Mwandishi Mwingereza aitwaye Lewis Carroll aliwahi kusema, ''If you don't know where you are going, any road will get you there''.
Wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu, tuliwasikia UKAWA wakimponda mgombea Urais wa CCM kama hana lolote kwa sababu CCM ni ile ile. Kuna wengine walidiriki kusema CCM imeishiwa pumzi na iwekwe kando. Wengine wakasema kama CCM ni kitanda chenye kunguni kama Dk. Magufuli anavyosema, basi wao hawataki kuhangaika kuwauwa kunguni bali watakichoma moto na kununua kitanda kingine.
UKAWA walicheka na kumdhihaki Rais Magufuli aliposema amepania/kudhamiria kuleta mabadiliko bora pindi atakapoingia madarakani kwa kubana matumizi ya serikali, kuongeza mapato ya serikali, kuboresha mfumo wa utendaji na ufanisi, kupitia kodi na ushuru unaowaumiza wakulima, wafugaji na wavuvi, kupitia upya baadhi ya sheria zinazoleta kero kubwa kwa wananchi, kuunda serikali ndogo, kupunguza au kumaliza kero za watumishi wa umma na kupendekeza muundo wa kitaasisi ili kutekeleza kwa ufanisi ahadi zake.
Two weeks down the line, UKAWA kwa sasa wameanza ''kudandia treni'' ya Rais Magufuli kwa mbele wakati huo huo baadhi yao hawajatuambia kama wanamtambua ni Rais wa Tanzania.
Eti wanadai wameanza kumkubali Rais Magufuli kwa sababu ameanza kutimiza Ilani ya UKAWA! Wamesahau ni wiki mbili zilizopita walikuwa wanasema Rais Magufuli hana lolote jipya katika mchango wa mabadiliko bora nchini. Kuna wengine kwa sasa watadai Rais Magufuli ni UKAWA. Wanachofanya kwa sasa ni kutaka kuhalalisha hii dhana ya kuitwa nyumbu na bendera fuata upepo!
Kabla ya viongozi wa UKAWA kuanza 'kudandia treni' ya Rais Magufuli kwa mbele, lazima wawaombe radhi Watanzania kwa kutaka kuliangamiza taifa kupitia mgombea wao wa Urais wa Tanzania ambaye walituletea na kuanza kutuuzia kwenye gunia wakati wanafahamu ni mra rushwa, fisadi na hafai kuwa Rais wa Tanzania.
Mtu muungwana ni yule anayeomba radhi na pia taifa la waungwana ni lile linalosamehe baada ya kuombwa radhi.
UKAWA kabla hamjaungana na juhudi za Rais Magufuli, lazima muombe radhi kwa wapiga kura wengi, otherwise, endeleeni kusimama na Lowassa mwenye mabadiliko fake yakisaidiwa na Ilani yake ya Uchaguzi yenye vipao mbele vitatu, 1)Elimu, 2)Elimu na 3)Elimu.
Kwa wale wanaoamini uwepo wa Mwenyezi Mungu, kwa sasa wanasema Mwenyezi Mungu bado analipenda Taifa letu kwa kutuletea Rais Magufuli.