Kwa mara ya kwanza leo nimepanga foleni kupata mafuta lakin napo nimeyakosa
Nimekaa kwenye foleni kama dk 45 hv,baadae boss wa kituo cha mafuta akatoka ofisin na kusema mafuta yameisha akarudi ndani
Wakat huo watu wanaendelea kupewa mafuta,baadae akatoka tena na kuwaambia wafanyakaz wake kuwa mashine ikivuta upepo atawafukuza kazi,ikabid nao wasitishe kutoa mafuta
Nimekaa nikatafakar sana,mpaka nikafikiria kwanini boda boda wasijichange wakatengeneza kituo chao cha mafuta kila wilaya maana wao ndo walikuwa wamejazana pale