Magazeti ya Mabeberu yameanza chokochoko El País wamuita John Magufuli, the African Bolsonaro. Nini kipo nyuma ya tuhuma hizi ?

Magazeti ya Mabeberu yameanza chokochoko El País wamuita John Magufuli, the African Bolsonaro. Nini kipo nyuma ya tuhuma hizi ?

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
EYguiasXkAcZIxV.jpeg

Gazeti la pili kwa uuzaji nchini Hispania El País limechapisha habari isemayo "John Magufuli the African Bolsonaro" kutokana na njia anayotumia kupambana na janga la virusi vya corona. Gazeti hilo limetaja viongozi kama Donald Trump (Rais wa Marekani) na Jair Bolsonaro (Rais wa Brazil) kama viongozi waliokataa kuchukua hatua madhubuti dhiti ya virusi vya corona.

Gazeti hilo limemtaja Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania kama kinara wa Africa kwa ukaidi, limetoa shutma kwa Rais Magufuli kwa kugoma kutoa taarifa kuhusiana na idadi ya visa na vifo vya ugonjwa huu tishio duniani. Wameongezea kwa kuponda mbinu mbali mbali kama maombi, na upimaji wa sampuli za mapapai na mbuzi katika kugundua mapungufu ya maabara ya Taifa.

Hata hivyo gazeti hilo limemsifu Rais Magufuli kwa uwezo wake wa kuchapa kazi na kutokupokea rushwa na ujenzi wa miundo mbinu mingi wakati akilitumikia taifa kama Waziri wa Ujenzi.

Source: John Magufuli, o Bolsonaro africano

Maoni yangu: Taarifa hizi si nzuri kwa sekta ya utalii na hata biashara, japokuwa tuna mapungufu katika vita hii lakini hakuna taifa lisilo na mapungufu kila moja kuna sehemu limeteleza natumaini serikali litafuatilia nini ni chanzo kwa vyombo hivi kutufanya tuonekane wazembe na kudhihakiwa na kupakwa sifa mbaya.

Lazima tujiulize ni nini kipo nyuma ya tuhuma hizi? Hii ni vita na kama alivyosema Mh. Rais leo kuna kitu zaidi lakini hawezi kukisema sasa.
 
Nani kakwambia jpm anataka kusifiwa na mambuzi dume?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sidhani kama anashida ya kusifiwa na Mabeberu lakini Rais ni alama ya taifa, shutma yoyote inaakisi taifa letu, leo hii hizi chokochoko wanazoanzisha zinafanya Tanzania isionekane salama ama kuwa na visa vingi vya ugonjwa huu wa corona. Kuna mahali wanajaribu kututingisha na kuna sababu, ukisikiliza kauli za Rais kuna kitu zaidi nyuma ya pazia lakini kwa sasa hataki kukisema. Muda utatupa majibu sahihi.
 
Leo nilikuwa nasikiliza KBC asubuhi nikasikia wanaitaja nchi moja kati ya zile za Scandinavia aidha Denmark au Norway siikumbuki inafuata hatua kama za Tanzania. Hawakuwa na lockdown wala nini, ila maisha yaliendelea. Sasa mnakuja na hoja kana kwamba Tanzania pekee ndio imefuata utaratibu huo. Acheni siasa maji taka tunataka nchi iwe na wanasiasa shupavu wenye hoja nzito zenye tija kwa jamii.

Sent from Geneva_ Switzerland
 
Kuna kitu nyuma ya pazia..kuna nchi nyingi zinadunda tone moja na Tz ila cha ajabu yenyewe ndo inafuatiliwa zaidi...Ngoja nisitie neno zaidi ila Mola akitujalia tutajua tu.
 
Hiyo lugha inaonekana nyepesi sana ingawa sijaelewa kilichoandikwa
 
Back
Top Bottom