Mafundi simu wa upande wa hardware naomba tukutane hapa

Mafundi simu wa upande wa hardware naomba tukutane hapa

Hiyo taa niliyoweka jumper haikuwepo nimechukua taa ya nokia 1280 nimejumper namna hiyo.




Sehemu niliyoweka TWIZER nataka niweke jumper

nimebadili kioo kipya kinasoma ila tatizo hakioneshi mwanga.



NI HAYO WAKUU.


hazole1
hiyo simu kama iliingia maji kwangua na wembe kwanza kwenye njia za mwanga uangalie kama hazijakata.
 
Tecno W5 yangu unasumbua speaker siku hizi sauti ndogo Sana Nasikia kwa shida je naweza badilisha? Hakuna risk yoyote
hapo solution ni kubadilisha ila kama ni speaker ya sikioni tu jaribu kusafisha na mswaki huenda kuna vumbi.
 
Mimi napenda kuwa fundi simu ila sijui kozi zakusoma naweza kupata msaada kozi zipi na chuo kipi kinafundisha hizi mambo
ila inatakiwa hapo kwenye maeneo ambayo upo jaribu kumtafuta fundi mzuri. ujifunze kwanza ule mwanzo wa ufundi. kwa mfano kufungua simu. kuunga mic. kuunga speaker. kubadilisha vioo. kubadilisha temino. kubadilisha syestem chaji. na ujifunze kutumia mita hata kidogo.
hivyo vingine utajiongeza mbele ya safari kwa mfano baadhi solution unaweza ukawa unajisomea kwenye google.
ila kiujumla ufundi hauna mwisho kwasababu teknolojia inabalika kila siku.

kwahiyo hata sisi hapa bado kuna mambo bado tunajifunza.
 
Habari mh, mtaalam wa sim..Nina sim aina ya Nokia asha201 tatizo lake ilizima gafla tuu... Baadae nikaipeleka kwa fundi akaiflashi ikawaka sasa nikanunua na betr mpya sasa tatizo limerudia tena hata kama betr inachaji haiwaki au ionyeshe MwaNgA kisha inazima moja kwa moja tatizo n nn mkuu
mpekee tena huyo fundi aingalie tena.
 
Wakuu mi sio mtaalamu wa hardware ila nipo fiti kwenye software tatizo langu nimepata huawei g610-u00 nataka kuiflash lakin haitaki kudetect... Nikiiwasha inaishia kwenye logo tu... Nimeweka collect drivers lakin bado haitak kudetect
hiyo labda itakuwa imeua memory. kwamaana huawei huwa zinatabia hiyo.
 
Hii imekataa kabisa kusoma LAINI no itel
efae0a022d5692f5e6f25d4aa8f4c243.jpg
hiyo itakuwa ya kuflash.
 
sasa mziki unakua pale kwenye kuitoa na kioo kinaweza kupasuka.
Mkuu,uwezekano wakupasuka ni mdogo san 0.000001%.
Kama mimi sijawah kupasua tangu hizo touch zianze kupatkana.Si izo tu,hat J7,C8,C9,L8...
 
Mkuu,uwezekano wakupasuka ni mdogo san 0.000001%.
Kama mimi sijawah kupasua tangu hizo touch zianze kupatkana.Si izo tu,hat J7,C8,C9,L8...
mkuu labda sisi kwasabu huwa tunakomaa kutolea bloa na ndio maana sometime huwa zinazingua.
ila saizi nilikua na mpango wa kununua mashine ya kubadilishia. hivi hapo mjini huwa zinatembea bei gani?
 
hiyo simu kama iliingia maji kwangua na wembe kwanza kwenye njia za mwanga uangalie kama hazijakata.
Haikuingia katika maji ilzima tuu.


Ila ngoja niangalie njia.


Njia niliyoonesha kwa jumper na twizzer ni sahihi?
 
Back
Top Bottom