Magari ya viongozi wa Serikali na afya za wananchi wa Tanzania kipi muhimu?

Mnasahau kuwa kupitia bima ya nhif mtu anaweza kufanyiwa hadi upasuaji lkn hii hamuongelei kwa nn mnazi kwa kiasi kdg hicho ndio kinafanya mtu apate huduma hiyo lahasha bali umoja wetu wa kutoa michango ndio inawasaidia wagonjwa walio wengi ndio mana tuhimizane kutoa michango
Hueleweki hata umeandika nin ndio asali imekulevya
 
Juzi kati natoka dodoma naenda moro,nakuta hard body 75 za ma DAS zimepaki zinaenda dodoma,nikasema kumbe nchi hii sio masikini,
 
Kuna hoja zingine bana yaani unaziona zina uchuki na Wivu ndani yake kwani suala la magari halihusiani kabisa sababu huu ni usafiri kama usafiri mwingine ni sawa na kusema mtu aache kula sababu hana nguo za kubadilisha.
Hoja hii jamani imeshaelezewa mara nyingi sana na kutolewa ufafanuzi nikusema tu kama tumejizima data watoto milioni 30 wamejiunga laki 2 unadhani Mfuko utaweza kujiendesha lakini suala la Bima ya Toto Afya kadi limeelezewa vizuri Bima imehamishiwa Upande wa Shule watoto wakajiunge kwa bei ile lakini haukatazwi kumkatia Mtoto kifurushi pamoja na Wazazi
 
Mnyonge Mnyongeni haki yake Mpeni #NHIF haina mazuri hata kidogo ama tunashindwa kusema ukweli kwa sababu ya Chuki ,Ukifika hospitalini Wamama wanasema yaani kama tusingukua na #Bima hapa tungepata shida hivyo tunaona hayo ndo mazuri ya Bima sijui tumerogwa wapi

Pamoja na kelele zote hizi #BimayaNHIF ndio kimbiliooo la wengi tuwapongeze kwa kidogo chao
 
Mhubiri 8:9
"Mwanadamu amemtawala mwanadamu MWENZAKE KWA KUMUUMIZA".
 
MASIKINI ATABAKI KUWA MASIKINI na tajiri atatajirika zaidi aliimba msanii Jaguar toka Kenya. Msemo huu unaonekana kukita mzizi nchini Tanzania.

Tanzania inatumia bilioni 558 kwa mwaka kununua magari ya viongozi! Hatujapigia mahesabu gharama za vipuri,matengenezo na mafuta ya bure wanayopewa viongozi!

Wakati unatafakari hilo unashangaa kusikia, mfuko wa Taifa wa bima ya afya NHIF hauwezi kulipia pesa za matibabu Shilingi za kitanzania Bilioni 40?
Je magari ya viongozi ni muhimu kuliko afya za watanzania?

Viongozi wanaopewa magari wana mishahara mizuri ya kuweza kumudu bima ya afya kwa mwaka mfano, mshahara wa mbunge kwa mwezi ni zaidi ya Shilingi Milioni 14 ,lakini wanapewa bima ya bure, matibabu bure mafuta na magari bure ilhali mwalimu wa mwezi mzima anaambulia 500,000 ikiwa na makato !

Makada mtasema ni uchochezi na maneno mengi lakini hali hii inakera hivi mtu kama Abood anahitaji kupewa bima ya bure? Au Mwigulu au Makamba? Ummy Je hawezi kumudu bima ya afya au?

Inakuwaje basi unamlipia Shabiby bima ya bure halafu mwananchi wa kawe unamwambia achangie? Hivi viongozi wa Taifa hili mnashindwa kuweka maisha ya watanzania mbele??

Kila mwezi mnakusanya Bilioni 80 kwenye tozo za miamala kwa mwaka ni Sh 960 Bilioni pesa hii hamuwezi kuipunguza kwa NHIF ishughulikie matibabu ya watoto wa wapiga kura wenu?

Kama NHIF haiwezi kuja na strategy ya kuleta bima ya afya kwa wananchi basi muibinafshishe kwa DP WORLD

NB:Unavyokuja kucomment usihusishe vyama vyenu hapa. Sijataja chama cha mtu hapa
Muhimu CCM kwanza
 
Africa hii ndugu yangu.
Gari Moja kwa mwaka inagharimu hata millioni 50 mpaka 100 kuifanyia service, mafuta na matengenezo.
Haya Kuna magari mangapi?
 
MASIKINI ATABAKI KUWA MASIKINI na tajiri atatajirika zaidi aliimba msanii Jaguar toka Kenya. Msemo huu unaonekana kukita mzizi nchini Tanzania.

Tanzania inatumia bilioni 558 kwa mwaka kununua magari ya viongozi! Hatujapigia mahesabu gharama za vipuri,matengenezo na mafuta ya bure wanayopewa viongozi!

Wakati unatafakari hilo unashangaa kusikia, mfuko wa Taifa wa bima ya afya NHIF hauwezi kulipia pesa za matibabu Shilingi za kitanzania Bilioni 40?
Je magari ya viongozi ni muhimu kuliko afya za watanzania?

