Magari ambayo unaweza kuendesha miaka 15 bila shida kubwa

Sniper

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2008
Posts
1,957
Reaction score
827
MwanaJF,

Naomba tujadili magari magumu zaidi kwa mazingira ya Tanzania. Magari ambayo unaweza ukaendesha zaidi ya miaka 15+ bila shida kubwa kubwa. Services za kawaida na replacement ndogo ndogo.
Kwa uzoef wangu naona yafuatayo

1. Toyota Carina Ti
2. Rav 4 old model
3. Suzuki Escudo
4. Toyota Hilux
5. Land Rover Defender 110

Naomba tuendeleze list
 
Isuzu injection
 
We nunua toyota au Nissan any car old model... 2005 kurudi nyuma ...

Hizo utadumu nazo kama ndoa katoliki...

Sema zinaboa kwenye mwendo, ila kama una advanced age sio issue .. hapo ni wewe tu na maji yako kwa Radiator (rejeta), na Ku change oil...
Mengine muachie Mungu.
 
Magari ambayo unaweza ukaendesha zaidi ya miaka 15+ bila shida kubwa kubwa. Services za kawaida na replacement ndogo ndogo.
Kwa uzoef wangu naona yafuatayo

1. Toyota Carina Ti
2. Rav 4 old model
3. Suzuki Escudo
Carina is the BEST of all.

Carina SI, Carina TI na Baba lao Carina GT turbo.

Hizi ni gari ambazo unaweza badilisha OIL mara mbili kwa mwaka na ikapiga mzigo fresh (ROHO YA PAKA), Safari ndefu unaenda nayo bila wasiwasi, Ikiharibia popote huwezi kosa spea zake(kijiji chochote ambacho watu wanamiliki magari basi huwezi kosa spea za Carina). Vilevile unaweza itumia Kibiashara na matumizi binafsi.

Ni moja ya gari za zamani zinazovumilia mazingira ya Mtanzania.

Hii hapa chini ni Carina GT, zipo chache sana hapa mjini. Unaweza kaa mwezi usikutane nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…