Wakati Mhe. Rais anakwenda Kujiandaa kuapishwa kwa Mara ya pili mwaka huu baada ya Ushindi wa Kishindo, ukweli ni kwamba Rais Magufuli ni Mhe. Mwenye mvuto na anapendwa na Watanzania wote. Mhe. Magufuli Anaongoza nchi kwa Ubunifu na Uzalendo wa kipekee na hotuba zake zimekuwa zenye mvuto mkubwa sana; kila mkoa akipita basi hali ya huo mkoa huwa shwari na furaha mioyoni mwa Watanzania wengi hurejea.
Kwa sasa hakuna kitu kinacholiliwa kama hotuba zake na ziara zake kila Mkoa.
Hata Wapinzani wenyewe huwa wanalilia hotuba yake. Nadhani mnakumbuka kipindi cha Corona walikuwa wanamsema weee kinafiki kumbe walikuwa wanahamu na hotuba yake tu. Huu ndio ukweli Mhe. Rais hotuba yake ni faraja tosha kwa Watanzania na Dunia nzima.
Kumbuka hotuba yake akiwa Chato aliweza kuongea hotuba fupi tu ambayo Vyombo vya Habari Dunia nzima viliijadili hotuba yake ya Chuma Mhe. Dr.Magufuli mtaalamu wa Kemia. Kuna mambo mengi sana lakini kwa Leo niishie hapa.
Watanzania Tujivunie Mhe. Rais wetu na tuendelee kumuombea.
Mimi nitaendelea kumuombea Mhe Rais wetu kipenzi cha Watanzania.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu Mlinde Rais Magufuli.
#Team Magufuli.
#JPM Mitano Tano.
#Team Chemistry.