Ni kweli kabisa mkuu, ila n bora uwepo wake kuliko kama asingekuwepo
US ana haribu sana stability ya dunia hasa middle East.Kule alisema Sadam ana nuclear ,kumbe hana kaangamiza raia kibao,inchi haitawaliki magaidi kule Iraq wanajiachia, Tony Blair anajuitia hii mistake mpaka kesho. Ukija Gazza,mataifa yote (98+) yanataka vita isitishwe yy na UK hawataki tu kwa ajili ya maslahi yao.Kwenye baraza la Ulinzi la UN kura zishapigwa mara tatu,US kakataa mpaka Malaysia wanataka kudiscuss hii kura ya veto na kutaka itizame upya kwani kuna mataifa wanaitumia vibaya.
Obama anakwambia ktk mistakes zake kubwa ni kuivamia Libya, ambaye ukiangalia hakuwa na kosa lolote, matokeo yake magaidi wamejazana kibao Libya sababu inchi haitawaliki. Ukienda Yemen, US ana misheni nyingi za kijeshi ambazo za kimya kimya ambazo zimeangamiza raia wengi wasio na hatia, hili lilifichuliwa na BBC.
Manake utasema labda ni demokrasia ila Saudi hamna demokrasia ila hamgusi sababu ana maslahi makubwa ya kiuchumi na Saudi may be wamemwacha sababu wanajua ni mzee wa fitina. So ukitizama sehemu yoyote ambayo US,anataka kuiba au kujinufaisha kwa ajili ya maslahi yake na kiongozi wa hiyo nchi akakataa lazima ataleta zengwe. Vita zote alizopigana US,kapigana kwa ajili ya maslahi ya taifa lake ni si kwa ajili ya taifa hilo.
Kitendo cha kiongozi yoyote kujitambua kwamba anaibiwa na US,basia ajiandae kuwa adui wa US kwani ataundiwa zengwe, fitina na hata kuuliwa Assad yupo pale kwa mkono wa Putin la sivyo yy angeondolewa na kupotezwa kama ilivyokuwa kwa Sadam na Ghadafi na huwaga hajali maamuzi ya mabaraza ya UN wala hizi taasisi za haki za binadamu.
Afrika haijawahi kunufaika na ushirikiano na US au EU,kwani kwa mujibu wa Al Jazeera walipo fanya uchunguzi wao jinsi wa fedha zinavyo ibiwa na kufichwa huko Shelisheli kwa kushirikiana na hawa viongozi wetu wanao kubalika na nchi za magharibi,kiwango tunacho pewa Afrika kama msaada,kichukue then kizidishe mara kumi ndipo utapata hela inayo pigwa Afrika na nchi za magharibi kwa kushirikiana na viongozi wetu wa Afrika.