Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Kwa sababu ya mapungufu yetu binadamu, hakuna kiongozi anayekubalika na kila mtu! Kwa mtaji huo basi, pamoja na kwamba kiongozi anaweza kuwa hakupata kura yako na alishinda kwa kura za watu wengine tu, huyo kiongozi ni kiongozi wako hata wewe usiyempenda. Labda uhamie kwingine, na sijui utahama mara ngapi!
 
Katika marais waliofanya vyema ni mzee wa msoga japo alikuwa na mapungufu mengi
 
Kwani kushangiliwa yeye ss inatuhusu nini? Ndo inapunguza au kuongeza nini kwako wewe kama wewe?
 
Kwani kushangiliwa yeye ss inatuhusu nini? Ndo inapunguza au kuongeza nini kwako wewe kama wewe?
Kama hujui inapunguza basi pole sana; tena sana na sidhani hata kama ukieleweshwa utaelewa manake huelekei kama ni mwenye kuelewa!
 
Rais MAGUFULI ameona umuhimu wa kuifufua njia za reli ambazo ziliachwa zijifie anafahamu na ameona umuhimu wa reli ktk maendeleo ya nchi yeyote duniani,Rais MAGUFULI anaweka umememe wa uhakika ktk kwa ajili ya maendeleo ya kweli,Rais MAGUFULI amenunua ndege ameifufua Atc iliyokuwa imejifia,kwa haya mambo matatu tunapotamka mageuzi ya kilimo na hata viwanda bila kuwa na haya mambo matatu kama msingi wa mageuzi itakuwa tunajidanganya kwa sababu tunahitaji umeme wa uhakika kwa ajili ya viwanda bila kujali ni viwanda vya kusindika mazao yatokayo mashambani ama kutengeneza bidhaa za kawaida,tunahitaji njia ya reli kwa urahisi wa kusafisha bidhaa za viwandani na hata mazao ya mashambani kutoka sehemu moja kwenda nyingine,hii njia ya reli ni rahisi kwa bei na hata ina uhakika kuliko barabara.tunapoongea utalii wa ndani na hata nje bila uhakika wa usafiri kwa njia ya anga tutakuwa tegemezi tusiokuwa na uhakika..hongera MAGUFULI,MUNGU akutunze.
 
Nitsashangilia saana utakapoRUDIHWA USAFIRI WA WARRANT kwa wanafunzi na watumishi wa serikali aisee na pia kuifufua reli ya Manyoni Singida na ile ya Arusha yaani
 
Umesahau kumsifia pia kwa jinsi alivyoipaisha 1.5 trln toka hazina na jinsi anavyotoa 2.4trln hazina na kumzuia CAG kuyakagua matumizi yake.
Heko kwake [emoji85] [emoji85] [emoji85]
 
Umeshindwa kuweka hata paragraph kwenye huu upumbavu uliouandika.
Hebu mwambie huyo unaempa sifa za kijinga atueleze ataifanyia nini korosho maelfu ya tani yanayoendelea kuoza?
Pia muulize atawalipa lini wananchi pesa zao za korosho?
Tatu, muulize ata recover vipi hasara aliyoisababishia nchi kwa maamuzi yake yasiyo na tija kwa taifa hili?
Kuanzia ameingia kila kitu kinakufa tu
 
Juzi niliona Member wetu mleta mada za jikoni akileta swali la uchokonozi kuhusu kwamba umaarufu wa Magufuli umeisha duniani, hii hapa kwenye picha ni kundi la watu huko Namibia baada ya kumuona Magufuli anaanza safari za nje wameanza movement Magufulification of Naminia





Mitaa imeshaanza kuwekwa Bendera na picha za Magufuli

 
Safi sana....... Chadema tuko pamoja nao!
 
Hivi kukubalika nje ya nchi au kutokukubalika kunapimwaje? Kwa kuwekwa picha ya mhusika? au kupokelewa au kwa jinsi unavyoongelewa kwa kule unachokifanya,MaCCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…