Watanzania Wazalendo wamemteua Ndugu John Joseph Pombe Magufuli kuwa #MzalendoNamba01 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Magufuli ni Mzalendo Namba 1 wa Chato na sio wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ni kutokana na ukweli huo ndio maana:-
1. Alipoingia madarakani alikuta bohari za madawa zipo kwenye kanda tu lakini yeye kuingia na kuingia, akaanza kwa kujenga bohari ya madawa Chato, na hatimae Chato kuwa kijiji cha kwanza Tanzania kuwa na bohari ya madawa!
Magufuli alifanya hayo katika kipindi ambacho hata miji mikubwa kama Morogoro, Iringa, Tabora, na mingine kadhaa ikiwa haina bohari ya madawa!
2. Alipoingia madarakani alikuta viwanja vya ndege vya kimataifa vipo kwenye miji mikubwa tu tena ambayo ipo kwenye strategic location, lakini yeye kuingia na kuingia akajenga uwanja wa ndege wa kimataifa Chato na hatimae Chato kuwa kijiji cha kwanza Tanzania kama sio East Afrika kuwa na uwanja wa ndege wa kimataifa kwa ajili ya kuhudumia chato!
3. Alipoingia madarakani alikuta mbuga za wenyewe ambazo hazikuanzishwa na marais wa maeneo hayo lakini ile kuingia na kuingia tu, Magufuli akabadilisha hifadhi ya taifa na kuifanya kuwa mbuga ya wanyama huko huko Chato!!
Lakini kwa kuwa hifadhi hiyo haikuwa na sifa ya kuwa mbuga ya wanyama, Magufuli akalazimika kuhamisha wanyama kutoka sehemu zingine za nchi na kuwapeleka kwenye mbuga iliyopo kijijini kwake, na kwa mara nyingine kuandika historia ya kuwa rais wa kwanza Tanzania kukamata wanyama kutoka mbuga moja na kuwapeleka kwenye mbuga aliyojianzishia nyumbani kwao!
4. Alipoingia madarakani alikuta hospitali za rufaa za kanda zipo kwenye makao makuu ya kanda pekee ili kuhudumia watu wa kanda mzima lakini yeye kuingia na kuingia tu, hospitali yake ya kwanza ya kanda kuijenga alijenga Chato, na kwa mara nyingine Chato kuwa ndio kijiji cha kwanza Tanzania kuwa na hospitali ya rufaa ya kanda!!
Kwa kumbushana tu, Chato ipo pembezoni kabisa mwa mkoa wa Geita, na kwa maana nyingine, wananchi wa Geita wa maeneo mengine wanatakiwa kusafiri maili kadhaa kwenda Chato kupata huduma ya matibabu!
Ni kutokana na sababu hizo 4, ingawaje pia zipo nyingine kadhaa, ndo maana sina japo punje ya shaka kutangaza kwamba Magufuli sio Mzalendo No.1 Tanzania bali ana sifa zote za kuwa Mzalendo No. 1 kijijini kwao Chato!!