Magufuli alikuwa na kibali kikafutwa! Rais ni kibali, anajitambua? Je, tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake ili kisifutwe, au tumuachie mwenyewe?

Yaani hapa ndio umepuyanga, nilidhani upo siriaz 🤣🤣, mada yako umeiharibu kwa kuweka mapenzi binafsi kwenye jambo lililoonekana la msingi hapo mwanzo. Uncle unaleta uchawa.
 
Amepoteza kibali hafai tena.
 
7. Somo la Saba: JPM alikuwa na kibali, Japo Kilitumika, Kilikatishwa na Kufutwa!.
Rais JPM, pia alikuwa na kibali, ila kibali chake sina uhakika kama kilikuwa ni kibali kifupi cha miaka 5 tuu, hivyo JPM alikitumia kibali chake hadi mwisho, lakini alipoamua kujiongeza kwa kuufuata mtindo wa mserereko wa CCM, kibali hicho kikaondoshwa, au pia kibali chake kilikuwa ni kibali cha miaka 10, lakini hapa katikati akatofautiana kitu na mtoa vibali, mtoa vibali akaamua kukikatisha kibali cha JPM, na kumpa Rais Samia Kibali.

JPM ana kibali, infact alizaliwa na kibali huko alikozaliwa, makuzi na mapito yake yote ni uthibitisho wa kibali. Kabla hata yeye mwenyewe hajagombea, watu humu tulishikwa sikio tukaambiwa ni JPM Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Muda wa kuchukua fomu, walijitokeza wana CCM, 62!. Kati ya hao 62, kuna watu wazuri kuliko JPM, lakini kwasababu JPM ndio alikuwa na kibali, ni JPM aliyeshinda, tukamshauri mtu wetu Elections 2015 - Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo, Vunja Kambi, Jisalimishe!

Alipoanza, nilisema humu, Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania ilihitaji Dikiteta, tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba! na tukashauri Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! hii maana yake usikute kibali chake kilikuwa ni kuinyoosha tuu nchi na kujenga mabarabara. na baada ya miaka yake 5, apumzike, watu wa kushauri tulishauri Magufuli, "Kama Unaona Kazi ya Urais ni Ngumu Kwako, Jiuzulu! ".

Kwa vile Samia alikuwa ni msaidizi wake, sisi watu wa kudurusu, tukamdurusu Samia, tukamuona ana uwezo, tukamshauri JPM term yake ya pili ampishe Samia Pascal Mayalla alitabiri mwaka 2017 kuwa Samia atakuwa Rais wa JMT baada ya 2020

Pia tulitoa angalizo muhimu Elections 2015 - Kama hii ni kweli, then serikali yetu ni serikali dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake! Alipoamua kundelea na term yake ya pili, ndio mambo yakawa kama vile, sijui ni kibali kilifutwa au!,
Nilisema mtu ukiwa na kibali ni lazima ujitambue kwanza kwa kujua kuwa una kibali, ujue ni kibali kufanya nini, na ni cha muda gani, then kitumikie kibali chako, kwa mujibu wa kibali chako na muda wako ukiisha pisha wengine, maisha yaendelee.

Miongoni mwa vitu vinavyosabisha kufutwa kwa vibali ni ukosefu wa haki kwenye demokrasia yetu na umwagikwaji wa machozi, jasho na damu zisizo na hatia, zinazopekekea kitu kinachoitwa a bad karma hivyo tulipopata fursa ya kukutana nae, tulimkabili Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

JPM alikuja kubadilika na tukampa big up
Mwishoni akabadilika, akaanza kuwa mtu mwema na kutenda matendo ya huruma
Mwisho wa siku, nikaelezwa sasa yuko zake Mbinguni Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Naombeni tumwacheni huyu baba apumzike.
P
 
8. Somo la Nane: Je Rais Samia ni Kibali?, Je Anajitambua kuwa yeye ni kibali?Anakitumia Kibali chake Ipasavyo?
Mtu wetu wa sasa ni Rais Samia.
Hoja ya kwanza ya Rais Samia, je ni Kibali?.
Jibu ni ndio, Rais Samia ni kibali, mapito yake toka alipoanza mpaka hapa alipofikia, kote kuna viashiria vyote kuwa huyu ni kibali.

Kwa vile siku hizi, kumeibuka fani ya uchawa, na watu wanaitwa machawa, hivyo ukimsifu Rais Samia kwa lolote, unaitwa chawa!, mimi mwenzenu 60 inabisha hodi, kwa umri huu kuitwa chawa sio kunitendea, naomba nikupitishe kidogo uone Samia, nilianza nae lini na nilisema nini,
Samia nilianza nae 2010 kwenye uzi huu New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa! nikaja Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material? kisha nikaja
Hivyo mtu kuniita mimi ni chawa kwa kumzungumzia Rais Samia kwasababu sasa ni rais, ni kunionea bure!

Kwa vile Rais Samia ameupata urais wa JMT kwa kudra tuu za Mwenyeezi Mungu, ili kutokea jambo kama lile kisha mtu kuukwaa urais bila kutegemea ni ishara tosha ya kuthibitisha kuwa hicho ni kibali tosha. Kama nilivyoeleza huko nyuma, aliyempa kibali, anaweza kuwa amemweleza kwanini amekifuta kibali cha mtangulizi wake, hivyo yeye anatakiwa kufanya nini kurekebisha makosa ya mtangulizi wake ambaye time frame ya kibali chake mwisho ni 2025.

