Najua wengi wamempongeza na wanaendelea kutoa pongezi nyingi sana kwa kiongozi wa nchi yetu Mh jemedari Dr John Joseph Magufuli, nami pia nimewiwa, nafsi yangu imeshindwa kujidhuia wala kuridhika kama sitaweza kuandika neno la shukurani hapa.
Mh Rais,wewe ni Baba yetu! wewe ni mlezi wetu na wewe ndiyo dira ya uelekeo wetu katika kila jambo,ama kiuchumi au kijamii.
Nakupa heko na pongezi nyingi sana kwa namna unavyoshughulika na changamoto za ndani ya nchi yetu, bila kujali wachache wanaobeza na kupiga miluzi mithili ya mbwa afukuzwaye kwa lengo la kukupoteza uelekeo lakini umesimama imara, hongera sana.
Mh Rais tumeona na tunaendelea kuona mambo mengi ya maendeleo yaliyotekelezwa na yanayotekelezwa katika kipindi cha awamu yako ya uongozi,tukiachana hata na miradi mikubwa inayoendelea ndani ya nchi yetu juu ya barabara,reli pamoja na nishati lakini kwa sisi tunaoishi maeneo ya vijijini mambo yamebadilika sana, zahanati zetu zimeboreshwa, barabara nyingi saizi zinapitika maana madaraja madogo madogo yamejengwa kwa wingi, zahanati nyingi zimeboreshwa na kuongezewa hadhi kuwa vituo vya afya,shule zetu za kata hakuna michango tena zaidi ya sare ya shule ya mwanafunzi.
Mh Rais, ombi langu kwako ni kuwa ongeza msimamo zaidi katika mambo yenye tija kwa maendeleo yetu,hawa washamba wachache wanaojifanya hawaoni kila kitu ipo siku watajibu tuhuma mbele za Mungu, lakini pia tusingependa kila wakati watutukanie Rais wetu, wanapofanya hivyo washughulikiwe ipasavyo, na basi sikubahatika kuwa kwenye idara ya usalama wangenikoma washamba hawa, tumechoshwa na ushamba wao.
Yaani inafikia mahala wanashangilia watu kupata corona ili wapate cha kuongea huu ni ushamba wa hali ya juu, wanapokamatwa na madawa ya kulevya wanaanzisha propoganda mara kawekewa na mwanamke, huyo mwanamke si demu wake? Kama wana akili kiasi hicho sasa wanashindwa kutambuaje kama watawekewa madawa kwa hiyo wajiepushe? Yaani utoto mtupu!
Mh PIGA KAZI TULIOKO NYUMA YAKO NI WENGI KULIKO KAKIKUNDI KA HAWA WASHAMBA WACHACHE.
Sent using
Jamii Forums mobile app