Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania


Juzi tuu mkopo wa WB kuzuiwa tuu Wanaccm kwa umoja wao wataka Zitto auwawe halafu Leo unaleta ngonjera?
Lakini ndio zenu hizo maana hata mwenyekiti wenu Leo kusema hii no bluu na kesho kusema ni nyeusi ndio zake hivyo hatuwashangai.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wala hawanipotezie mda hapa nipo zangu kazini nimekutana na upupu wako nkasema nikuulize tu. Bado siku chache mshahara wangu mnono uingie kwa acount.
So wala hawanipotezei mda.
Kichinjio changu tu siku ya kukitumia kidoogo ndio ntapotezewa mda kwenye kupanga mstari lkn naamini itakua siku ya jumapili. So sio issue.
Ishukuru CCM kwa huo mshahara mnono bwashee vinginevyo ungeungana na shoe shiners pale Useri!
 
Hilo tu baasi? kwa hiyo kwenu nabii siyo yule anayeagizwa na Mungu kufikisha maagizo yake kwa wanaadamu siyo?
Ukichaguliwa na Mungu wewe ni nabii tayari!

Magufuli ni chaguo la Mungu hata sheikh wa mkoa alhad Salum hutukumbusha hilo mara kwa mara!
 
Ishukuru CCM kwa huo mshahara mnono bwashee vinginevyo ungeungana na shoe shiners pale Useri!
Bwashee mimi sikusomea Tanzania wala na Niko zangu nabeba box kwa shift huku.
Hayo mambo zako za ccm hazihusiki. Jaribu kingine labda
 
Sijui unatumia nini kufikiri! Juzi tu tumepokea msaada wa vifaa tiba
Kwani majuzi kabudi alienda USA kufanya nini?Bajeti iko huko tril karibu arobaini,uwezo wetu wa kukusanya ni haifiki hata nusu ya bajeti,je kiwango kinachobaki tunatoa wapi?Yaani wanaongea as if sasa hivi bajeti haitegemea misaada!
 
Ukichaguliwa na Mungu wewe ni nabii tayari!

Magufuli ni chaguo la Mungu hata sheikh wa mkoa alhad Salum hutukumbusha hilo mara kwa mara!

Nini sheikh wa mkoa? Hata akisema wa dunia kama hilo halipo katika dini hilo ni la kwake mwenyewe kama unavyosema wewe ni la kwako kwa maana huwezi kuthibitisha kwa maandiko, Nabii ni yule aliyetumwa na Mungu kuwafikishia binadamu ujumbe wake, sasa huyu wa kwako ni ujumbe gani mpya aliokuja nao??
 
Hallow habari zenu


Ninerud Tena baada ya jana kuleta Uzi unao zipongeza juhud za MAGUFUL kupambana na Corona bila kuleta athar kubwa ya ki uchumi

Yamekua masaa machache tu toka tulipo sema Jana kua MAGUFUL atakuja kua mfano wa kuigwa dunian pia ataonesha kua kupambana na corona suluhu Sio kufungia watu ndani.suluhu ni kutoa elim namna ya kujikinga na kutafuta dawa. Turud kwenye point kwanin nasema maguful amekua mfano wa kuigwa ni baada ya baadh ya nch kuanza kuona kwamba kufungia watu ndani nikuatarisha maisha ya watu ajira pia hata uchumi wao na bila faida yoyote ya kupunguza maambukiz Bali kupata hasara

Kitu kizur na Cha kufuraisha ni baada ya marekan leo kutangaza kua hawato ifunga New York Yan hawawez New York karantin watu waendelee kufanya shughuli zao Ila tu wasiende Safar zisizo na ulazima pia waakikishe wananawa mikono kila wakati na kujiweka saf. Ukiangalia marekan New York ndio majimbo yanayo ongoza kwa kua na maambukiz ya korona lakin wameona athar watazo zipata pind watakapo ipiga Lock down New York hisa zitashuka pia uchuki utatetereka.
Na kwa mtizamo wangu siku si nying nch zingine zitaanza kuiga mfani mzuri wa Rais maguful na kukubaliana na mawazo yake ya Kaz lazima zifanyike na mapambano lazima yaendelee.

Pia watu walisema Jana kua ni mapema Sana kumsifia magugul ndio ni sawa Ila kwa mapema io io bado magufuli anafanya vizuri so acha tumpe sifa Mana yanayo endelea nch za jitan yanaogopesha na pia wote walio funga nch zao hawato weza kuendelea kufunga lazima watafungua tu Mana Corona CHANJO itapatikana mpaka baada ya nwaka mmoja so watu wataendelea kukaa ndani nwaka mzima?
Na wengine watafungua sababu tu marekan hajafunga

Hongera magufuli Ila wananch wako tumesikia kua Kuna nanii anaumwa Kama nikwel mzee asije akakuchafulia sifa zako aende kwenye kituo Mana vijana wa ufipa wanatafuta silaha ya kukuumizia




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika Hali hii iliyopo, Kwanza inabidi, tuondoe hofu, watalaamu wetu wakae, wajadiri Kwa kina, halafu waje na pendekezo ambalo litakuwa mbadara wa yanayo/yaliyotumika kwenye mataifa mengine,

