Watumishi wa umma wamenufaika sana na utawala wa Rais Magufuli, 306,917 wamepandishwa vyeo na madaraja na kulipwa madai yao mbalimbali ya jumla ya shilingi bilioni 472.6.
Kati ya hizo shilingi bilioni 114.5 yalikuwa ni madeni ya mishahara na shilingi bilioni 358.1 yalikuwa ni madeni yasiyokuwa ya mishahara kama vile uhamisho.
Watumishi wengi wa umma ni mashahidi jinsi walivyopandishwa vyeo na madaraja wakati wa utawala wa Rais Magufuli baada ya kugota katika madaraja hayo kwa miaka mingi. Kupandisha watumishi 306,917 kati ya watumishi takriban 500,000 wa umma haijawahi kutokea.
Viva Rais Magufuli, viva watumishi wa umma. Kura zetu tunampa Mhe Rais Magufuli. (Source za takwimu ni hotuba ya Rais Magufuli akifunga Bunge tarehe 16 Juni 2020).
Tunakwenda na Rais Magufuli.