mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 88,759
- 123,368
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kasa mtamu sana ananyama tam, ukimla kwa wale wapenzi wa lager, rangi ya mende ukishushia na safari 3 kubwa bariiidi, utajihisi goliatiMpaka muda huu watu sita wamefariki dunia baada ya kula nyama ya kasa kisiwani Mafia wakiwemo watoto wawili ambao ni ndugu huku baba yao na mama yao wakiwa wapo hospitali hapa Mafia wamelazwa.
Taarifa zinakuja sababu bado huduma inaendelea watu ni wengi waliokula taarifa inakuja ishazikawa miili ya watu watatu, bado watatu.
=======
Watu saba wamefariki dunia baada ya kula samaki aina ya kasa anayesadikiwa kuwa na sumu katika Kijiji cha Bweni na Kanga Wilayani Mafia Mkoani Pwani.
Watu hao wanatoka kwenye kaya nne tofauti kijijini humo na walifariki kwa nyakati tofauti Machi 12 mwaka huu mara baada ya kula samaki hao.
Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa kipolisi Rufiji, Canute Msacky amesema kati ya watu hao saba waliopoteza maisha ni watoto sita.
Kamanda Msacky ametaja majina ya waliokufa ni Mohamed Makame umri miezi Saba, Minza Hatibu (miezi kumi), Ally Seleman (miezi nane), Ramadhan Karimu (miezi nane), Abdala Nyikombo (miaka 4), Makame Nyikombo (miaka tisa) pamoja na Salima Mjohi (miaka 28).
"Ni kweli tukio lipo ni watoto sita wa kuanzia miezi saba na mtu mzima mmoja ndio wamefariki, na taarifa za awali ni kwamba wamekufa baada ya kula samaki aina ya kasa anayesadikika kuwa na sumu, na hawa watu walipoteza maisha kwa nyakati tofauti tofauti kuanzia usiku majira ya saa Moja Machi 12 "amesema Kamanda Msacky.
Ameongeza kuwa miili ya marehemu wote imeshafanyiwa uchunguzi wa kitabibu katika hospitali ya Wilaya ya Mafia na tayari wameshakabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi. Kuhusu chanzo cha tukio hilo, amesisitiza kuwa bado kinaendelea kuchunguzwa.
Aidha Kamanda Msacky ameeleza tayari watuhumiwa watatu wanashikiliwa na Jeshi hilo kwa mahojiano zaidi.
"Tumefanikiwa kuwakamata watu watatu kwa mahojiano zaidi ambao nao wamelazwa hospitali ya wilaya hapa Mafia baada ya kuzidiwa wakiwa chini ya uangalizi wa Jeshi hilo kwani nao walikula nyama ya samaki huyo" ameongeza
Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mafia limetoa wito kwa wavuvi kuacha tabia ya kuvua samaki aina hiyo ya kasa ambao ni nyara za Serikali.
Kamanda Msacky ameshauri wafuate kanuni na sheria za uvuvi wa samaki hao kwani Polisi wataendelea kuchukua hatua kali kwa wavuvi wasiofuata taratibu na sheria za nchi.
Pia soma > Kwanini watu wanakula Kasa licha ya wengine kufa kwa sumu waliyonayo?
Huo ni ulafi
Watu hawajatosheka na nyama zote hizi duniani
Weamua kuhamia kula Kobe[emoji119]
Matatizo mengine ya kujitafutia.
Ukome kula vitu vya ajabuajabu, mmekuwa kama wachina hamchagui nini mle.naendelaea vyema ila mwili hauna nguvu
wewe ishia kula sangara, sato na panya bukuYaani mtu unakulaje kasa sijui pweza
Kuna aina at least mbili za kasa, wale wanaoliwa na wenye sumu.Ulishawahi mla?
Uliumwa?
Au zamani hakuwa na sumu sasa ana Sumu?
Somo kuu la jiografia:Hivi Zanzibar ina visiwa vingapi maana nilikua nafikir ni unguja na pemba.
Hiyo mafia ipo wapi??
naendelaea vyema ila mwili hauna nguvu
kasa hana sumu ila ikitokea ikawa amekula mwani na bahati mbaya akavuliwa ma watu ndio hutokea haya sababu mwani ndio wenye sumu mimi nilimkuta tayari ashapikwa nikala kiasi mwingine nikaweka nimalizie asubuh kumbe dah we acha tuMkuu unachangamsha genge au ni kweli na wewe ulimla huyo kasa? Najua wewe ni mvuvi huko mafia na mzoefu wa kuwajua samaki ,na kuna misemo sana tunaitumia mashuleni kama "umenilisha kasa yaani umenipa sumu desa bovu" inakuwaje bado elimu ya hawa kasa hamuijui? Kila siku kesi za vifo vitokanavyo na ulaji wa kasa vinatokea lakini nashangaa hadi nyinyi wazoefu hamjifunzi,nini tatizo?
kasa hana sumu ila ikitokea ikawa amekula mwani na bahati mbaya akavuliwa ma watu ndio hutokea haya sababu mwani ndio wenye sumu mimi nilimkuta tayari ashapikwa nikala kiasi mwingine nikaweka nimalizie asubuh kumbe dah we acha tu
upimaji wake wakati wa kuikata nyama pale inapokuwa mbichi huwa inawasha mikononi sasa sijajua wale jamaa walomvua ila maajabu waliokamtawa sio waliovua bahariniMkuu inabidi uwape elimu wavuvi wenzako kwamba wakivua kasa before kumla watafute wataalam wapime kama ana sumu au lah.
Si Kobe huyu jmn
Si Kobe huyu jmn
Nacheka kama mazuri 🤭🤭 kimsingi Tu stay away na huyo Kobe maji , hakuna haja ya kubet na uhai huu wenye Mashakakasa hana sumu ila ikitokea ikawa amekula mwani na bahati mbaya akavuliwa ma watu ndio hutokea haya sababu mwani ndio wenye sumu mimi nilimkuta tayari ashapikwa nikala kiasi mwingine nikaweka nimalizie asubuh kumbe dah we acha tu
Shukrani sana mkuu, hao wadudu wote hawana mvuto asee, uyo mwenye miba mimba nshamwona beach akiwa amekufa mara kadhaaView attachment 2549206
[emoji115]Bunju anakuwa kama chura fulani na ana miba kibao
View attachment 2549203
[emoji115]mkunga kama nyoka wapo wanatishia kinoma Kuna wengine ni jamii ya nyoka wa bahari ukileta Tamaa ukafiria mkunga ukamla ndo kwisha habari yako...Kuna wavuvi wanagonjwa na wale nyoka bahari wakifiria ni mkunga
🤣🤣Shukrani sana mkuu, hao wadudu wote hawana mvuto asee, uyo mwenye miba mimba nshamwona beach akiwa amekufa mara kadhaa
Huyo sio kasa... Labda unazungumzia "mkunga"Kula kasa au sea turtle ni sawa na kula nyoka au reptile. Kasa ni jamii ya nyoka.
Hiki ni kisiwa kwahiyo wenyeji wengi ni walowezi kutoka rufiji ambao ni wandengereko. Pia wapo watu kutoka mtwara na kilwaNimekupata, asante sana!
Hiyo wilaya imejitenga sana maana mara ya mwisho kusikia neno Mafia duu, miaka kadhaa imepita.
Kabila gani wanapatikana huko!?