Kwa sababu gani, Sina utafiti wa kutosha kuhusu nchi mbalimbali zilizochukua uamuzi wa kufungia watu wao, kama ndiyo njia Bora na imeleta matokeo Kwa haraka, Kwa sababu, Leo hii ni Kati ya miezi miwili SASA kwenye nchi kama USA na kwingineko, lakini idadi ya waathirika imekuwa ikipanda kila leo, na wakiwa under lockdown

Janga hili linahitaji itumike akiri kubwa sana ktk nchi zetu hizi za mwishoni kabisa, ukifanya masihara kuamua Jambo Kwa mihemko, unaweza kusababisha janga kingine kubwa zaidi kuliko Corona yenyewe,

Mimi nadhani, kila mtu ifike pahali aanze kumwona mtu mwingine ni kama muuwaji, au jambazi, hivyo akae naye mbali Sana, Tufanye kama hatujuani Kwa muda huu tulionao, na hii ndiyo iwe lockdown yetu, ikiwezekana, fimbo zitembee, ikiwa watu watakuwa wanakaa Kwa karibu karibu, Tusisogeleane Kwa sababu kufanya hivyo ni kama kujiruhusu wewe ufe.

Hili la kujifungia, ni kama imekuwa ni njia yenye mateso halafu haisaidii, lkn labda miji yetu ndiyo ifungwe,hakuna kuvuka kwenda mji mwingine, wa dar ni wa dar Tu, mwanza na Arusha na mikoa mingine iwe hivyo hivyo,
 
NI wazi Watanzania wengi wapiga kura, labda kwa ujinga wa kisiasa na uwezo mdogo wa kuona mbele, wana silka ya kuchagua viongozi kishabiki. Hili jambo alilikekemea sana Mwal. Nyerere wakati fulani juu ya Kikwete, ambaye alikuja kuwa raisi baada ya Nyerere kufa. Wengi tunaamini kwa dhati kama Nyerere angekuwapo Kikwete asingekuwa mgombea wa CCM pale 2005.

Lakini acha tugange yaliyopo. Kwa sababu moja au nyingine Magufuli alichaguliwa kuwa mrithi wa KIkwete. Wapo wanaoona walikuwa na sababu za msingi kumchagua yeye, lakini wengi ni wale ambao wa,imchagua kishabiki tu, bila kufikiria ya baadaye.

Sasa labda tuchukue muda na kujiuliza, tuweke ushabiki kando. Je baada ya hii miaka karibu mitano ya Magufuli, nini maoni yako katika utendaji wa Magufuli ukilinganisha na kama raisi wetu angekuwa Bernard Membe, Mark Mwandosya, Mwigulu Nchemba au January Makamba, hasa ukifikiria jinsi wangeshughulikia maendeleo na uchumi wa Tanzania, siasa za upinzani nchini, uhusiano wa kimataifa, uwajibikaji katika kazi na uongozi, kuchunga rasilimali zetu, utawala wa sheria na demokrasia kwa ujumla, na hata kukabiliana na janga la Corona?

Hili ni swali ambalo linahitaji utumie akili kidogo kujibu. Kama una majibu ya kishabiki na huna uwezo wa kupembenua mambo afadhali ukae kimya.
 
Magufuli is the Best

Anatupeleka na tumekaribia Nchi ya ahadi


Nikuambie kitu kimoja sifa moja ya Nchi inayotaka kupiga hatua kiuchumi na kimaendeleo
Ni lazima ipambane na Rushwa kwa vitendo pia lazima ikusanye kodi kwa 100%


Serkali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli
Ilianza na hivyo vitu viwili, kwa nidhamu kubwa sana na wamefanikiwa kwa 90%

Ukiangalia Mfumo wa ulipaji kodi uliopo hata Magufuli akistaafu 2025 hata ukija utawala mpya hautapata shida labda taratibu zibadilike

Rais Magufuli anatengeneza vyanzo vya uchumi ambavyo vitabadilisha kabisa maisha ya Mtanzania

Angalia bwawa la umeme likikamilika litainua sana uchumi wa Tanzania

Angalia reli mpya inayojengwa ikikamilika impact ya maendeleo itakavyokuwa

Usisahau kila mwaka zaidi ya wanafunzi million moja wanamaliza shule kutokana na elimu bure wanayopewa na Rais Magufuli

Hii inamaana gani kuanzia 2016 hadi 2025 wanafunzi zaidi milion kumi na tano watwkuwa wamefaidika na elimu bure ya Rais Magufuli

Rais Magufuli ameleta nidhamu maofisini kwa kweli
Sahivi ukienda kwenye maofisi ya mawaziri unskaribishwa tu vizuri na kusikilizwa unaondoka umefurahi

Magufuli amevuka viwango vya ubora, anastahili kuongoza
Alichelewa sana kuja Tanzania, acha atupeleke Nchi ya ahadi
 
Magufuli is the Best

Anatupeleka na tumekaribia Nchi ya ahadi
Hapana mkuu. Acha majibu ya jumla kama tuko kwenye mnada wa samaki ferry. Be specific. Amefanya nini kutupeleka karibu na nchi ya ahadi ambayo unaona hao wengine wasingeweza kufanya?
 
Back
Top Bottom