Mafia: Watu 7 wafariki dunia baada ya kula nyama ya Kasa

Mafia: Watu 7 wafariki dunia baada ya kula nyama ya Kasa

Watu saba wamefariki dunia baada ya kula samaki aina ya kasa anayesadikiwa kuwa na sumu katika Kijiji cha Bweni na Kanga Wilayani Mafia Mkoani Pwani.

Watu hao wanatoka kwenye kaya nne tofauti kijijini humo na walifariki kwa nyakati tofauti Machi 12 mwaka huu mara baada ya kula samaki hao.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa kipolisi Rufiji, Canute Msacky amesema kati ya watu hao saba waliopoteza maisha ni watoto sita.

Kamanda Msacky ametaja majina ya waliokufa ni Mohamed Makame umri miezi Saba, Minza Hatibu (miezi kumi), Ally Seleman (miezi nane), Ramadhan Karimu (miezi nane), Abdala Nyikombo (miaka 4), Makame Nyikombo (miaka tisa) pamoja na Salima Mjohi (miaka 28).

"Ni kweli tukio lipo ni watoto sita wa kuanzia miezi saba na mtu mzima mmoja ndio wamefariki, na taarifa za awali ni kwamba wamekufa baada ya kula samaki aina ya kasa anayesadikika kuwa na sumu, na hawa watu walipoteza maisha kwa nyakati tofauti tofauti kuanzia usiku majira ya saa Moja Machi 12 "amesema Kamanda Msacky.

Ameongeza kuwa miili ya marehemu wote imeshafanyiwa uchunguzi wa kitabibu katika hospitali ya Wilaya ya Mafia na tayari wameshakabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi.

Kuhusu chanzo cha tukio hilo, amesisitiza kuwa bado kinaendelea kuchunguzwa.

Aidha Kamanda Msacky ameeleza tayari watuhumiwa watatu wanashikiliwa na Jeshi hilo kwa mahojiano zaidi.

"Tumefanikiwa kuwakamata watu watatu kwa mahojiano zaidi ambao nao wamelazwa hospitali ya wilaya hapa Mafia baada ya kuzidiwa wakiwa chini ya uangalizi wa Jeshi hilo kwani nao walikula nyama ya samaki huyo" ameongeza

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mafia limetoa wito kwa wavuvi kuacha tabia ya kuvua samaki aina hiyo ya kasa ambao ni nyara za Serikali.

Kamanda Msacky ameshauri wafuate kanuni na sheria za uvuvi wa samaki hao kwani Polisi wataendelea kuchukua hatua kali kwa wavuvi wasiofuata taratibu na sheria za nchi.

MWANANCHI
 
Mwenye kiharufu ni papa, labda Ndo maana na nanihiii ikaitwa papa🤣
Nathani ni huyo maana niliwahi kula mahali yaani ilibidi niwaulize wanyeji mchuzi umeingia mafuta ya taa kwa kweli sikuendelea na chakula kile.
 
Na unaweza kuta ni degree holder wewe tena UDSM.
Elimu za sasa hizi dah...

Kwa ukiambiwa zanzibar ni visiwa vitatu utakubali, au ukiambia mafia ni mkoa wa pwani utakubali...

Upo upo yaani hauna unalolijua
Hata kiswahili chako kinaonesha upo vzr umekamiliza.!
 
Halafu kuna binadamu wenzetu wanakula!
Nyie , tule tu nyama za ng'ombe na kuku inatosha.

Pweza tu nikiona mtu anakula huwa najisikia kuruudisha chenji.
Daah chakula kizuri kabisa hicho Pweza wewe urudishe chenji?pana kaa wa baharini nao wanaliwa pia..
 
Back
Top Bottom