Mafuriko makubwa mjini Ifakara leo Mei 5

Mafuriko makubwa mjini Ifakara leo Mei 5

Hali ni mbaya. Maji ni mengi mji wa Ifakara kwa 80% upo kwenye maji.

Hasara ni kubwa haswa kwa wafanya biashara za hardware. Cement na gipsam zimeharibika kwa kiwango kikubwa.

Kuna baadhi ya familia zinahitaji msaada.

Mtuombee.
Mji wa Ifakara unapaswa kuhamishwa hapo na kupelekwa maendeleo ya milimani juu ya uwanja wa ndege.
 
Daraja Pekee linalopitisha maji ya Mto Lumemo toka eneo linalojulikana kama kwa Shungu mjini Ifakara.

Muda mfupi uliopita kabla maji hayajaanza kupita Juu ya Daraja hili.
 
Hali ni mbaya. Maji ni mengi mji wa Ifakara kwa 80% upo kwenye maji.

Hasara ni kubwa haswa kwa wafanya biashara za hardware. Cement na gipsam zimeharibika kwa kiwango kikubwa.

Kuna baadhi ya familia zinahitaji msaada.

Mtuombee.
Tulikuwa mei mosi hapo weka picha na maandamano tumefanya
 
Hapana.

Mto Lumemo una Kona kali sana na mara nyingi mto Kilombero ukikataa kupokea maji ya mto Lumemo, ndipo mafuriko hutokea.

Ingawa maji ya mwaka huu ni mengi sana kwa zaidi ya miaka 50 hayajapata kuonekana kwa simulizi wa wakongwe wa eneo hili.
Kuna watu hawajui maana ya mafuriko ni nini. Wanafikiri ni mvua tu ya kuondolewa na simple drainage system.
 
Kuna watu hawajui maana ya mafuriko ni nini. Wanafikiri ni mvua tu ya kuondolewa na simple drainage system.
Tatizo ndiyo Hilo.

Mafuriko maana yake ni mifumo ya kutoa na kusafirisha maji inazidiwa na wingi wa maji uliopo kwa wakati husika.
 
Yes, ni uzembe utokanao na short-sighted mind. Japan Sasa hivi kwenye mji wa Fukushima-Daichi na Fukushima-Daini wameanzisha mradi mkubwa wa kujenga ukuta/ukingo imara na madhubuti kabisa ili kuzuia maji ya bahari yasifurike kwenye miji hiyo endapo kama itatokea tena Tsunami ya hatari Kama ile iliyotokea mwaka 2011 ambayo iliua watu zaidi ya elfu arobaini sambamba na kuharibu kabisa zaidi ya 70% ya miji hiyo.
Hii kali
 
Poleni watu wa Ifakara, Afrika nayo inafikiwa taratibu baada ya Asia, Ulaya na Amerika. Hizi natural hazards tuombe tu zikae mbali na sisi.

Nilikuwa najaribu kufikiria upepo wa 100km/hr sikupata majibu, upepo wa namna hiyo ukiichapa Dar es Salaam tumekwisha kwa asilimia 50%, ukiambatana na mvua ndio kabisa we'll be gone by 70%.
 
Back
Top Bottom