Magari ambayo unaweza kuendesha miaka 15 bila shida kubwa

MwanaJF,

Naomba tujadili magari magumu zaidi kwa mazingira ya Tanzania. Magari ambayo unaweza ukaendesha zaidi ya miaka 15+ bila shida kubwa kubwa. Services za kawaida na replacement ndogo ndogo.
Kwa uzoef wangu naona yafuatayo

1. Toyota Carina Ti
2. Rav 4 old model
3. Suzuki Escudo
4. Toyota Hilux
5. Land Rover Defender 110

Naomba tuendeleze list
Kwenye defender 110/90 weka toleo kabisa maana zenye roho ya uvumilivu ni tdi 200/300 zingine hamna kitu labda mbio mfano puma.
 
Wale wa City bus (daladala) msimsahau mchizi DCM, japo hayupo mtaani na wale wa Transit (malori) msimsahau Mzee FIAT
Aisee DCM sijui jamaa waliiundaje, madude hayafi kirahisi rahisi yanadunda tu miaka na miaka
 
Mkuu,

Haya magari unaendesha miaka 15 gari moja hiyo hiyo au unakuwa na gari zaidi ya moja siku nyingine unayapumzisha?

Maana ukiwa na gari zaidi ya moja siku nyingine unaipumzisha gari ya kwanza unatumia ya pili gari zinaweza kudumu sana kwa sababu zinagawana kazi.
Gari haichoki Mkuu, labda wewe mtumiaji ndio uichoshe.

Huwa sijui kwanini watu wanawaza kutumia sana gari inachoka.

Fanya service kwa wakati, na matengenezo pale unapohisi dosari.

Gari sio kiumbe hai useme kinahitaji kupumzika.
 
Ukishasema "fanya service" ushakubali gari inachoka, ndiyo maana unafanya service.

Gari ingekuwa haichoki usingehitaji kufanya service.

You are contradicting yourself.

Na hiyo service unayoisema, ikiwa unatakiwa kufanya service kila baada ya km X, ukiwa na magari mawili unabadilisha badilisha kutumia, kuzifikia hizo km X itakuchukua muda zaidi ya ukiwa na gari moja unalitumia kila siku.

Huelewi wapi hapo?
 
Kwanini uingie gharama yote hiyo ya kumiliki magari mawili kwa kisingizio cha kukwepa gharama ya service ya gari moja wakati gharama ndio inapanda zaidi?.

Gari halichoki na hata vipuri havichoki bali vipuri na gari lisilotunzwa vinachakaa na sio kuchoka.

Ukifuata maelekezo yaliyopo kwenye kitini cha gari husika linaweza kudumu hadi miaka 100.
 
Siingii gharama. Kuwa na gari la backup ni jambo standard katika maisha.

Tatizo unaishi maisha ya kimasikini halafu unafikiri kuishi maisha standard ni anasa na gharama.

Nyumba kuwa na gari moja maana yake Baba akiwa anaendesha hilo gari Mama hawezi kufanya shughuli nyingine za kutegemea gari mpaka Baba arudi.

Hayo si maisha standard, ni umasikini tu.
 
Tunapoteana sehemu moja ndogo tu ya hoja ya kuwa na gari mbili ili kuepuka gharama za matengenezo kwa kutokuchosha gari.

Hoja haikuwa kwenye haya uliyoyaleta sasa hivi.

Na pia usiweke kanuni ya jumla ya familia. Wako watu single wengi wenye magari hivyo hiyo hoja ya mama kukosa gari ni dhaifu na sio standard ya jumla ya maisha. Kuna watu tunaishi wenyewe (single).

Kanuni ni moja gari anakuwa nalo mtu mwenye matumizi nalo, wala sio lazima sana kuwa na gari ikiwa mizunguko yako haiathiriwi na kutokuwa nalo.

Turudi kwenye hoja ya msingi, kwa hiyo unakubaliana na mimi kuwa kuwa na gari mbili hakupunguzi gharama za matengenezo?
 
Tangu mwanzo sijaongea gharama nimeongea gari kudumu muda mrefu.

Ukiwa na gari zaidi ya moja all other things remaining equal gari zina uwezo wa kudumu miaka mingi, kwa sababu zinapokezana kazi huendeshi gari moja kila siku. Hapo kuna kitu gani huelewi?

Hata ukiwa single kuwa na gari la backup ni muhimu kwenye standard life.

Watu wengi wangekuwa na uwezo wangekuwa na gari zaidi ya moja.

Wengine wana gari la kazi na gari la starehe. Gari la safari ndefu na gari la misele ya mjini tu.

Sema wengi hawana uwezo tu.

Sasa unachobisha kipi hapo?
 
MwanaJF,

Naomba tujadili magari magumu zaidi kwa mazingira ya Tanzania. Magari ambayo unaweza ukaendesha zaidi ya miaka 15+ bila shida kubwa kubwa. Services za kawaida na replacement ndogo ndogo.
Kwa uzoef wangu naona yafuatayo

1. Toyota Carina Ti
2. Rav 4 old model
3. Suzuki Escudo
4. Toyota Hilux
5. Land Rover Defender 110

Naomba tuendeleze list
Passo?
 
Back
Top Bottom