Viongozi wanaopewa magari wana mishahara mizuri ya kuweza kumudu bima ya afya kwa mwaka mfano, mshahara wa mbunge kwa mwezi ni zaidi ya Shilingi Milioni 14 ,lakini wanapewa bima ya bure, matibabu bure mafuta na magari bure ilhali mwalimu wa mwezi mzima anaambulia 500,000 ikiwa na makato !

Makada mtasema ni uchochezi na maneno mengi lakini hali hii inakera hivi mtu kama Abood anahitaji kupewa bima ya bure? Au Mwigulu au Makamba? Ummy Je hawezi kumudu bima ya afya au?

Inakuwaje basi unamlipia Shabiby bima ya bure halafu mwananchi wa kawe unamwambia achangie? Hivi viongozi wa Taifa hili mnashindwa kuweka maisha ya watanzania mbele??

Kila mwezi mnakusanya Bilioni 80 kwenye tozo za miamala kwa mwaka ni Sh 960 Bilioni pesa hii hamuwezi kuipunguza kwa NHIF ishughulikie matibabu ya watoto wa wapiga kura wenu?

Kama NHIF haiwezi kuja na strategy ya kuleta bima ya afya kwa
 
Wakati unatafakari hilo unashangaa kusikia, mfuko wa Taifa wa bima ya afya NHIF hauwezi kulipia pesa za matibabu Shilingi za kitanzania Bilioni 40?
NHIF inalipa kwa mahospitali Bilioni 40 kwa saa, kwa siku, kwa mwezi, kwa mwaka ???
 
Kulingana na Waziri wa afya, makusanyo yalikuwa 5 bilioni wakati NHIF ililipa 40,bilioni hivyo kuna upungufu wa 35bilioni Kwa mwaka
(I stand to be corrected)
 
MASIKINI ATABAKI KUWA MASIKINI na tajiri atatajirika zaidi aliimba msanii Jaguar toka Kenya. Msemo huu unaonekana kukita mzizi nchini Tanzania.

Tanzania inatumia bilioni 558 kwa mwaka kununua magari ya viongozi! Hatujapigia mahesabu gharama za vipuri,matengenezo na mafuta ya bure wanayopewa viongozi!

Wakati unatafakari hilo unashangaa kusikia, mfuko wa Taifa wa bima ya afya NHIF hauwezi kulipia pesa za matibabu Shilingi za kitanzania Bilioni 40?
Je magari ya viongozi ni muhimu kuliko afya za watanzania?

Viongozi wanaopewa magari wana mishahara mizuri ya kuweza kumudu bima ya afya kwa mwaka mfano, mshahara wa mbunge kwa mwezi ni zaidi ya Shilingi Milioni 14 ,lakini wanapewa bima ya bure, matibabu bure mafuta na magari bure ilhali mwalimu wa mwezi mzima anaambulia 500,000 ikiwa na makato !

Makada mtasema ni uchochezi na maneno mengi lakini hali hii inakera hivi mtu kama Abood anahitaji kupewa bima ya bure? Au Mwigulu au Makamba? Ummy Je hawezi kumudu bima ya afya au?

Inakuwaje basi unamlipia Shabiby bima ya bure halafu mwananchi wa kawe unamwambia achangie? Hivi viongozi wa Taifa hili mnashindwa kuweka maisha ya watanzania mbele??

Kila mwezi mnakusanya Bilioni 80 kwenye tozo za miamala kwa mwaka ni Sh 960 Bilioni pesa hii hamuwezi kuipunguza kwa NHIF ishughulikie matibabu ya watoto wa wapiga kura wenu?

Kama NHIF haiwezi kuja na strategy ya kuleta bima ya afya kwa wananchi basi muibinafshishe kwa DP WORLD

NB:Unavyokuja kucomment usihusishe vyama vyenu hapa. Sijataja chama cha mtu hapa
Bima ya Afya ni suala la kila mmoja, hivyo tuendelee kuhimizana kila mmoja ajiunge kugharimia matibabu. Kwa upande wake, NHIF imeandaa vifurushi ambavyo mwananchi anaweza kujiunga kwa kutegemea umri wake, idadi ya wanufaika katika familia na mahitaji ya huduma kuanzia TZS 192,000 kwa mwaka.
 
ukijifanya mzalendo sana hii nchi utakufa masikini najua hata ungekua wewe ungepiga tu
mtumishi wa bwana hula madhabahuni hatukatai,ndio sababu the big 5 wanaangaoiwa kutunzwa mpaka kufa,lakini sio hao peke yao wapo na baadhi ya watu ni serikali inahusika nao mpaka wafe,ila wanachotufanyia hata shetani anashangaa.

kwa hulka zao hata katiba ingesema watunzwe wao,walipwe milioni 50 kil mwezi baad ya kustaafu,bima kubwa za matibabu na mishahara milioni 5 kwa kila memba kwa koo zao zote,bado wangetupiga tu.

mlafi hana shukrani.
 
Back
Top Bottom