Mafuta ya kupikia yaadimika mitaani

Mafuta ya kupikia yaadimika mitaani

Si mnamshabikia Putin?

Tanzania inazalisha 45%ya mahitaji yake ya mafuta ya kula na huagiza 55% toka Malaysia, India na Uturuki.

Duniani mzalishaji mkubwa wa mafuta ni Ukraine, sasa baada ya uvamizi wa Urusi, Ukraine amestop uzalisha na Rassia anaemfuatia amewekewa vikwazo hivyo mafuta ya Uturuki saivi yanaenda ulaya na ya Malaysia yanaenda Japan na Korea ili kuziba pengo la mafuta ya Urusi na Ukraine ambapo hayapo sokoni. Na Korea na Japan wananunua Bei nzuri kuliko sisi

Mungu ajalie mvua Ifike mwezi wa 4 nivune alizeti yangu ni jenge.
Sijasikia hata siku moja malighafi ya kuzalishia "Korie" ama "Singida" kuagizwa toka Ukraine ama Russia!

Au wazungumzia Petrol products?
 
Sijasikia hata siku moja malighafi ya kuzalishia "Korie" ama "Singida" kuagizwa toka Ukraine ama Russia!

Au wazungumzia Petrol products?
Most ya mafuta ya kupikia yametoka nje Ila kinachofanyika hua ni kuyapaki kwenye ndio tu kwa hapa kwetu.
Viwanda vya uzalishaji mafuta singida,Kigoma ni 45%
 
Si mnamshabikia Putin?

Tanzania inazalisha 45%ya mahitaji yake ya mafuta ya kula na huagiza 55% toka Malaysia, India na Uturuki.

Duniani mzalishaji mkubwa wa mafuta ni Ukraine, sasa baada ya uvamizi wa Urusi, Ukraine amestop uzalisha na Rassia anaemfuatia amewekewa vikwazo hivyo mafuta ya Uturuki saivi yanaenda ulaya na ya Malaysia yanaenda Japan na Korea ili kuziba pengo la mafuta ya Urusi na Ukraine ambapo hayapo sokoni. Na Korea na Japan wananunua Bei nzuri kuliko sisi

Mungu ajalie mvua Ifike mwezi wa 4 nivune alizeti yangu ni jenge.
Namshabikia Putin Tena Sana,
Na kwenye hili wala msingizie, mafuta yamepanda Bei kabla ya vita. Tuache uongouongo
 
Kuna watu wanamhujumu Mheshimiwa Rais na pengine yeye hajui hili. Kwa sasa huku mitaani mafuta ni adimu sana, na pale ambapo yanapatikana basi bei yake haishikiki. Dumu/Ndoo ya Lita 20 iliyokua ikiuzwa TZS 70,000/- mwezi wa sita mwaka jana leo inauzwa TZS 140,000/-

Aliekua Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda alipata kusema kua sababu ya kupanda huku ni kuadimika Kwa vibarua huko Malaysia sababu ya COVID-19. Kigoma inaongoza Tanzania Kwa kuzalisha chikichi, je wameweza kuchukua mazao yote yanayozalishwa pale mpaka yakaisha imebidi waagize Malaysia sasa?

Kwanini wasi encourage na ku facilitate kilimo hiki Kwa hapa Tanzania mpaka tulazimike kuagiza nje? Singida wanalima sana Alizeti, na mikoa ya kusini wanalima sana Ufuta, je mazao haya yamechukuliwa yote na bado kukawa na upungufu wa mafuta?

Haya maeneo (Singida na Mikoa ya Kusini) bado kuna mapori mengi tu, kama wanazalisha malighafi za mafuta na bado hazitoshi kwanini Serikali isiwawezeshe basi kuongeza zaidi maeneo ya kulima kwenye hayo mapori yaliyobaki ili kuongeza zaidi malighafi hizi?

