Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Trust me TRA kuna uwezekano mkubwa wakawa wanakusanya trillion 2.5 kwa mwezi katika kipindi cha kuanzia miezi 6 ijayo. Kuna jamaa yangu anadai amepigiwa simu na bosi wake (Mchina) katika hali ya dharura (urgency ya ajabu) na kwa kushtukiza (as if mtu anaepiga simu fire/ambulance) akimsihi na kumsisitiza atoe risiti za TRA kwa kila mzigo atakaouza hata ukiwa ni mzigo Wa millioni 50, ahakikishe anaandika risiti ya 50m exactly bila kupunja hata 100 kwa kuandikia nusu risiti Kama wafanyavyo wafanya biashara wengi. Wakati Mchina huyo anapiga simu hiyo alikuwa akihema kama anakimbizwa, ikabainika alikuwa anarush ku-solve ishu nzito ya Mchina mwenzake alie tiwa nyavuni na mamlaka kwa masuala ya ukwepaji kodi..., ni mkimbizano na mtifuano mkali sana unaendela kwa sass..
Kodi muhimu.
 
Ee Mungu simamia hawa ndugu zangu Watanzania wazidi kumuoombea rais wetu Magufuli. Nakuomva pia uzidi kumpa ulinzi wqoko wa heri ili azidi kufichua yote yaliyojificha. Baba katika jina la mwanao Yesu Kristo ninaomba na kuamini kuwa utazidi kutenda miujiza na kuzidi kumbariki Magufuli.
Mungi ibariki Tanzania
Mungu M bariki Magufuli.
Amen.
 
Tatizo la Tanzania sio chama, tatizo tulikosa kiongozi mwenye mapenzi na taifa lake, anaetaka kuwatumikia watanzania kwa hali na mali, mwenye uchungu na taifa lake hili halikuwa upande wa ccm ila ata ukawa kwa Lowassa walifeli pia hivo huwezi kusema kama pandikizi ikiwa yule wao walibugi
Sasa kapatikana.
 
I second you.
CCM (Ilani) sio muasisi wa ufisadi. Lakini CCM (wanachama) ndio waasisi wa ufisadi, halikadhalika CDM na Ukawa yote (misingi ya chama) hawaelekezi watu kuwa mafisadi bali hao wanaojiita Ukawa (wanachama) hawana title ya ( usafi)
Nirudie tu kusema nchi hii tulikosa mtu atakaye tekeleza yale yaliyo katika maandishi (Ilani zetu na katiba).
Kweli mkuu.
 
Kwaiyo wakina.Lissu ndio wangeongoza nchi????'! Hivi unajua mamlaka ya raisi???? We mende kweli yani Chadema ndiyo walikuongopea hivi???

Tafakari kauli hizi;-

1) Muda mwingine yatubidi kubadili gia angani- Mbowe

2) Tuko tayari kusaini mkataba na shetani ilimradi tuitoe CCM - Lissu

Kama ungenielewa vizuri basi ungejua kuwa ata wapinzani wanania ya kwenda ikulu kupiga dili na sio kuwatumikia watanzania na hili ndilo nililozungumza tatizo letu mtu atakaeongoza na sio chama ndugu usijifanye unajua sana mie mwenyewe nilikuwa hiyo chadema naijua vizuri tu ila ujio wa fisadi ulinifanya niachanenao maana tukilolipigia kelele leo tunalikumbatia
Duh! [emoji15]
 
Wajinga nyinyie watu wa Ukawa mlisema hata CCM ikileta mgombe Malaika ata geuka kuwa shetani,naona mna mfagilia Magufuli mmesahau kejeli zenu vibaraka wa Mbowe hamna akili kabisa,mkamshabikia yule Fisadi Lowassa eti awe Rais!
[emoji3][emoji3][emoji3] Wepesi wa kusahau.
 
Ndugu zangu,
... Ni moja ya vichwa vya habari vilivyopamba gazeti moja nchini Sweden vikisimulia habari ya Rais wa Tanzania aliyetoka Ikulu kwa miguu na kuingia mitaani kufagia na kuzoa takataka kwa mikono. Nimetafsiri kwa uchache kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswidish.
Tafsiri yangu:
Naam, kwa wenzetu, John Magufuli anachukuliwa kama mfano mzuri wa kiongozi anayeongoza kwa kuonyesha kwa vitendo, na asiye na makuu wala tamaa ya kujilimbikizia mali.

