Magari ambayo unaweza kuendesha miaka 15 bila shida kubwa

Magari ambayo unaweza kuendesha miaka 15 bila shida kubwa

Carina old model ni roho ya paka
 
Wazambia na Wamalawi wanaona kama tumerogwa kutokupenda magari mazuri na magari yao mazuri mengi yanapita hapa kumbe sisi mchawi wetu ni TRA ndio maana leo hii tunazungumzia gari za mwaka 2000.
TRA ni tatizo
 
Hilux 2001, Km468125, full Ac… Gari ina 20 yrs bongo na bado msumari
 

Attachments

  • IMG_3990.jpeg
    IMG_3990.jpeg
    806.2 KB · Views: 5
Vitz RS old model utakaa nayo hata miaka 20
 
aisee brother natafuta hizi chuma.
Zipo sema changamoto kupata ambayo imetunzwa vizuri ndio kipengele…Halaf pia kwa kiasi pia pick up hasa za zamani huwa ni nadra kukuta zinauzwa, unaweza ukaipata lakini utakuta imechoka sana…Kuna page ya Insta inaitwa Mjerumani mweusi huwa naonaga mara moja moja anazipost, unaweza ukapreview humo
 
Yaani ukiwa na akili za kimasikini jamani balaa. Yaani ni sawa na kuniambia ninunue shati la kudumu miaka 10 hahaha kama huna hela utaanza kifikiria hivyo
We ni maskini pia ila kujifaragua tu.Zaidi ya kumiliki gari za mitumba Gari mpya unaushia kuiona kwa TV tu.

Unaweza kuta wewe ni fukara ila mwenzio maskini
 
Kwanini uingie gharama yote hiyo ya kumiliki magari mawili kwa kisingizio cha kukwepa gharama ya service ya gari moja wakati gharama ndio inapanda zaidi?.

Gari halichoki na hata vipuri havichoki bali vipuri na gari lisilotunzwa vinachakaa na sio kuchoka.

Ukifuata maelekezo yaliyopo kwenye kitini cha gari husika linaweza kudumu hadi miaka 100.
Nahisi unabishana na toto la form two.
 
Back
Top Bottom