Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

NDUGU wakigombana chukua jembe ukalime na wakipatana chukua kapu ukavune.!
 
Wakati huu wa awamu ya Tano wahujumu uchumi,Mafisadi wameumbuliwa na kufrdheheshwa magerezani kama Raia wengine
Awamu iliyopita hatukuwaona wenye uwezo kifedha wakiwa magerezani,yaani fedha zilikuwa zinaongea,wanyonge walikuwa wanauziwa kesi kila kukicha,ilikuwa hatari sana.Wanyonge walikuwa wanateseka magerezani bila yakosa lolote huku wenye makosa wakiwa wanakula maisha mtaani kisa wameuza kesi,waliofikwa na haya ndio watakoona ukweli

Kulikuwepo na IPTL,Escrow,Richmond na huduma mbovu za kijamii,Mshine ya MRI na CT-Scan kutokufanya kazi ktk Hospitali ya Rufaa Muhimbili,wagonjwa walikufa wasiokuwa na fedha,baadhi kuambiwa wakalipie vipimo vya MRI katika Hospitali ya Regence kwa faida ya watu binafsi,kwani mashine ya MRI waliiharibu na kusingizia ni mbovu ili Regence wafaidike,pia barabara zilikuwa mbovu sana
Kiongozi wa awamu ya nne alikuwa anakwenda nchi za ugenini kama mtu anayetoka Dar kwenda Morogoro,kwanini hizo ziara asingezifanya ndani ya nchi yake ili ajue shida za wanyonge

Hayo yote hayakuonekana?

Hahhahahaa

Mapambano ya ufisadi!

Eti mafisadi wameshikwa!

Guess what?

Mapambano yanakwepa “Wanasiasa au Viongozi”!

Yanashika “Wafanyabiashara” wasio na power yoyote!

Wenye power ya rushwa na kila kitu ni “Wanasiasa au Viongozi”,hao Magufuli hawezi washika wala kusema lolote!

Mpaka akishika Viongozi wote wala rushwa then come talk to me!
 
Hakuna aliyeumbuliwa ni kuwa utasemea wapi wakati hatuna mahakama!
Ni sawa na kumsifia bondia kuchakaza washindani wake huku washindani wanapandishwa jukwaani wamefungwa pingu mikono na miguu.
Hakuna awamu wizi umefanyika kama hii, Trillion 2.4 hazijulikani ndani ya miaka miwili? Huo sio wizi ila kukwapua na kula bila kunawa
 

Ziara ya Waziri Mkuu mkoa wa Singida imedhihirisha upigaji umezidi awamu hii
 

Ziara ya Waziri Mkuu mkoa wa Singida imedhihirisha upigaji umezidi awamu hii
Mafisadi hawawezi kuisha kwani wapo waliobobea,lakini wengi wao watalipa walichokula
 
Rais wa awamu ya Tano anamuenzi baba wa Taifa katika kila eneo husika .Hivyo ni wazi hakuna mpinzani yeyote atakaye thubutu kushindana nae 2020.

Amedhibiti ubadhirifu wa mali na pesa za umma.Anapambana na wala rushwa.

Akitoa maagizo anahakikisha yanatekelezwa.Mtu akifanya kosa hana ushikaji wala msalie mtume.Ameanza kutekeleza sera ya Tanzania ya Viwanda.

Wazee wanamuombea kwa Mungu afanikiwe.Maana kuna kipindi kuna baadhi ya viongozi waliteleza

Hivyo wapinzani labda mdili na nafasi za udiwani na ubunge 2020. Msipoteze muda na pesa zenu
 
Ni kweli, nimeona mafuriko kwenye ofisi za kata wanajiandikisha kupiga kura, tena wamebeba na vipeperushi vya tunaimani na ccm inayomuenzi Nyerere......

Yani kila ofisi ya kata watu wamejaa wanajiandikisha,hadi kufika keshokutwa, watu milioni 70, watakuwa wamejiandikisha.

Hongera Magufuli kwa kumuenzi Nyerere
 
Rais wa awamu ya Tano anamuenzi baba wa Taifa katika kila eneo husika .Hivyo ni wazi hakuna mpinzani yeyote atakaye thubutu kushindana nae 2020. Amedhibiti ubadhirifu wa mali na pesa za umma.Anapambana na wala rushwa.Akitoa maagizo anahakikisha yanatekelezwa.Mtu akifanya kosa hana ushikaji wala msalie mtume.Ameanza kutekeleza sera ya Tanzania ya Viwanda. Wazee wanamuombea kwa Mungu afanikiwe .Maana kuna kipindi kuna baadhi ya viongozi waliteleza .Hivyo wapinzani labda mdili na nafasi za udiwani na ubunge 2020. Msipoteze muda na pesa zenu
 
Rais wa awamu ya Tano anamuenzi baba wa Taifa katika kila eneo husika .Hivyo ni wazi hakuna mpinzani yeyote atakaye thubutu kushindana nae 2020.

