Mafundi simu wa upande wa hardware naomba tukutane hapa

Mafundi simu wa upande wa hardware naomba tukutane hapa

Mambo vp mkuu
Nina tecno W4 ilizima gafla nikiwa naangalia video haionyeshi chochote kwenye screen ila nikiichomeka charger inawasha taa nyekundu tatizo linaweza kuwa lipi
Nadhani tatizo ni Betri charge yake imeisha sana imepelekea kwamba hiyo simu yako inashindwa kuli charge li boost kwa kutumia kobe km huna kobe julisha nikupe maelekezo namna ya kutengeneza kobe yako
 
Nadhani tatizo ni Betri charge yake imeisha sana imepelekea kwamba hiyo simu yako inashindwa kuli charge li boost kwa kutumia kobe km huna kobe julisha nikupe maelekezo namna ya kutengeneza kobe yako
betri ni built in mkuu haitoki
 
Wadau mi nina Techno Y2 ina miezi mitatu tangu niinunue lakini siku nne baada ya kui ununua ikaanza kujizima niliporudi dukani wakanambia labda tatizo ni betri wakanipa betri nyingine lakini hali ikawa ni ileile.
Ikijizima haiwaki mpaka utoe betri halafu uirudishie.
Nimeongea na watu kadhaa wanaomiliki simu kama hii wameniambia kuwa wana tatizo hilo hilo.
Waungwana naomba ushauri wenu kuhusu tatizo hili.
Natanguliza shukrani
Pole hiyo day 4 ilipaswa wakupe nyingine. swali ukirudishia hilo betri kuwaka inachukua muda gani
 
Wakuu msaada,kuna simu imenizingua hapa,nimehangaika nayo ni samsung sm-b350e inajichaji yenyewe tu
 
kazi ya hardware ni ngumu sana na yenye lawama nyingi.

kuna simu unaweza ukaifungua ukaifunga na ikagoma kuwaka na wakati huo mteja alileta umbadlishie mic tu. na ukatemgeneza ugomvi mkubwa na mteja na akasema umembadilishia saketi na mnaweza kufikshana hata polisi mteja kama sio muelewa.

tatizo linakuwa wapi?

inamaana wakati unaifungua hiyo simu ulitoa betri bila kuzima simu. kwahiyo unapo toa betri hakikisha unazima simu.
na ikizima hivyo solution yake simu inatakiwa iende ikaflashiwe.
lakini tatizo lingine hawa mafundi software wanatuangusha sana mafundi hardware huwa hawataki kukomaa kabisa na wanapenda kazi rahisi rahisi na sijajua tatizo nini kwamba mazingira yanawabana au vipi.
kwasababu wao simu nyingi ukiwapelekea za kuflash. wanakuambia memory imekufa au kwenye computer haisomi lakini ukipima njia za usb ziko safi.

kazi ya hardware inahitaji akili yako zaidi tofauti na majamaa wanao deal na software wao kila kitu wanagoogle.

sisi upande hardware kuna baadi simu hata ugoogle vipi huwezi kupata solution hasa hizi tecno.

na ktk matatizo ya simu ambayo yanawatesa mafundi simu ni haya matatizo ya tecno.
na hii tuseme ukweli tecno na simu ya kimaskini na ndio maana kila mtanzania mwenye kipato cha chini anakimbilia.
na tecno ni simu ambayo matatizo yake ni pasua kichwa na ndio maana tatizo lolote ukiwapelekea tecno wenyewe wanakimbilia kubalisha saketi.

mm ni fundi ambaye natengeneza simu nyingi ambazo mafundi huwa wanzangu wanazishindwa.

siri ya ufundi simu.

1 ni kujua kuitumia mita vizuri 2 kujua kutumia gani vizuri 3 kuwa msafi 4 na kuwa mkweli.


kuna baadhi simu za tecno ambazo mafundi simu walisha kata tamaa kwamba hazi tengezeki lakini leo nitawapa baadhi ya solution kadri muda utakavyo kuwa unaniruhusu.
na kama hata ww utakuwa unasolution yoyote tutaomba tuzidi kusaidina.

tecno h5 p5 m3 hizi simu zimekuwa na tazizo sugu ukitaka kuiwasha tu inakuwa inajiminya button ya kujifomart

lakini mm kadri ya uwezo wangu nilijitahidi kugungundua solution ya hii tecno m3 kwa 100%.
6f06381cdf67ac7eb57f385f2952f45f.jpg


na leo nataka nianzie hapo baadaye nitaleta solution
za tecno

fake charging tecno h6 l5 l6 tecno c8 c5

harafu nitaleta solutiona ya mic ya tecno ya tecno t340 na tecno zote zina zinazotumia system ya chaji ya v3

na hizo solution huwezi kuzipata pale na zamani tulizoe solution kutoka india lakini hizo simu india hazipo kwahiyo waafrika tukomae.
a944acda1b58e4797615d8effa838260.jpg

a67f5381f1ad179f27405ce8800c3316.jpg
Anzisha group whatsapp mkuu itasaidia sana
 
Back
Top Bottom