Magari ambayo unaweza kuendesha miaka 15 bila shida kubwa

Wazambia na Wamalawi wanaona kama tumerogwa kutokupenda magari mazuri na magari yao mazuri mengi yanapita hapa kumbe sisi mchawi wetu ni TRA ndio maana leo hii tunazungumzia gari za mwaka 2000.
Lakini pia, wengi wetu tunaendekeza sana umasikini. hata wanaopata misamaha ya kodi, bado wanapambana na 2010
 
Mkuu,

Haya magari unaendesha miaka 15 gari moja hiyo hiyo au unakuwa na gari zaidi ya moja siku nyingine unayapumzisha?

Maana ukiwa na gari zaidi ya moja siku nyingine unaipumzisha gari ya kwanza unatumia ya pili gari zinaweza kudumu sana kwa sababu zinagawana kazi.
 
Lakini pia, wengi wetu tunaendekeza sana umasikini. hata wanaopata misamaha ya kodi, bado wanapambana na 2010
Wengi hawataki kulipa kodi maana gari nyingi kodi zake ni 18m mpaka 28m gari nzuri kabisa ila utawaona nao wapo kwenye gari za kawaida harafu zimefika kwa gharama kubwa tu.
 
Nimeangalia TRA Ford a ranger wildtrak ya 2022, kodi 33+M, kweli hii serikali haina huruma. Imagine 33M!,!
Ndio maana magari mengi watu wanakwepa kulipa kodi ipo Land Cruiser ya kawaida tu ya 2022 kodi inasoma 79m...nilichukua Wildtruck ya 2018 kodi ilikua inasoma chini ya 20M ingawaje sokoni ningeweza kuchukua Ford ya 2023..wildtruck ya 2016 kodi ni 23+M.kwenye magari ya mizigo ndio hatari na mizigo ipo ya kumwaga Tanzania mingine inaoza huko mashambani ni kama tumerogwa..
 
Na hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa.

Mfano gari za zamani kwa masafa marefu ni nzito pia hazina matumizi mazuri ya mafuta n.k Lakini Kwa purukushani za hapa na pale Kwa sisi watu wa kazi zinatufaa sana
Ukiwa na pliers, bisibisi na copper wire haulali porini .
 
Kiukweli wasomi wetu wanahitaji kuwa innovative kwenye swala la kodi. Wao kila siku ni kuongeza ushuru kwenye, magari, pombe na sigara! ushuru wa Audi Q5 ya 2020 50+M!!!!!!!!!

Imagine mtu unanunua gari ya 2010.. hiyo ni 15 years. Na ndo tunasema ni new model…

Halafu uniambie kwamba ufisadi unaweza kuisha bongo?
 
Toyota Harrier old model roho ya paka, jinsi kulivyo na shida ya maji huwa nabebea madumu ya maji.
 
Ukitaka ucheke angalia Mercedes benz saloon ya 2016 mpaka 2022 hizo kodi zake za ajabu wakati hizo gari huko sokoni bei chini tu.Tipper Fusso ndogo hizi za mwaka 1998 zinafika kwa 80m bajaji miguu mitatu mpaka inafika eti 10M mpaka 11M kama sio utani ni nini huo..wakati huo huo gari zao nyingi za 2024 zinaingia kwa msamaha wa kodi baadae zikitokea ajali kwa haya magari chakavu wanajifanya kusema chanzo ni mwendokasi tu.
 
Yaani ukiwa na akili za kimasikini jamani balaa. Yaani ni sawa na kuniambia ninunue shati la kudumu miaka 10 hahaha kama huna hela utaanza kifikiria hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…