Mafundisho ya ndoa miezi tisa ni sahihi?

Mafundisho ya ndoa miezi tisa ni sahihi?

Vijana wa hovyo hatuishiwi mbinu ya kukimbia hiyo miezi 9. Ukweli kuna madini haswa maana kuna wakati hadi wanasaikolojia na Wanasheria wa kanisa wanaletwa kuwapigia pindi.

So twakwepaje???
Unaenda kwa paroko unamuelezea kwamba mm nafanyia kazi mkoa X. Unapewa barua ya kwenda kufanyia mafundisho hukohuko. So mikoa mingi mafundisho ni 2Weeks.
Ila njia hii ni applicable kwa sie ambao tunatembea tembea mikoa mingi
Jitahidi tuu hivyo hivyo huna namna rfk
 
Ndoa nyingine miezi 9 zimeshajifia huko.

..... Eti taja tofauti kati ya mwanamke na mwanaume ....
Ni swala pana sana ukilitafakari kwa kina ni kama vile Yesu alivyouliza mimi ni nani??? Majibu yake yanaweza kujaza pages
 
Kumbe mnafundishwa biology kabisa. kama ni hivyo wapige miaka miwili kabisa.
By the way ni namna ya upigaji, muwawezeshe maparoko kusurvive. alafu wenyewe hawaoi so kuchelewesha hata haiwahusu
Wameweka muda mrefu ili watu mpate muda wa kufahamiana na kujipanga
 
Wakuu,

Kikawaida mafundisho ya ndoa za kikatoliki hua kati ya wiki 2 mpaka mwezi 1 lakini katika jimbo XXX (Jimbo katoliki) na parokia zake zote hali ni tofauti kabisa mafundisho ya ndoa ni lazima uhudhurie kwa miezi 9. Watu wamelalama kuhusu hili lakini askofu wala hana habari sana paroko atakwambia kama hujarizika na utaratibu hama Makanisa mengine.

Since utii ndio nguzo ya ukatolikii watu inabidi tuwe wapole tutii...yaani unahudhuria mafundisho mpaka unaweza kuachana bure na mchumba wako mkiwa bado mpo kwenye mafundisho.

Lakini vijana wa hovyo hovyo wamebuni mbinu ya kukwepa miezi hiyo ya mufundisho. Ambayo sitaisema Ili kama paroko au askofu husika akisoma mada hii asigundue siri za kambo😅

___

Unaweza kujiuliza miezi tisa yote hiyo wanafundishwa vitu gani? Wanafundisha vitu viiiingi sana, hadi wanasaikolojia kama Carl Jung na Maria Montessori wanawasoma. Baadhi ni topic zifundishwazo
  • Saikolojia, hasa maswala ya Personalities
  • Reproduction
  • Genetics
  • Malezi ya mtoto from prenatal to postnatal Stage
  • Uzazi wa mpango
  • Sheria za ndoa KiKatiba
  • Sheria za ndoa Kikanisa
  • Jinsi ya kumuandaa na kumlizisha mwenza wako kitandani 🤣🤣🤣🏃🏃🏃
  • Nk..
Halafu kuna mtihani na nilazima ufaulu... Nongekua na soft copy ningewawekea mjisomee.
Chini hapo nitaweka baadhi ya maswali yanayoulizwa kwenye paper.

Wakuu swala hili ni swa kweli jamani kufuata mafundisho kwa muda wote huo?

View attachment 2737753
View attachment 2737755
Ukitoka hapo kafanye mgihani wa Biology na Civics unachukua score ya A🤣
 
Katoliki ni wanoma sana.. nimegundua faida ni nyingi za miezi yote hiyo
Wanaziba pengo la mafundo ya unyago.

Juzi nimenunua Biblia walioichapisha Paulines Publication ya Katoliki. Fahrasa kaandika Pengo in da house.

Biblia ya kiswahili. Pamoja na mazonhe yao lakini jamaa wana mambo adimu kwenye elimu na machapisho ya kiimani
 
Wanaziba pengo la mafundo ya unyago.

Juzi nimenunua Biblia walioichapisha Paulines Publication ya Katoliki. Fahrasa kaandika Pengo in da house.

Biblia ya kiswahili. Pamoja na mazonhe yao lakini jamaa wana mambo adimu kwenye elimu na machapisho ya kiimani
Wanazingua sana mafundisho yao yana muda maalumu. Yaani yanaanza August to may. Ukichelewa huo muda ndio usubir mwaka mwingine inaboa sana
 
Katoliki ndoa mnafundishwa ndoa na mapdri wasioo

Wabajua nini? Kuhusu ndoa ? Utafundishwa mafundisho ya ndoa na asiyejua ndoa?
Usiskize stori za vijiweni. mafunzo yanatolewa na wataalam mbalimbali. Tena wengi wao hata sio mapadri kabisa
 
Usiskize stori za vijiweni. mafunzo yanatolewa na wataalam mbalimbali. Tena wengi wao hata sio mapadri kabisa
Wakifundisha Saikolojia wanakuja wataalam wa Saikolojia. Hadi wataalam wa afya wanakuja. Ndio maana hafundishwi mtu mmoja bali linakua darasa kabisa. Mkimaliza mafundisho kuna graduation eti😂
 
Back
Top Bottom