Amedhibiti ubadhirifu wa mali na pesa za umma.Anapambana na wala rushwa.

Akitoa maagizo anahakikisha yanatekelezwa.Mtu akifanya kosa hana ushikaji wala msalie mtume.Ameanza kutekeleza sera ya Tanzania ya Viwanda.

Wazee wanamuombea kwa Mungu afanikiwe.Maana kuna kipindi kuna baadhi ya viongozi waliteleza

Hivyo wapinzani labda mdili na nafasi za udiwani na ubunge 2020. Msipoteze muda na pesa zenu
WTF!!!
 
ALIYOHARIBU JPM.

Leo 16:30pm,15/10/2019.

Ahsante msomaji wangu kwa kunipigia simu na kusifu kipaji changu cha kuandika na kusema Msemakweli Chakubanga ni kati ya watu wanne wanaothamini juhudi za "Hapa Kazi Tu" maana zinaonekana na zinaandikwa kuwekwa kwenye historia kwa ajili ya vizazi hadi vizazi.

Leo nikuletee makala ya aliyoharibu Jpm ili upate kujua mengi au machache aliyoharibu jpm.

Lakini,Je ni kweli Jpm kaharibu kila kitu kwa muda wa miaka minne tu? Fuatana nami hadi mwisho kuweza kujua hili,

Jpm kaharibu kujenga mradi wa umeme mkubwa,Bwawa la Rufiji (Bwawa la Mwalimu Nyerere) unaozidi uwezo wa umeme wote unaozalishwa tangu mkoloni,Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete na Sasa hakuna tena mgao wa Umeme,tutapata Umeme na kusaza,tutasahau habari ya iptl,dowans,Richmond na Escrow!.

Jpm kaharibu kujenga Reli ya Umeme,Reli ya kisasa yenye uwezo mkubwa wa kwenda kwa haraka na kubeba mzigo mkubwa kuliko Reli zote nchini,Treni ambayo itatumia saa moja na nusu toka Dar hadi Morogoro,na Massa matano tu toka Dar hadi Mwanza,hii itafanya kuharakisha Maendeleo,badala ya kusafiri Masaa 17 toka Dar hadi Mwanza.

Jpm kaharibu kujenga maghala ya kutunzia vyakula kwa mikoa yote inayozalisha vyakula kwa hifadhi za taifa letu,Sasa Taifa litakuwa na hifadhi ya kutosha ya Mazao ya Chakula.!.

Jpm kaharibu kwa kufufua shirika la ndege la atcl na ununuzi wa ndege zake kumi na moja kwa ajili ya kukuza na kuboresha sekta ya Utalii,hivi sasa tunashuhudia Watalii zaidi ya 1,000 wakitua nchini.

Jpm kaharibu kwa kutoa ruzuku ya kielimu ( elimu bure) kwa shule za misingi na sekondari,hivi sasa hakuna mtoto asiyejua kusoma wala kuandika.!.

Jpm kaharibu kwa kujenga hospitali kwa wilaya zote ambazo hazikuwa na hospitali za wilaya na vituo vya Afya zaidi ya 300 nchini baada ya kuvikuta vituo 67 tu!

Jpm kaharibu kwa kumalizia miradi iliyoanzishwa na watangulizi wake ambayo ilikwama kuendelea baada ya pesa kupigwa ama ujenzi usioridhisha kama barabara,Madaraja,Viwanja vya ndege vya zamani na Vipya,Kujenga barabara za juu na zile za kukatisha bahari ya hindi na kule ziwa Victoria na vivuko mbalimbali.

Jpm kaharibu kwa kuendelea kujenga miundombinu ya bandari na ujenzi wa meli mpya kwa maziwa ya Nyasa,Victoria na Tanganyika!.

-Kwa nini Jpm aliharibu,Kwa sababu ni Mzalendo na ayafanyayo yapo damuni,ukimchana hivi damu yake inasema Mimi ni Mtanzania,nitapenda kuiona Tanzania ikiwa Taifa kubwa kama China.

-Jpm aliharibu baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanza miradi mingi nchi nzima,miradi inayoonekana kwa macho na sio miradi hewa ama ya kitapeli kama miradi tuliyowahi kuisikia siku za nyuma,Miradi inayofanyika sasa na inayoonekana wazi na Wananchi wanapata faraja,ni miradi ya barabara nchi nzima,meli,vivuko,umeme,maji,afya,utalii,bandari,na viwanja vya ndege,Siku za nyuma tulikuwa tunaambiwa maneno tu ama kuishia kuona ujenzi usioridhisha.

