Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Kweli katuletea heshima. Ndiyo maana hata kitaifa kidogo cha Zambia kimetupiga ban kuingia nchini kwao. Hata Malawi kwa kutudharau watatupiga ban kuingia Malawi
Ndio maana sisi sio Zambia. Tungeweza kuwapiga ban pia nini kunatuzuia.
Solution zao eventually zitarudi kuwa kama zetu. Mhemuko.
 
Tunapata heshima au ndio tunaonekana mandorobo

tyari tushaanza kufungiwa mipaka tushaonekana wapuuzi, cryl kule south juzi ndio alimuona mzee ndorobo kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila mtu anaruhusiwa kuona anavyoona. Watu sasa hivi wanaondoa lock down, obvious hawa nao soon aidha wataondoa au watatamka kisiasa na watu wataendelea kupita. This is Africa not Europe
 
Mtawezaje kuwapiga ban na kipimo hamna?
Nategemea utaenda pande zote kufikikiria hicho unachosema. Tulianza vipi na tumefikaje tulipo. Hivyo, usipojitoa ufahamu utajua kwamba kama tungehitaji maamuzi hayo tungekuwa mbele ya wote wanaofunga leo. Si kipaumbele
 
We mbwa weka mafanikio ya watz sio ya magufuli. Mafanikio ya magufuli yako chato sio tanzania
 
Mbwa hawapo hapa, pole sana. Bado hakuna mbwa anayeshiriki Jamii forum. Hata wewe sio mbwa kwa sababu hatuwezi ongea na mbwa
Mbwa ni yule anayesifia ujinga. Badala ya kuelezea mafaniko ya watz anaelezea mafanikio ya magufuli huu ni ufala wa hali ya juu sana
 
Najua wengi wamempongeza na wanaendelea kutoa pongezi nyingi sana kwa kiongozi wa nchi yetu Mh jemedari Dr John Joseph Magufuli, nami pia nimewiwa, nafsi yangu imeshindwa kujidhuia wala kuridhika kama sitaweza kuandika neno la shukurani hapa.

Mh Rais,wewe ni Baba yetu! wewe ni mlezi wetu na wewe ndiyo dira ya uelekeo wetu katika kila jambo,ama kiuchumi au kijamii.

Nakupa heko na pongezi nyingi sana kwa namna unavyoshughulika na changamoto za ndani ya nchi yetu, bila kujali wachache wanaobeza na kupiga miluzi mithili ya mbwa afukuzwaye kwa lengo la kukupoteza uelekeo lakini umesimama imara, hongera sana.

Mh Rais tumeona na tunaendelea kuona mambo mengi ya maendeleo yaliyotekelezwa na yanayotekelezwa katika kipindi cha awamu yako ya uongozi,tukiachana hata na miradi mikubwa inayoendelea ndani ya nchi yetu juu ya barabara,reli pamoja na nishati lakini kwa sisi tunaoishi maeneo ya vijijini mambo yamebadilika sana, zahanati zetu zimeboreshwa, barabara nyingi saizi zinapitika maana madaraja madogo madogo yamejengwa kwa wingi, zahanati nyingi zimeboreshwa na kuongezewa hadhi kuwa vituo vya afya,shule zetu za kata hakuna michango tena zaidi ya sare ya shule ya mwanafunzi.

Mh Rais, ombi langu kwako ni kuwa ongeza msimamo zaidi katika mambo yenye tija kwa maendeleo yetu,hawa washamba wachache wanaojifanya hawaoni kila kitu ipo siku watajibu tuhuma mbele za Mungu, lakini pia tusingependa kila wakati watutukanie Rais wetu, wanapofanya hivyo washughulikiwe ipasavyo, na basi sikubahatika kuwa kwenye idara ya usalama wangenikoma washamba hawa, tumechoshwa na ushamba wao.

Yaani inafikia mahala wanashangilia watu kupata corona ili wapate cha kuongea huu ni ushamba wa hali ya juu, wanapokamatwa na madawa ya kulevya wanaanzisha propoganda mara kawekewa na mwanamke, huyo mwanamke si demu wake? Kama wana akili kiasi hicho sasa wanashindwa kutambuaje kama watawekewa madawa kwa hiyo wajiepushe? Yaani utoto mtupu!

Mh PIGA KAZI TULIOKO NYUMA YAKO NI WENGI KULIKO KAKIKUNDI KA HAWA WASHAMBA WACHACHE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chini ya Jemedari Mkuu, Mwamba usio tikisika Rais wetu Magufuli nchi yetu imezidi kusonga mbele mbali na kelele nyingi za lockdown lakin tumeendelee kuchapa kazi huku tukichukua tahadhari ya kujikinga na mlipuko wa Covid19.

Wananchi walio wengi haswa wa kipato cha chini na cha kati wana mshukuru sana Rais Magufuli Kwa kuwa Na msimamo wa kutokubaliana Na mawazo au shinikizo la lockdown (yaani watu wote kubaki ndani bila kutoka kufanya shughuli za kila siku) Kwa hakika kama nchi yetu ingetii au kufuatia utaratibu wa lockdown basi idadi ya vifo kutokana na njaa na matukio ya kihalifu yangeongezeka mara dufu, Hongera sana Rais Magufuli, sijui kama tutapata Rais Imara kama Magufuli baada ya mwaka 2025? Sijui!

Hivi sasa tumeanza kuona nchi kadhaa zimeachana Na lockdown Na kuruhusu wananchi wake waendelee na shughuli zao, mfano Ufaransa, Norway, Uingereza nk, Tanzania tuko vizuri sana!

Awamu hii ya 5 ndio nimebaini kuwa kumbe nchi yetu ina uhuru wa kimawazo/kifikra hili limejidhihirisha kwa kauli na Misimamo aliyo ionyesha Rais wetu. Wale wote wanao tumia ugonjwa wa corona kama kete ya kisiasa haswa Kwa dhamira ya kutaka uchaguzi mkuu uahirishwe ili wajipange imekula kwao. Uchaguzi mkuu upo palepale .

Wanasiasa haswa vyama vya upinzani ni vyema mkajipanga kwa sera kuliko kujificha katik agenda ya ugonjwa wa corona, Hadi sasa Tanzania tuko vizuri sana.

Kwa ndugu zangu waislama ambao wapo ktk mfungo mtukufu Na kumi la mwisho hili tusisahau kuiombea nchi yetu Na Rais wetu tuvuke salama ktk kampeni na Uchaguzi mkuu ufanyike kwa salama na Amani.

Mungu ibariki nchi yetu Tanzania na Rais wetu JPM.
 
luirhu,

Wewe bado hujaona vifo na utakapofiwa ndio utaweka siasa zako kando na kuelewa kuwa serikali inacheza na maisha ya watu.
 
Wewe bado hujaona vifo na utakapofiwa ndio utaweka siasa zako kando na kuelewa kuwa serikali inacheza na maisha ya watu.
Katika kupambana an corona inatupasa tukabiliane na ugonjwa Kwa kujikinga na kuzingatia masharti sio kujifungia ndani, tunaambiwa na WHO kuwa tutaendwlea kuishi na corona miezi mingi zaidi, sasa tukae ndani hadi lini! Haiwezekani ila yatupasa tuendelee na shughuli zetu za kutafuta riziki
 
Back
Top Bottom