Hakuna ubishi kutokana na kazi nzuri anayoifanya rais wetu mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu John Pombe Magufuli ya kututumikia Watanzania kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu kuelekea Tanzania mpya, kuna kila sababu rais wetu mpendwa apewe cheo cha "sir".
Kusimamia uadilifu serikalini, mapambano ya ufisadi na rushwa, kuimarisha uchumi wa nchi, maboresho ya elimu na afya , ujenzi wa miundombinu ni baadhi ya mafanikio ya rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli.
Kwa sasa Watanzania wengi wanaunga mkono juhudi za rais wetu katika ujenzi wa Taifa imara la Tanzania lenye kutumia rasilimali zake kwa maendeleo ya Taifa.
Hivyo ni wakati sasa Mamlaka ya Malkia wa Uingereza wampe
cheo cha " sir" kwani anasifa zote za kupewa heshima hii.