Hajto
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 5,646
- 5,606
Nimekupata vizuri kabisa,Ni ivi izo separate mita za kusoma matumizi ya mteja inatakiwa mita kuu ya Tanesco iwe na Umeme,izo separate mita hua zinafungwa sana kwenye majengo makubwa ama hata yale ya kawaida isipokuwa mita kubwa isiwe ya kutumia Luku,Kwetu Tanzania wenye majengo makubwa wao wanatumia zile mita za bili yaani mita zao zinasomwa mwezi hadi mwezi,sasa izo separate mita zilivyo ni zilezile tu kama zile za Tanesco kwani hao agent ndio wanaowauzia tanesco mita,sasa wewe ukishakuwa na mita kubwa unaongea nao kisha wanakufungia halafu kuna ki-softwear wanakupata kinakuwa kinaunganishwa na mita unit zinazosoma mita kubwa,utaamua wewe wakuunge utumie kwenye desktop,laptop ama simu kwaiyo mteja akitaka umeme kwenye mita yake unaingiza mita yake kisha kinakupatia tokeni ndio unayoingiza na mteja hapo atapata umeme na pia ukiisha umeme kwake utakata ila kwa wapangaji wengine wataendelea kupata,ni nzuri sana izo mita ama kama utataka pia kutumia kwa mita ndogo za luku ya tanesco itabidi mwenye nyumba awe anaingiza umeme mwingi kisha anawauzia wapangaji wake umeme,na pia gharama za kununua umeme ni zile zile wanazouza tanesco,View attachment 2292606
Hiko kifaa ni saparet meter maswali yangu ni haya,,
1/ Nikinunua, kimoja kinatumika, kwa, mpangaji mmoja tu?
2/ Kama ni kwa, mpangaji mmoja tu je ile buku ya kila mwezi nikitaka kununua, umeme nikiweka itakatwa?
3/ Vipi kuhusu meter kuu kama wenzangu hawajaingiza umeme na tuko giza mimi wangu nao ukaisha je nitaweza kuendelea kujihudumia umeme bila meter kuu kuwa na umeme?
4/Hii huduma je TANESCO wameipitisha? (inakubalika)
Karibuni mnipe elimu.
NB: Uzi usiunganishwe sehemu nahitaji majibu ya fasta nipate chaguo langu kabla ya maamuzi.
ASANTE!
Kuna sehemu nilipo zimefungwa izo mita kama utataka uje uzione karibu