha ubinafsi SGR ya Dar Kigoma ndiyo hasa ina sound economically.
Kwa hiyo ni matumaini wenye nchi wazinduke na kutupia macho Katavi na Kigoma. Mikoa yote isaidiwe ipate maendeleo. Isibaguliwe mikoa michache. Inawezekana ubaguzi unaoonekana siyo wa makusudi bali ni kukosa uchambuzi sahihi. Ikiwa ni sababu hiyo ni bahati mbaya maana tunahitaji sana fikra makini za kutekeleza ndoto zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…