Mbaya zaidi ni bei ya hiyo injini ya 1ZZ. 'Mswaki' ni 2mil, complete ni 2.3mil.
Niliwahi kufanya overhaul ya hiyo injini mwaka 2018. Ilisumbua baada ya hapo ila ilikuja kubainika mafundi wa awali waliruka jino moja la timing chain. Ilipofika 2022 ikaanza tena kuchoma oil. Kila baada ya wiki 2-3 unaongeza lita 1.
Nikafanya overhaul tena (ingawa fundi alishauri tuchukue 'mswaki', pesa ikawa na mipango mingine mikubwa na muhimu zaidi) iligharimu around laki 5 (parts na ufundi). Baada ya hapo kukawa na leakage ya oil. Kila asbhi unakuta oil imechuruzika chini. Ikarekebishwa tena, ikatulia. Hivi karibuni nimeanza tena kuona matone ya oil chini.
Bado ninasukuma nayo siku kabla sijavuta chombo kingine.