Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Twiga wa Asia(Asian Tigers)[emoji15] [emoji15] [emoji15]

Hii bangi niliovuta leo sijui ya Kagera imenifanya nipate tetemeko la lugha.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Uongo mtupu! Magufuli mkumbatia Mafisadi hadi leo hii yuko kimya kuhusu ufisadi wa MV Ufisadi ya bilioni 8 ambayo haikutembea hata wiki mbili sasa iko juu ya mawe. Magufuli anayekwepa na kuogopa kutia neno lolote kuhusu wizi mkubwa wa Escrow bilioni 321 zilizokwapuliwa na mwizi na fisadi Rugemarila kwa kushirikiana na Kikwete aliyebariki wizi ule kwa kudai kwamba "pesa zile hazikuwa za umma." Magufuli ambaye yuko kimya kuhusu hukumu ya Tanesco kutakiwa kulipa $148 million. Magufuli ambaye alikuwa mstari wa mbele kuzuia ripoti ya tume ya Wabunge kuhusu ufisadi wa Lugumi wa $37 billion. Magufuli ambaye nchi imeshamshinda anabaki kwenda kuonea wafanyakazi wa Bandari na JKN Airport.

Magufuli mwenye roho mbaya sana ambaye ni wiki ya tano sasa hajatia mguu kule Kagera kwenda kuwafariji wahanga wa tetemeko. Magufuli ambaye amekusanya zaidi ya bilioni 15 lakini hataki kutwambia kiasi halisi kilichokusanywa na ni akina nani waliochangia huku akiendelea kuzishikilia pesa hizo wakati wahanga wakiendelea kulala nje, kutokuwa na chakula wala maji safi kwa wiki tano sasa. Acheni kutufanya Watanzania majuha bhana! Eti anajenga nchi! hakuna ajira zaidi ya mwaka sasa, promotion kazuia zaidi ya mwaka sasa, uchumi wa nchi unayumba. Kwa kipindi cha miezi 8 tu tangu aingie madarakani amepaisha deni la Taifa kwa 55.8% sawa na trilioni 24 na hivyo kuliongeza deni la Taifa kutoka 43 trillion hadi 67 trillion na bado anataka kuendelea kukopa kwa speed ya kutisha! Uongo wenu pelekeni mtaa wa Lumumba.
Ujenzi wa Nyumba Bukoba kwa kipindi hiki bado mpaka tetemeko liishe. Nyumba zitabomoka tena. Subiri miezi mitatu.
 
Tumpe ushirikiano. Jamaa anatupeleka pazuri sana. Sipati picha miezi 10 Ndege mbili..ina maana miaka 10 ndege 22
Very poor conclusion!! Ni mpango upi ambao unaonyesha ununuzi wa ndege mbili kila mwaka?
Be objective.
 
Mheshimiwa raid akienda Kagera ndio Nyumba zitainuka zenyewe nn maana ya Kuwait's NA mawaziri,raisi amefika kupitia hao NA bado anafuatilia kinachoendelea kule.Tunaolaumu tumechangia nini Kagera toa boriti kwako ndio uone kibanzi kwa mwenzio hata raia wa kawaida anamwakilisha raisi timiza wajibu wako kama raia .Acha kulaumu NA kutafuta dosari tujenge nchi yetu.
 
Asian Tiger au East African kitten? Don't count you chickens before they hatch, people!
 
Kabla ya uchaguzi wa oct 25 watanzania wengi walitaka kiongozi atakae weza kuleta mabadiliko kwenye nchi yetu,sio mabadiliko tu pia walitaka kiongozi mwenye maamuzi magumu na yaliyo sahihi.Hivi watanzania hayo mabadiliko tuliyokua tunayataka unafikiri ni nani yangemgusa zaidi ya sisi wenyewe wananchi
Leo hii mkulu anafanya mabadiliko mbalimbali kwenye system lakini hao hao watanzia waliokuwa wanataka mabadiliko wanamchukia mkulu
Mkulu anafanya maamuzi magumu lakini hao hao watanzania wanamuita dikteta
Ni wazi kwamba haya mabadiliko yatamgusa kila mmoja kinachotakiwa ni sisi watanzania kukubali kubadilika ili nchi isonge mbele,na tuumpe muda mkulu maana kuna mambo mengi yalikua yameoza inabidi afanye mabadiliko kwanza ili nchi iende mbele.......na tusimuukumu ndani ya mwaka mmoja tusubiri paka 2020 ndo tuanze kumuukumu
 
Kwa mwendo wa serikali ya Dr Jpm ipo siku kila post ya jamii forum itakuwa ni ya kumpongeza Jpm
 
We jamaa leo post zako zina walakini Kuna moja umesema ETI jamii forum haipo salama 100 post yenyewe fupi fupi hata haijadiliki.. Rekebisha Hilo swala usiwe na haraka Sana tulia upange hoja KUMBUKA humu wapo watu WENYE uelewa utasaidiwa Sana ukiwa na nidhamu kwenye ku post
 
We jamaa leo post zako zina walakini Kuna moja umesema ETI jamii forum haipo salama 100 post yenyewe fupi fupi hata haijadiliki.. Rekebisha Hilo swala usiwe na haraka Sana tulia upange hoja KUMBUKA humu wapo watu WENYE uelewa utasaidiwa Sana ukiwa na nidhamu kwenye ku post
kwa nataka msaada umu
 
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.

# Ipo siku !!
 
Back
Top Bottom