Sasa kuna Hussein Bashe kwenye hii Wizara, nilidhani ni mtu Smart lakin naona nae mfumo umemmeza, amesha adopt tabia za mfumo alioko. Juzi nimemsikia akiwa mkali kweli kweli juu ya kupanda Kwa mbolea kutoka 108,000/- Kwa gunia mpaka 140,000/-, lakini nimkumbushe tu hata hiyo 108,000/- bado tunapigwa, kwani hapo kabla ilikua haizidi 60,000/-

Mafuta Sasa hayako tena mitaani, wenye vigenge/duka wanasema Kwa yalivyopanda bei hata wakiyaleta hawajui watauzaje. Mafuta yanagusa kila mtu, isije ikawa ni bomu linategwa kwenye most consumable products ili likilipuka liguse sehemu kubwa ya watu. Zama hizi za "Kazi Iendelee" tunashuhudia mfumuko mkubwa wa Bei.
Sasa wewe unakuja na suluhisho la mda mrefu badala ya suluhisho la mda mfupi.

Hakuna anaemhujumu bali demand ni kubwa kuliko supply,na hujataja ni mafuta yapi hayo.

Kama ni ya kula sio lazima utumie ya alizeti bali tumia mengine.

Bei hiyo ndio iliyopo mtaani na hayajaadikika ila yamepanda.
 
Namshabikia Putin Tena Sana,
Na kwenye hili wala msingizie, mafuta yamepanda Bei kabla ya vita. Tuache uongouongo
Ngoja nikupe mfano
Miaka yote mafuta ya alizeti kwa singida huwa 50k Hadi 75k kwa January Hadi April.Baada ya Covid19 November 2020 dumu lilifika 100k na Last season dumu lilianzia 75k Hadi 110k kwa September 2021

Lakini baada ya Putin kuvamia Ukraine yamefika 140k na kwa sisi wakulima wa alizeti tunataka yafike 200k kabisa
 
Kazi iendelee...
Mama anaupiga mwingi sana...
Muacheni mama apige kazi...
Hakuna kama Samia ndani ya miezi 6 tu....

Kupata vibonzo vingine kama hivi bonyeza CM 1774858 ama Mtanzania Halisi2021
Tulia wewe mama afungue Nchi,kulalamika hakutafanya bei ipungue.

Demand ya mafuta ni kubwa kuliko uzalishaji na mnavyozidi kuzaa ndio mtajua hamjui.
 
Ngoja nikupe mfano
Miaka yote mafuta ya alizeti kwa singida huwa 50k Hadi 75k kwa January Hadi April.Baada ya Covid19 November 2020 dumu lilifika 100k na Last season dumu lilianzia 75k Hadi 110k kwa September 2021

Lakini baada ya Putin kuvamia Ukraine yamefika 140k na kwa sisi wakulima wa alizeti tunataka yafike 200k kabisa
Unajua hapa ndio wengi mnafeli, wewe unalima alizeti unasema dumu lifike 200k ili upate pesa nyingi, sawa Ila hapohapo ukienda kununua vitu vya kukaangaa utavinunua kwa Bei kubwa. Unarudi pale pale
Inflation inakuongezea pesa nyingi mfukoni, alafu hapohapo inachukua nyingi mfukoni kwako kununua mahitaji
Mfano mwingine
Ni Bora ulipwe laki 3 kwa mwezi alafu chakula ununue kwa kwa laki 2, au ulipwe laki 2 alafu chakula ununue kwa elfu hamsini?
 
Sasa wewe unakuja na suluhisho la mda mrefu badala ya suluhisho la mda mfupi.

Hakuna anaemhujumu bali demand ni kubwa kuliko supply,na hujataja ni mafuta yapi hayo.

Kama ni ya kula sio lazima utumie ya alizeti bali tumia mengine.

Bei hiyo ndio iliyopo mtaani na hayajaadikika ila yamepanda.
Kuanzia Juma tatu iliyopita, bei ya mafuta takribani aina zote imelingana.
 
Nchi kama malaysia walijikita kwenye kilimo cha chikichi ambapo mbegu walitoa kigoma, leo hii wana export kwenye soko la dunia mafuta ya chikichi kama hawana akili nzuri, pale kigoma waha wanazubaa na michikichi yao..........bongo kufanya initiatives zenye maslahi mapana na ya kudumu ni mtihani.
Hii inchi ina laana..kuanzia viongozi hadi wanachi wenyewe..

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom