Katika Hali hii iliyopo, Kwanza inabidi, tuondoe hofu, watalaamu wetu wakae, wajadiri Kwa kina, halafu waje na pendekezo ambalo litakuwa mbadara wa yanayo/yaliyotumika kwenye mataifa mengine,
Kwa sababu gani, Sina utafiti wa kutosha kuhusu nchi mbalimbali zilizochukua uamuzi wa kufungia watu wao, kama ndiyo njia Bora na imeleta matokeo Kwa haraka, Kwa sababu, Leo hii ni Kati ya miezi miwili SASA kwenye nchi kama USA na kwingineko, lakini idadi ya waathirika imekuwa ikipanda kila leo, na wakiwa under lockdown
Janga hili linahitaji itumike akiri kubwa sana ktk nchi zetu hizi za mwishoni kabisa, ukifanya masihara kuamua Jambo Kwa mihemko, unaweza kusababisha janga kingine kubwa zaidi kuliko Corona yenyewe,
Mimi nadhani, kila mtu ifike pahali aanze kumwona mtu mwingine ni kama muuwaji, au jambazi, hivyo akae naye mbali Sana, Tufanye kama hatujuani Kwa muda huu tulionao, na hii ndiyo iwe lockdown yetu, ikiwezekana, fimbo zitembee, ikiwa watu watakuwa wanakaa Kwa karibu karibu, Tusisogeleane Kwa sababu kufanya hivyo ni kama kujiruhusu wewe ufe.
Hili la kujifungia, ni kama imekuwa ni njia yenye mateso halafu haisaidii, lkn labda miji yetu ndiyo ifungwe,hakuna kuvuka kwenda mji mwingine, wa dar ni wa dar Tu, mwanza na Arusha na mikoa mingine iwe hivyo hivyo,