-Mwaka 2016 Jpm aliharibu pale alipoanza kwa vitendo na watu waliita nguvu ya soda,lakini siki zilivyozidi kwenda watu waligundua si povu wala nguvu ya soda bali mtendakazi yupo kazini.Ujenzi ulioanza na kumalizika ulitoa picha ya utendaji wa kutukuka katika awamu hii ya tano,Mwaka 2016 tulianza kuona matunda halisi ya maneno,ahadi na utendaji kazi wa Awamu ya tano.

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 zikaja ndani ya Mwaka huo huo wa 2016).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dar es Salaam.
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.

-Mwaka 2017 Jpm aliharibu pale tulipoona ujenzi mkubwa miradi mbalimbali ukianza.

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

-Jpm kaharibu kwa ukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji,Dar,Morogoro,Dodoma,Kigoma,Tabota,na Shinyanga.

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga.

-Jpm kaharibu kwa kuwa kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea.

Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano barabara imejengwa,Mitaa ya Kinondoni hivi ina lami,Ubungo Interchange inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa kwa kiwango cha barabara nane.

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa

-Jpm kaharibu kwa ujenzi wa Flyovers zinajengwa pamoja na barabara za ziwani na baharini.

-Jpm kaharibu kwa kuisimama vyema miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe,Miradi wa Umeme wa Gas wa Kinyerezi,na mradi wa Bwawa la Umeme la Rufiji (Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere)

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji.

Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

-Jpm kaharibu kwa kusimamia utendaji kazi na kufanya performance appraisals, Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto.Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

-Jpm kaharibu kwa kuleta Uwajibikaji,Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika,hakika nidhamu imeimarika.

-Jpm kaharibu kwa usimamizi madhubuti wa mapato ya Serikali, sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiashara na si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio.

Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

-Jpm kaharibu kwa kusema nidhamu kazini,Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

-Tujikumbushe Walioitendea kazi Tanzania.

Nyerere alilifanyia kazi taifa miaka 23.

Mzee Mwinyi alihudumu miaka 10 ambapo alifanikiwa kupata stimula kwa ajili ya kufufua uchumi ulioharibiwa na Vita vya Uganda.

Mzee Mkapa alihudumu miaka 10 alifanikiwa kuondoa gharama zisizobebeka za mashirika yaliyoleta hasara kwa kushindwa kuleta Gawio kwa Serikali.

Mzee Kikwete alihudumu kwa miaka 10,alifanikiwa kuanza kulipa Watumishi wa Umma baada ya kutaifishwa kwa mashirika ya Umma yaliyoitia hasara Serikali.

Mh JPM ni miaka 4 sasa lakini kwa takwimu chache ameweza kufanya yale yote yaliyoshindwa kufanywa miaka 23 na kumi kumi mara tatu.

Ikiwa haya yote ni ya kuharibu basi baada ya miaka 10 yake kuisha taifa letu litabaki halina rasilimali iliyoibwa kiasi cha kufanya Tanzania kuwa kama China.

Mungu mbariki Rais wa Tanzania,Ndugu John Pombe Magufuli,Mungu ibariki Tanzania.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.
 
Kweli huyu jini ccm atafute pesa stress zinamuua yeye na jiwe lake.
 
Tunajua Congo ni failed state ndivyo ambavyo ingekuwa kwa Tanzania baada ya Mzee kikwete kustaafu kama tusingempata Magufuli hakika Tanzania ingekuwa imeharibika kama Congo

Ile tano bora ilijaa wagombea wapole kiliko hata Mzee kikwete ukitoa Magufuli

Tunaona upole wa kikwete ulivyopelekea Mafisadi kuchezea Nchi
Hebu fikiria dada amina au migiro angekuwa Mkuu wa Nchi Au Mzee membe angekuwa Mkuu wa Nchi

Ule ufisadi ungetamalaki mara mbili,mgao wa umeme ungekuwa mara mia zaidi Kwasababu Hakuna hatua ambazo zingechukuliwa

Niseme tu wazi ugomvi wa kisiasa wa Mzee lowasa na kikwete ulikuwa ni mpango wa Mungu kwa watanzania

Ona Nchi inavyopaa chini ya mzalendo Magufuli
 
Kiukweli mheshimiwa Rais anafanya vizuri kuinyoosha hii nchi! Hata hivyo ni wajibu wake na kulikuwa hakuna haja ya kupiga kelele kila siku kumpongeza kwa kuwa kufanya hivyo ni sehemu ya wajibu wake.
 
Unalipwa kiasi gani wewe kwa siku na huyo magufuli wako? Maana muda wote unawaza kumsifia, kumsujudia, kumpamba na kumtukuza tu! Hivi huchoki?
 
Back
Top Bottom