Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Binafsi nakushukuru sana kwa niaba ya Wananchi wenzangu wa Mwanza. Wakati wa utawala wa JK umeme hapa Mwanza ulikuwa kama janga la Taifa wakisingizia mara ukame na sababu zisizo na msingi kabisa. Leo hii hapa Mwanza matatizo ya umeme yanataka kuwa historia.

Sasa yapata majuma mawili mfululizo umeme haujakatika na tunaendesha sana shughuli zetu kama kawaida ukichukulia kuwa kwa karne ya sasa umeme ndiyo kila kitu. Mimi najiuliza utawala wa JK kulikuwa na matatizo gani wakati hakuna mabadiliko kwenye miundo mbinu ya umeme.

TUNAKUSHUKURU SANA MHE.MAGUFULI
 
Tumekutuma lini? Mbona hayo matatizo bado yapo hata kama sio kama wakati ule? Usije kuwa unaishi kwenye line ya Umeme unaokwenda hospital kuu ukadhani in wote.
Muhimu jiepushe na huo uongo wa "kwaniaba ya wakazi wa Mwanza"
 
Alishasema
Enough is enough tumeshachezewa sana sasa hivi ukibainika unahujumu hatusubiri taratibu kukuweka nje ya ofisi ni unawekwa pembeni ndipo taratibu zinaendelea!
 
Koryo ulitakiwa uende magogoni uombe kuonana Na mh. Umpe shukrani zako, Na sio hapa,
 
As a Tanzanian studying outside Tanzania, i have been meeting with different students coming from different part of Africa and most of them have been speaking highly about our current leadership. By leadership i mean the leadership of his HE. Dkt Magufuli phase, in person i have never felt so proud to being a Tanzanian as i have never felt ever before. I would like to quote one of my friend from South Africa what he had to say about HE. Dkt Magufuli " As a south African i cannot resist showing my jealousy for Tanzania's president. His dedication, at a personal and professional level, is exemplary for the rest of African leaders. Africa needs a new type of leaders, the ones to free its people to promote economic promotion and better standard of living for all. As a strong allied of South Africa i hope you become an example for all all of us, future leaders, we appreciate your dedication and love for a functional Africa. We support what you stand for in South Africa". We as Tanzanians we need to support and protect our president for the journey he has started to take Tanzania to where we are suppose to be, lets unite and value whats ours instead of fighting it. Viva my president

May God protect you and shower you with much of his blessings.
 
Wewe msukule na picha ya "mungu"...wako mweupe Triump kwenye avatar...vipi hujaona waafrika...au ndo unafurahi kutawaliwa naye.
Kwi kwi kwi kwi kwi!! Aisee umenichekesha sana kwa hiyo mitusi. Haya ngoja niweke picha ya Shein ama Mseveni ufurahi sawa mrembo!?
 
Kwi kwi kwi kwi kwi!! Aisee umenichekesha sana kwa hiyo mitusi. Haya ngoja niweke picha ya Shein ama Mseveni ufurahi sawa mrembo!?
Bange hutengeneza misukule hatari sana na ipo siku mtawala nyama hao viongozi wenu
 
Thats how we felt over 40 years ago, during the Mwalimu era.

Ndugu unashangaa huyo mtu mmoja wakati Ewura wanaomba kupunguza bei ya umeme kwetu sisi watanzania kwa kutumia kiingereza? Nilichojifunza katika nchi hii serekali inapotaka kufanya jambo lake ambalo inaona wananchi watapiga kelele utaona wanaandika kiingereza. Cha kuchekesha hao wanaoandika hayo mambo kwa kiingereza ukiwaambia wasimame hadharani watete hayo mambo yao kwa kiingereza unaweza ukatapika. Mwacheni huyo mtu kwani hii ndio tabia iliyojengeka hata kwenye taasisi zetu za umma.
 
Kwani ukiandika kiswahili hatutajua unasoma ng'ambo!? Jitambue ewe mtumwa wa ukoloni mamboleo.
Dah...huu ndio wivu wa kijinga! Omba tafsiri sio mbaya, maana Kiswahili na Kiingereza zote ni lugha za Taifa
 
Perception ya Magufuli katika nchi zinazotuzunguka ni highly positive, wasiwasi wangu ni je ataweza ku-liveup to such perception and expectations?
 
hivi kuficha ujinga wako umeshindwa kabisa??dah!
Ebu toa kwanA hiyo picha ya avatar yako ya Donald Trump.
Mjinga ni huyo dada yako aliyetekwa na ukoloni mamboleo. Huwezi leta habari ya kumsifu raisi wetu mwenye mapenzi mema na wananchi wake kwa lugha ya Kikoloni. Angalia hata Facebook page ya Zuma uone Wasouth tena waliokaa na wazungu karne kwa karne wakiposti kwa lugha ya kwao. Trump huyo ndo baba wa majipu yote ya Africa na namkubali kama ninavyomkubari Magufuri, Arsenal,Barca na Yanga. Huyo hata ukifuatilia anakosoma hawezi tumia jina la asili yake. Nakupa changamoto wewe popoma. Tafuta majina ya Wasouth ama Wabotswana uone kama utapata jina la Kikoloni huko. Unaweza kuta kati ya 10 mmoja ndo anatumia jina la kikoloni. Jitambue
 
Aah Mshana jr, usimyime sifa yake rais wetu
Simnyimi la hasha lakini huko tuendako tukakutana na hali ngumu sana hasa yeye kwakuwa vita anayopigana ni yake binafsi na hana support ya jeshi ya kisiasa na kimkakati (ccm and organs)kashfa za TRA kashfa za meter za mafuta na huko kwingine alikopita, mgomo wa chini kwa chini wa mawaziri wake kugoma/kupuuzia/kukataa kurudisha fomu za maadili mpaka walipochimbwa mkwara si dalili njema hata kidogo
Kuna majipu ya maliasili mitandao ya simu nk yanakuja utashuhudia mengi huko....ishu ya sukari umeona ilivyoleta sintofahamu kubwa? Wasaidizi wake ni chui waliojivika ngozi ya kondoo na shida itaanzia hapo
 
Back
Top Bottom