Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Hakika naanza kuona taifa jipya la Tanzania baada ya kazi kuanza, naona jicho la tatu la wote waliopendekeza na kumpigia kura Rais John P. Magufuli.

Bila ya kuwepo kwa hatua ambazo Rais Magufuli anazichukua.....tusingeanza kuhisi mabadiliko.ila k, a sasa kazi zimeanza kuonekana.

Hongereni mliooona mbali kiasi hicho.
 
Watanzania wengi ni watu wa KUJAWA na matumaini haraka sana bila kufanya utafiti, ni watu wa KUSAHAU masuala ya msingi haraka sana(hali hii imewapa fursa wanasiasa kuendesha nchi kwa matukio), ni watu wa KULALAMIKA haraka sana na pia ni watu wa KULAUMU haraka sana.

Wanasiasa wanajua nini tunataka ambacho kwao wao kwao wakikitoa HAKIWAATHIRI, wanajua kwamba wakikupa mamlaka wewe utawaadhibu, wanajua kila SAA na DAKIKA kuwa tatizo ni UJI na SIO UNGA.

Lakini ukiwaambia unataka UNGA upike uji wewe mwenyewe, hawakupi ila haraka sana wanakuletea uji tena mtamu wenye 'karanga na mchele'.

Ukijisahau kudai UNGA ili uwe unapika uji unaoutaka wewe, HAWAKUKUMBUSHI, tena hufurahia na kujitangaza pale wanapoona UNANENEPA ili hali wanajua siku za usoni HUTAKUWA na UNGA na wakati huo watakuwa wamestaafu.

Mimi sio miongoni mwa WATANZANIA wanaolilia UJI na kushangilia pindi wanapopewa na KUSAHAU kudai UNGA kwa ajili ya kesho.

Nitasimama IMARA kudai UNGA, najua UJI ni sehemu ndogo ya kesho yangu.

Kusahau haraka haraka kudai UNGA na kuchelekelea UJI tu NI HATARI SANA, siku ukiukosa uji kwa sababu hukudai MISINGI YA KUUPATA UNGA, usimlaumu MTU!!

-Namalizia kwa kusema kuwa Watanzania Kupewa UNGA kuanze kwa kupata KATIBA MPYA.
 
Nchi hii imejaa mbulumbulu wengi mpaka natamani niondoke! Mijitu haitaki vitu vya msingi vifanyike wanakimbilua UJI kama ulivyosema! Sasa hivi kutokana na propaganda za media za huyu jamaa mpenda sifa, watu ukiwaambia tutafute katiba kwanza utaona mijitu inaingia mitini imesharidhika na story za vitanda vya muhimbiri, sijui na safari za nje! Ni ujinga wa hali ya juu kushabikia vitu vidogo kama hivi kwa nchi yenye miaka 50 ya uhuru! Maendeleo yanahitaji misingi mizuri ikiwemo katiba nzuri itakayomlazimisha kila anayekuwa Rais wetu kutenda yale ya msingi!

Tataizo la nvhi hii ni elimu na ndiyo maana hawadhubutu kutoa elimu bure mpaka vyuo vikuu maana wasomi wakiongezeka yote haya yanakuwa ni historia!
 
Ni kweli mkuu, tumuombee sana rais wetu JPM kwani viongozi wapole ndo wengi zaidi
 
Ingawa hujaandika mada yako vzr ila una point kwa mbaali! The only problem nilionalo n kuwa hujui tofauti ya uji na unga! Kiukweli mwananchi wa chini anachohitaji sio CCM/UKAWA anachohitaji n maisha mazuri meaning barabara nzuri mpaka mlangoni kwake, shule na elim nzuri kwa wanae,hospital na huduma zake ziwe za viwango ..... so either hivo vinaletwa na ukawa/ccm we dont care!
Ndo maana pamoja na mapungufu yote ya serikali (chama tawala) tunahitaji wabadala waliotayar! Ninapoona wapinzani wakiwa ktk hali ngumu zaidi napata na mashaka zaidi na kesho ya watanzania wengi zaidi, Manake kwa njaa ya madaraka waliyonayi wanaweza wakatuuza anytime!
Cha kufanya nn ss wananchi tuweke vyama pemben tupitishe mgombea ambaye anajua maslahi tunayoyahitaji na ambaye atakuwa yuko tayar kutupigania kwa ajili ya shida zetu na sio shida zake!
 
Mkwere alikuwa anacheka cheka,majizo yanajichotea,hebu cheki mkutano jumuia ya madola wanaenda hamsini,hapo Magufuli kawaotea,Je,kipindi cha Mkwere ilikuaje?
 
Nilimsikia Mh JK akisema anaondoka yeye mpole na sasa kudai ametuletea (sijui kwa mapenzi yake au ilibidi tu) Rais Mkali. Lakini ni kweli katika kipindi cha uongozi wake tumeshuhudia upole wake wa kushangaza kwenye maeneo mengi kama EPA, ESCROW, RICHMOND, UJANGILI hadi wa kupakis Twiga wetu waliohai kuelekea uarabuni.

Hebu fikiri. Magufuli hajaanza kuzalisha chochote lakini ukali wake tu, MRI imeanza kufanya kazi Muhimbili, Kwa ukali wake tu sherehe imetumia Mil 15 badala ya milioni 200 na zaidi. Na sasa tunasherehekea upatikanaji wa vitanda vya wagonjwa Muhimbili.

Vipi Rais wetu akiamua kupeleka hasira zake ESCROW, na kurejesha japo nusu ya zile Bil 300? si tutasahau ukosefu wa dawa mahospitalini? au wagonjwa kulala chini?

Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi hii tumuombee Rais wetu hasira zaidi kwenye upuuzi uliotuweka hapa tulipo. Tusisahau pia kumuombea ulinzi wa Mola wetu, maana sina uhakika kama wale viongozi wetu "wapole" wanafurahia Hasira za Rais wetu.

Pamoja nawe mkuu
 
Bado nasubiri, mpk nitakapoona sh ya tz imekuwa 500 kwa dola 1. Au shilingi ibaki hapo lakn tuwe na maviwanda yanayotengeneza bidha bora kuliko (Watz wenye akili mtakuwa mmeelewa kuhusu kanuni ya import na export economy).
 
WE LOVEEEEE YOUUUUUUU OUR DEAR PRESIDENT! tulitamani kuwa na kiongozi wa kuwasimulia watoto wetu miaka hiyooo.at last we have our maghufuli. we realy love you mr president.
 
Mimi xaxa naishi kwa amani kwani mungu ametuletea mtu sahihi nahatimaye naamini atashinda kwani yeyote afanyaye mazuri mungu humuongoza. Kazana baba kwan Taifa letu linakuhitaji

Kweli kabisa mkuu ila acha kuandika xaxa....andika tuu sasa inapendeza sana. Thanks
 
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.

This time Tanzanians need a person of Kagame calibre to order things!. Mazoea sasa bhaaaas na kwamba Hapa kaaaaaaazi tu!
Bahati mbaya CCM hayupo, na hatakuwepo!!
 
Back
Top Bottom