Magari yote ya kubeba maiti yatakiwa kulipa Tsh milioni

Magari yote ya kubeba maiti yatakiwa kulipa Tsh milioni

Maisha yanaenda kasi.Ipo siku watu watabeba miili yao wenyewe.Maana unasamehewa lile deni kule Hospital unakuja kukutana na 1m ya gari.
Mambo ni mengi sana muda nao mchache.
Heslb......wanatangazo lao lile la ndoa hahahaha
 
Duu! Hii tabu sana, mie nafkiri serikali ingetoa bei elekezi tena inayopungua ya kusafirishia maiti badala ya kutengeneza mazingira ya kuipaisha juu! Nakumbuka mwaka 2011 watu wengi waliotoka mikoa ya kusini na wagonjwa kupeleka kwa Babu wa kikombe kule Loriondo walikuwa wakiitupa miili ya ndugu zao waliokuwa wakifariki penye ile foleni ndefu na kutokomea mikoani wakiwa mikono mitupu! Hali hii ilitokana na kukosa fedha za kumudu gharama za kusafirisha miili ya marehemu wao!
 
Kwa hiyo mnataka wao wasilipe kodi au? Walipe tu!
 
Zile ndege tulizonunua kwa sifa zinaturudi sasa changisha changisha hii itazua balaa kubwa kwa serikali hii muda mfupi tu ujao, weka kumbukumbu.
 
Kila siku Serikali kupitia vitengo vyake mbalimbali wanabuni njia za kuongeza mapato.

Tozo mpya ya shilingi milioni moja kwa magari yanayokodishwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo ya kubeba miili ya marehemu inatazamiwa kupitishwa na kuanza kutumika, kumbuka tozo hiyo inayosimamiwa na (LATRA).

View attachment 1680568

Nini maoni yako mdau wa JF?
Naona ubunifu wa kuendelea kubana kengele za wtz bado unaendelea....daaah tutabinywa mpaka tuwe tunatapika kodi yaani.....uchichimame wala uchikae 🖐 tena.
 
Hali hii ilitokana na kukosa fedha za kumudu gharama za kusafirisha miili ya marehemu wao!
Hapo ☝🏾 umetoa maelezo yenye jibu, yaani mtu akifariki wafanyabishara wa magari ndipo wanapopatia mapato na ambayo hawayalipii kodi, tena huko njiani hata trafiki hawayasimamishi kisa maiti.

Nadhani kuna kitu watanzania tujifunze hapa.
 
Kama hospitali za serikali wanazuia maiti wa walishindwa kumtibu na kudai malipo hewa hili halishangazi
Mitano tena
 
Akitozwa mmachinga 20,000/- ya kitambulisho safi kabisa, akidaiwa retention fees ya mkopo wa elimu safi kabisa. Akitozwa mfanyabiashara wa kusafirisha maiti ni dhambi kisa anafanya biashara?

Acheni unafiki kodi /tozo hazitungwi bila kuangalia biashara inatengeneza faida kiasi gani na tozo liwe kiasi gani. Hiyo ni biashara kama biashara nyingine za usafirishaji zinazolipa hizo tozo (LATRA) au kisa wamegusa maiti?
Upo shihi mkuu maiti ni chanzo cha mapato cha serekali au na uongo ndugu zangu??
Serekali inatoza kodi maiti?????
 
Hii mada italeta maana km mwenye thread angedadavua yafuayo.
1. Hio kodi ni kwa trip, mwezi au mwaka?
2. Gharama wanazotoza wenye haya magari haya kwa trip zikoje, na wastani wa trips kwa mwezi upoje?

Hii itatusaidia kudadavua uwiano wa tozo za wenye magari against kodi wanayopaswa kulipa. Mfano km kwa trip wana charge 500k sidhani km 1m kwa mwaka inaumiza maana trip mbili tu keshalipa kodi baada ya hapo anahesabu faida. Na tukumbuke wanaokodi hayo magari ni wenye pesa zao ambao wako teyari ku pay more to get that premium service, sio sisi wa uswazi na vikirikuu vyetu vya 50k-100k.

Otherwise ku discuss hii mada kwa mihemko, mapovu na kisiasa bila kua na all the facts on the table haina tija yoyote ktk mjadala huu.
Kwa mwaka. Shida ni kua hizi gari zinalipa kodi na vibali vya biashara hiyo. Hii tozo mpya ya LATRA inakuja juu ya kodi/tozo nyingine hivyo kuongeza gharama za usafirishaji.
 
Kila siku Serikali kupitia vitengo vyake mbalimbali wanabuni njia za kuongeza mapato.

Tozo mpya ya shilingi milioni moja kwa magari yanayokodishwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo ya kubeba miili ya marehemu inatazamiwa kupitishwa na kuanza kutumika, kumbuka tozo hiyo inayosimamiwa na (LATRA).

View attachment 1680568

Nini maoni yako mdau wa JF?
HUo ni uchok.

Mtu akifa watu wanahangaika kujichanga laki nane ili waweze kusafirisha sasa hio 1mil ya wapi?
Anyway. Tano tena
 
Kama kodi ya mapato wanalipa kwa TRA hii ya LATRA ni double taxation. Masuala ya Kodi na tozo mbalimbali nchini yaangaliwe upya, kuna maeneo mengi sana kuna double taxation hususani Kwa wamiliki wa vyombo vya moto
 
Back
Top Bottom