Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Kuna watu wanasifia kupita kiasi. Hatari za kufanya hivyo ni:-

1. Kumwona yule anayesifiwa kama mungu machoni pa wanaosifu.
Hali hiyo inawavuruga na kuwapunguzia uwezo wa kujitegemea kiakili.

2. Kumfanya yule anayesifiwa kujiona mungu machoni pake mwenyewe.
Hii inamfanya msifiwaji kuamini yuko hapo alipo kwa stahili ya kiungu(divine right) na si kwa michakato ya kawaida ya kibinadamu.

3. Msifiwaji anafikia hatua ya kudhani kuwa ana hatimiliki ya kiungu ya kumiliki maisha na mali zote kwenye himaya yake na kwamba hastahili kupingwa na yeyote kwenye maazimio yake yawe mema au maovu! Na athari za hali hii zitajidhihirisha zaidi kwa wanaoguswa moja kwa moja na shughuli zake za kila siku.

Wasifiaji msimpeleke mwenzenu huko. Hakuna aliyefika huko akabaki salama. Na usalama wenu wenyewe utapungua na kwisha kabisa jinsi mtu wenu anavopanda ngazi za sifa.

Ni maoni tu. Sina nia ya kukirihisha mtu yoyote.
 
4 Julai 2020
Mbeya, Tanzania

Kina Mama Inawalazimu Kusafiri Kilometa 70 kupata Huduma za Afya


VIFO vya MAMA na MTOTO Wananchi Wamlilia RAIS MAGUFULI, -"Tusaidie Tumechanga Mill 102"



WANANCHI wa Kijiji cha Ifupa Wilaya ya Mbeya wamemwomba Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila kufikisha maombi yao kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli ili kuwasaidia ujenzi wa kituo cha Afya.

Source : Global TV Online
 
Magufuli ameendelea kulipa madeni bila kutetereka kabisa kitu ambacho kimewaacha hoi wazungu na kujiuliza huyu binadamu si wa kawaida..

Shirika LA Fedha nalo limeshangazwa kwa kuona uchumi wetu umeshrink kidogo tu na kubakia ukuaji chanya ukilinganisha na baadhi ya nchi ambazo uchumi wake unasinyaa hasi
 
Rais alisema nchi hii ni tajiri, tukapewa na wimbo - "Sisi ni Matajiri". Kwenye mkutano wa SADC tukaona mabango yameandikwa "Matajiri wanakutana", Tukashangilia. Leo Work Bank wanatuambia 'Nyie ni - Lower Middle Income Country - tunashangilia. Sisi ni nani?
 
Magufuli ameendelea kulipa madeni bila kutetereka kabisa kitu ambacho kimewaacha hoi wazungu na kujiuliza huyu binadamu si wa kawaida..

Shirika LA Fedha nalo limeshangazwa kwa kuona uchumi wetu umeshrink kidogo tu na kubakia ukuaji chanya ukilinganisha na baadhi ya nchi ambazo uchumi wake unasinyaa hasi
Tupe Mapato y TRA kwa mwezi Apil, May & June
 
Deni la taifa linazidi kukua Yeye analipa madeni yapi?
 
Wakati Mhe. Rais anakwenda Kujiandaa kuapishwa kwa Mara ya pili mwaka huu baada ya Ushindi wa Kishindo, ukweli ni kwamba Rais Magufuli ni Mhe. Mwenye mvuto na anapendwa na Watanzania wote. Mhe. Magufuli Anaongoza nchi kwa Ubunifu na Uzalendo wa kipekee na hotuba zake zimekuwa zenye mvuto mkubwa sana; kila mkoa akipita basi hali ya huo mkoa huwa shwari na furaha mioyoni mwa Watanzania wengi hurejea.

Kwa sasa hakuna kitu kinacholiliwa kama hotuba zake na ziara zake kila Mkoa.

Hata Wapinzani wenyewe huwa wanalilia hotuba yake. Nadhani mnakumbuka kipindi cha Corona walikuwa wanamsema weee kinafiki kumbe walikuwa wanahamu na hotuba yake tu. Huu ndio ukweli Mhe. Rais hotuba yake ni faraja tosha kwa Watanzania na Dunia nzima.

Kumbuka hotuba yake akiwa Chato aliweza kuongea hotuba fupi tu ambayo Vyombo vya Habari Dunia nzima viliijadili hotuba yake ya Chuma Mhe. Dr.Magufuli mtaalamu wa Kemia. Kuna mambo mengi sana lakini kwa Leo niishie hapa.

Watanzania Tujivunie Mhe. Rais wetu na tuendelee kumuombea.

Mimi nitaendelea kumuombea Mhe Rais wetu kipenzi cha Watanzania.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu Mlinde Rais Magufuli.

#Team Magufuli.
#JPM Mitano Tano.
#Team Chemistry.
 
Back
Top Bottom