Magari yote ya kubeba maiti yatakiwa kulipa Tsh milioni

Maisha yanaenda kasi.Ipo siku watu watabeba miili yao wenyewe.Maana unasamehewa lile deni kule Hospital unakuja kukutana na 1m ya gari.
Mambo ni mengi sana muda nao mchache.
Heslb......wanatangazo lao lile la ndoa hahahaha
 
Duu! Hii tabu sana, mie nafkiri serikali ingetoa bei elekezi tena inayopungua ya kusafirishia maiti badala ya kutengeneza mazingira ya kuipaisha juu! Nakumbuka mwaka 2011 watu wengi waliotoka mikoa ya kusini na wagonjwa kupeleka kwa Babu wa kikombe kule Loriondo walikuwa wakiitupa miili ya ndugu zao waliokuwa wakifariki penye ile foleni ndefu na kutokomea mikoani wakiwa mikono mitupu! Hali hii ilitokana na kukosa fedha za kumudu gharama za kusafirisha miili ya marehemu wao!
 
Kwa hiyo mnataka wao wasilipe kodi au? Walipe tu!
 
Zile ndege tulizonunua kwa sifa zinaturudi sasa changisha changisha hii itazua balaa kubwa kwa serikali hii muda mfupi tu ujao, weka kumbukumbu.
 
Naona ubunifu wa kuendelea kubana kengele za wtz bado unaendelea....daaah tutabinywa mpaka tuwe tunatapika kodi yaani.....uchichimame wala uchikae 🖐 tena.
 
Hali hii ilitokana na kukosa fedha za kumudu gharama za kusafirisha miili ya marehemu wao!
Hapo ☝🏾 umetoa maelezo yenye jibu, yaani mtu akifariki wafanyabishara wa magari ndipo wanapopatia mapato na ambayo hawayalipii kodi, tena huko njiani hata trafiki hawayasimamishi kisa maiti.

Nadhani kuna kitu watanzania tujifunze hapa.
 
Kama hospitali za serikali wanazuia maiti wa walishindwa kumtibu na kudai malipo hewa hili halishangazi
Mitano tena
 
Upo shihi mkuu maiti ni chanzo cha mapato cha serekali au na uongo ndugu zangu??
Serekali inatoza kodi maiti?????
 
Kwa mwaka. Shida ni kua hizi gari zinalipa kodi na vibali vya biashara hiyo. Hii tozo mpya ya LATRA inakuja juu ya kodi/tozo nyingine hivyo kuongeza gharama za usafirishaji.
 
HUo ni uchok.

Mtu akifa watu wanahangaika kujichanga laki nane ili waweze kusafirisha sasa hio 1mil ya wapi?
Anyway. Tano tena
 
Kama kodi ya mapato wanalipa kwa TRA hii ya LATRA ni double taxation. Masuala ya Kodi na tozo mbalimbali nchini yaangaliwe upya, kuna maeneo mengi sana kuna double taxation hususani Kwa wamiliki wa vyombo vya moto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…