Uongo mtupu! Magufuli mkumbatia Mafisadi hadi leo hii yuko kimya kuhusu ufisadi wa MV Ufisadi ya bilioni 8 ambayo haikutembea hata wiki mbili sasa iko juu ya mawe. Magufuli anayekwepa na kuogopa kutia neno lolote kuhusu wizi mkubwa wa Escrow bilioni 321 zilizokwapuliwa na mwizi na fisadi Rugemarila kwa kushirikiana na Kikwete aliyebariki wizi ule kwa kudai kwamba "pesa zile hazikuwa za umma." Magufuli ambaye yuko kimya kuhusu hukumu ya Tanesco kutakiwa kulipa $148 million. Magufuli ambaye alikuwa mstari wa mbele kuzuia ripoti ya tume ya Wabunge kuhusu ufisadi wa Lugumi wa $37 billion. Magufuli ambaye nchi imeshamshinda anabaki kwenda kuonea wafanyakazi wa Bandari na JKN Airport.
Magufuli mwenye roho mbaya sana ambaye ni wiki ya tano sasa hajatia mguu kule Kagera kwenda kuwafariji wahanga wa tetemeko. Magufuli ambaye amekusanya zaidi ya bilioni 15 lakini hataki kutwambia kiasi halisi kilichokusanywa na ni akina nani waliochangia huku akiendelea kuzishikilia pesa hizo wakati wahanga wakiendelea kulala nje, kutokuwa na chakula wala maji safi kwa wiki tano sasa. Acheni kutufanya Watanzania majuha bhana! Eti anajenga nchi! hakuna ajira zaidi ya mwaka sasa, promotion kazuia zaidi ya mwaka sasa, uchumi wa nchi unayumba. Kwa kipindi cha miezi 8 tu tangu aingie madarakani amepaisha deni la Taifa kwa 55.8% sawa na trilioni 24 na hivyo kuliongeza deni la Taifa kutoka 43 trillion hadi 67 trillion na bado anataka kuendelea kukopa kwa speed ya kutisha! Uongo wenu pelekeni mtaa wa Lumumba.