Maggid
Iringa
Viva JPM.
 
wenzetu wazungu huwa wanataka ukiwa unawaelewa kitu uwaangalie machoni......kwa sababu uso wa mtu humtambulisha mtu....ukimwangalia JPM usoni lzm uamini anachokisema coz you can read it from his face!!
Kweli kabisa.
 
Simnyimi la hasha lakini huko tuendako tukakutana na hali ngumu sana hasa yeye kwakuwa vita anayopigana ni yake binafsi na hana support ya jeshi ya kisiasa na kimkakati (ccm and organs)kashfa za TRA kashfa za meter za mafuta na huko kwingine alikopita, mgomo wa chini kwa chini wa mawaziri wake kugoma/kupuuzia/kukataa kurudisha fomu za maadili mpaka walipochimbwa mkwara si dalili njema hata kidogo
Kuna majipu ya maliasili mitandao ya simu nk yanakuja utashuhudia mengi huko....ishu ya sukari umeona ilivyoleta sintofahamu kubwa? Wasaidizi wake ni chui waliojivika ngozi ya kondoo na shida itaanzia hapo
Aaaah!
 
Imagine popularity ya JPM, mimi nilidhani ni DRC peke yake, wapi bwana mpaka hapa kwa mzee M7. kila kitu utasikia aaaaa huyu dawa yake JPM...... mhh inamaana mpaka huku? mimi nilifikiria ni Kenya na DRC tu.... wakati hii slogan ya @WhatWouldMagufuliDo? bado inavuma sana Why?

Heshima kwako Rais wangu
[emoji123][emoji123][emoji109][emoji109]
 
Tanzania tumempata Rais hakuna nchi ya Africa haitamani kuwa na Rais wa hivi mm ni chadema dam ila kiukweli hii kasi ata lowasa asingeiweza hata hayati baba wa taifa hakufikia hapa maguful ni Rais wa kipekee ana uchungu na nchi hii tajiri ila waliifaidi wachache sasa wanatakiwa waishi kama mashetani maskini waishi kama malaika.... huyu maguful ni Rais hataki mchezo ikiwezekana katiba ibadilishwe awe Rais wa milele..... tuu kwa maana hamna namna sasa matajiri wafanyabiashara wanamchukia ila maskini usiongee juu ya maguful utapigwa balaa..

acha waisome namba ee maguful mbele kwa mbeleeeeeeeeeeeeeee

tumbua majipu baba mungu yupo na ww na sisi tunasali na kukuombea daima mungu kwanza mbele
[emoji109][emoji109][emoji109][emoji120] Kula gwala kamanda, maendeleo hayana chama
 
Wacha niseme kutoka moyoni kabisa kuwa mimi CCM na Magufuli hawakupata kura yangu kwasababu ya kile kilichozoeleka kuwa ni watu wa kubebana na kulindana.
Lakini tangu Magufuli ameingia ameanza kunipa tumaini la TZ yangu niitakayo, na nilikuwa namtaka kiongozi ambaye akiingia atawabadilisha watu/watumishi kuwa walizonazo ni dhamana na si kuwa wao ni wafalme ila sisi ( wananchi) ndio mabosi wao.
Nchi ilifikia hatua mkuu wa mkoa/wilaya au wakurugenzi wa wilaya/mkoa ni kama miungu watu akosolewi na muda wote yeye yuko ofisini tu na mwendo wa kuiba tu na kujaza takwimu za uongo. Leo nadhani mnaona wakuu wa mikoa, wilaya,wakurugenzi na hata wakuu wa idara za serikali wanapiga kazi na wanatembelea sehemu za miradi au kusikiliza matatizo ya wananchi.
Leo hii wafanyabiahara walitaka waiendeleza tabia yao ( maana itakuwa hawajaianza leo wameshazoea) ya kuihadimisha bidhaa ili ipande thamani halafu apate faida kubwa sana wakati wananchi tunateketea kwa ukosefu wa sukari kisa eti yeye ana mtaji basi awatese wasiokuwa na uwezo huo.
[emoji109][emoji109][emoji109][emoji123][emoji123][emoji123]
 
Back
Top Bottom