Burungutu la pesa
Senior Member
- Feb 21, 2015
- 117
- 32
Vyama vingi vifutwe?Hakuna haja ya kubadili chama, nchi hii inahitaji head of state shupavu....
Nilimsikia Mh JK akisema anaondoka yeye mpole na sasa kudai ametuletea (sijui kwa mapenzi yake au ilibidi tu) Rais Mkali. Lakini ni kweli katika kipindi cha uongozi wake tumeshuhudia upole wake wa kushangaza kwenye maeneo mengi kama EPA, ESCROW, RICHMOND, UJANGILI hadi wa kupakis Twiga wetu waliohai kuelekea uarabuni.
Hebu fikiri. Magufuli hajaanza kuzalisha chochote lakini ukali wake tu, MRI imeanza kufanya kazi Muhimbili, Kwa ukali wake tu sherehe imetumia Mil 15 badala ya milioni 200 na zaidi. Na sasa tunasherehekea upatikanaji wa vitanda vya wagonjwa Muhimbili.
Vipi Rais wetu akiamua kupeleka hasira zake ESCROW, na kurejesha japo nusu ya zile Bil 300? si tutasahau ukosefu wa dawa mahospitalini? au wagonjwa kulala chini?
Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi hii tumuombee Rais wetu hasira zaidi kwenye upuuzi uliotuweka hapa tulipo. Tusisahau pia kumuombea ulinzi wa Mola wetu, maana sina uhakika kama wale viongozi wetu "wapole" wanafurahia Hasira za Rais wetu.
kama chaina,Vyama vingi vifutwe?
Kabisakabisa.Vyama vingi vifutwe?
Mimi xaxa naishi kwa amani kwani mungu ametuletea mtu sahihi nahatimaye naamini atashinda kwani yeyote afanyaye mazuri mungu humuongoza. Kazana baba kwan Taifa letu linakuhitaji
Bahati mbaya CCM hayupo, na hatakuwepo!!Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.
Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!
Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!
Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.
This time Tanzanians need a person of Kagame calibre to order things!. Mazoea sasa bhaaaas na kwamba Hapa kaaaaaaazi tu!