Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

He is nothing without democracy, empty Bottle,
 
He is nothing without democracy, empty Bottle,
Jamani Magufuri ameonyesha dira,tusibeze ndugu zangu. Nchi ilikuwa ishakuwa danguro,ni muda wa kumuunga mkono na kumuombea kwa mungu sijampigia kura hata ukiangalia posti zangu lkn kwa siku hizi chache alizokaa nimeamua kuweka siasa pembeni. Naamini Magufuri alikuwa na mzigo moyoni kwa namna Watanzania wanavyokosa huduma huku watu wakitanua tu watakavyo.
 
Kwa moyo wa dhati nawapongeza sana rais wetu Magufuli na WAZIRI MKUU Majaliwa kwa kufufua matumaini yetu watanzania!

Viongozi walikuwa wanaona nafasi zao ni za kujineemesha wenyewe wakiwemo wa ngazi za juu kabisa.

OMBI langu kwenu ni kwamba msikatishwe tamaa na maneno ya kejeli toka kwa watu ambao lengo lao ni kuwavunja moyo! Kazi yao ni kukosoa tu! Watu hao ni wachache sana lakini mamilioni ya watanzania tumshukuru sana Mungu kwa kutupa viongozi wazuri wenye nia ya dhati ya kuwahudumia wananchi kwa kuwatatulia kero zao!

Niwaombe watanzania wenzangu tuungane kuwakemea wote wanaowakejeli viongozi wetu. Nia ya viongozi wetu ni safi. Kwa hiyo katika harakati za kutuhudumia hata ikitokea wakakosea kwa namna moja au nyingine tuwasamehe kwa moyo mweupe na tuwatie moyo maana ni kwa nia njema!
Kambi ya mafisadi na majipu tarajiwa ndio wako bize kwenye mitandao ya kijamii kuwakejeli viongozi wetu ili kuwavunja moyo na kuwakatisha taamaa. Chonde chonde Magufuli usikate tamaa! Majaliwa usikate tamaa! Songa mbele! We are very proud of you!

Dunia itatushangaa sana tusipoweza kufurahia huu uongozi wa sasa ambao ni adimu sana chini ya jua! Binafsi namshukuru sana Mungu kwa kujibu maombi ya watanzania waliokuwa wamekandamizwa na ufisadi kwa miongo kadhaa na kutuletea kiongozi shujaa asiyeogopa sura ya MTU! Hapa kazi tu! Mafisadi wanajiharishia!
 
Namkubali Magufuli, lakini its too early kumsifia sana

Kuna mambo anatoa amri lakini hakuna ufuatiliaji, kama suala la safari za nje bado lipo sana, suala la ukusanyaji kodi limerudi palepale anakusanya 1.04Tillion, wakati JK alikuwa anakusanya 950/990Billion tofauti ni ndogo sana kuliko nguvu iliyotumika

meaning bado watu wanaendelea kula kama mwanzo, hakuna ufuatiliaji!! the same old story
 
Sasa bado kitu kimoja kawatafute watoto wao uwafunge kamba za viatu. Usisahau kuwabeba hadharani
 

Unajua ugonjwa ukisha kua sugu huwezi ukatibu kwa dozi mmoja ya antibiotic au dawa inayo stahili. Ugonjwa utachukua mda mrefu sasa ufisadi na uwizi wa hapa TZ ni kama ugonjwa sugu.
Watanzania wengi wanafikiri kwamba raisi akisema kutakua na mabadiliki basi mabadiliko hayo yatatokea kwa mara mmoja.
Watanzania wengi ni wavivu wakusoma lakini mahodari wa kuandika na kulalamikak hawasomi jinsi nchi zilizo endelea zilipitia changamoto gani hadi kupata maendeleo.
Hawajiulizi je wenyewe wamefanya nini ili kuleta maendeleo. Hata kuomba risiti wanashindwa wanaona haina maana.
Tunatoa rushwa wenyewe kila siku. Ukitaka leseni tuna tanguliza rushwa. Sasa hapo kutakua na maendeleo gani? Na pia tunashabikia siasa kama tunavyo shabikia mpira.
 
Sasa bado kitu kimoja kawatafute watoto wao uwafunge kamba za viatu. Usisahau kuwabeba hadharani
Hivi kinachokufanya uwe na chuki kiasi hiki kwa viongozi wetu ni nini? Kuna ubaya gani kumsifia kiongozi anayefanya vizuri?
Wewe naona si bure bila shaka ni mnufaika wa mfumo wa kifisadi ambao mheshimiwa Magufuli ameamua kuutumbua majipu!
Kama RAIA na marais wa mataifa mengine wanamsifia Magufuli, wewe ni mtanzania sampuli IPI usiweze kuona mazuri anayowafanyia watanzania?
Watu wa aina yako mko wachache na msipoamua kubadilika afadhali tafuteni nchi yenu inayoendekeza ufisadi!
Mmefisadi sana miongo mingi na bado MNA njaa ya kufisadi! Poleni! Mungu ameikumbuka nchi yetu na ametupa kiongozi shupavu! Ufisadi na mafisadi kafieni mbali! Mmekula wala hakuna dalili kuwa mnaweza kushiba! Poleni! Dhambi haishibishi Bali inatumikisha! Ufisadi ni dhambi na watumwa wa dhambi hii utawajua tu!
 
Dunia itatushangaa sana tusipoweza kufurahia huu uongozi wa sasa ambao ni adimu sana chini ya jua
kinachoendelea sasa hiv ni drama kutokana na sifa znazomwagwa........matumaini yanakujaje ikiwa mikataba mibovu ya madini,gas,ujangili umewashinda,hajira no soln,.kubana haki za wananchi......matumaini yepi mkuu uliyonayo???
tusisifie2 inapobidi kukuksoa tukosoe......ili wafanye kaz wakijua watu wanafatilia...............wawe naweledi.....
na kujali raia maskini saaana
ila Mungu awasaidie viongoz hawa wawe wabunifu na wawe wacha Mungu....wawe na uongoz bora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…