RUKUKU BOY
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 1,516
- 1,775
wakuu kuna uzi humu ulikuwa unabainisha ya kwamba JPM hatafanya lolote katika kipindi cha miaka mitano, me kuna mambo anayoyafanya yananiboa ila kwa mazuri anayo yafanya nampongeza pia. kwa upande wangu mazuri ambayo JPM,, ashafanya ni, kuondoa tatizo la kihstoria la wanafunzi kukaa chini kisa kukosa madawati, kupunguza tatizo la kihistoria la ukosefu wa mabweni UDSM, kufufua shirika la ndege sasa kuna bombardierq400 uku kuna oda ya ndege nne,SC300,Q400,unaweza kupitia mwenyewe kujionea kwenye web ya bombardier, pia oda ya BOEING787(dreamlinear) japo watu wanabeza lakini zikitua mwaka kesho litakuwa jambo jema, ujenzi wa ubungo flyover, jumaa tatu anaweka jiwe la msingi na ujenzi unakamilika 2020, ujenzi wa standard gauge, juzi katibu mkuu wizara ya fedha alizibitisha kuwa wameshalipa malipo ya awali ya bilioni300,jiwe la msingi wanaweka mwezi ujao. so sio kweli hatafanya kitu kuna vitu atavifanya na atakumbukwa mfano kuamisha serikari dodoma, mabaya yake ni udikteta uchwara, kunyima wanafunzi mikopo na ajira za kusuasua. mtu akifanya vizuri mpongezi