Sisi Watanzania, wengi wetu ni ma simple mind, they don't have time to think, kazi yao kubwa is to discuss people, wanaofuatia ni ordinary minds, they discuss events, wachache ni great minds ambao wana discuss ideas, humu tunawaita ni ma GT, na miongoni mwa hao ma GT, wamo ma deep thinkers, mmoja wa deep thinkers hawa ni Balozi Humphrey Polepole, huyu ndie pekee aliwahi kukifafanua kibali cha Rais Samia aliposema Rais Samia, ni rais wa 6, ila anamalizia kwanza awamu ya 5 ya JPM, kisha ndipo aanze awamu yake 2025, ila kwa vile ameipokea ndani ya mwaka mmoja, hii inahesabika ni awamu ya 6, lakini ilani ni ile ile ya awamu ya 5.

Hivyo Rais Samia alipoanza, alianza vizuri kwa kuyarekebisha makosa ya mtangulizi wake, tulimpongeza, sana tuu kwa kumwandikia humu, mitandaoni, magazetini na kwenye vipindi vyetu vya Redio na TV, our expectations of her, we had very high expectations, alipokuja na zile 4R, akaunda kikosi kazi, akaja na haki jinai, maridhiano, akafutia watu kesi, kwenye haya, nyonge mnyongeni haki yake mpeni, Rais Samia anastahili kupewa maua yake.
Licha ya pongezi, karibu kwenye kila pongezi, pia kulikuwa na maombi fulani, mengine yametekelezwa na mengine bado. Haya ni baadhi ya maombi mahsus kwake
Kwa vile kibali alichoingia nacho ni cha kumalizia ngwe ya Magufuli, ule utaratibu wa mserereko wa CCM, lengo lake ni kuondoa duplicity kwenye mchakato wa usaili wa ushindani wa wagombea urais ambao walisailiwa ili kumpata the best, Rais Samia eye hakusailiwa kwa ushindani, kwa vile ameupata urais kwa kudra tuu ya Mwenyeenzi Mungu, ni kibali kimemuepushia na ushindani, hivyo 2025 ndiye mgombea wa CCM wa mserereko.

Kwenye mahojiano na Kikeke, aliposema 2025, twende na mwanamke, tumemuunga mkono ila tukamuulizia kuhusu kibali Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Sasa sijui kama kwa vile ni mimi ndie niliulizia kuhusu kibali cha Rais Samia 2025-2030, then ni mimi niliambiwa kitu kuu HII issue ya 2025.

P
 
Kusoma watasoma, kuelewa sasa🤔
 
Kibali ni nini? Samia amepigiwa kura na nani? Ana kibali toka wapi?
 
Ukisimama kwenye UKWELI na HAKI Si Rahisi kuwa na upande au kueleweka.

Labda kosa pekee alilofanya ni kuchagua kuwa kada wa CCM!!
Sio hapa tu huwa najaribu kumwagalia hata kwenye vile vipindi vyake vya saba saba kama si nane nane, naona kabisa mzee wetu anahitaji kupumzika atume tu vijana yeye abakie kwenye menejimenti.
 
Mkuu P,


Hapa umekosea sana kumwita SSH eti ni "KIBALI"; are you serious about writing this out of your independent thinking?

The president of the USA JF Kennedy once said "....Trust, but Verify" Do you clearly understand what he meant? This is your new assignment to come up with deductive reasoning.

"..Jibu ni ndio, Rais Samia ni kibali, mapito yake toka alipoanza mpaka hapa alipofikia, kote kuna viashiria vyote kuwa huyu ni kibali......" P
 
Somo la Tisa: A Way Foward- Tumsaidie ili atimize matakwa ya kibali chake kikamilifu au Tumuachie Mwenyewe na Kibali Chake?
Japo kibali, kinatolewa na Mungu mwenyewe, na kila anayepewa kibali, pia anapewa uwezo wa kutekeleza mahitaji ya kibali chake, lakini binadamu ni kiumbe dhaifu, hakuna mkamilifu hivyo kunaweza kutokea makosa ya hapa na pale, na hakuna mtu anayeweza kufanya kila kitu yeye mwenyewe, ni lazima asaidiwe, ndio maana japo Rais wetu ana kibali lakini ana wasaidizi wa kumsaidia kwenye kila eneo, na bado kunatokea makosa ya hapa na pale Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Hivyo pamoja na uwepo wa wasaidizi wa kutosha ambao ni manguli, wazoefu, wabobezi na wabebovu, lakini bado makosa yanafanyika. Na kuna watu huku mtaani, sio wabobezi, sio wabebovu lakini wana uwezo wa kusaidia. ndipo nikauliza, unapoona Rais Samia na serikali yake, imeshindwa jambo fulani na wewe umeona unaweza kusaidia, jee tumsaidie au kwa vile yeye ndie mwenye kibali, then tumuachie mwenyewe na kibali chake? WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?

Pia hapa Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!

Niliuliza humu Kumuenzi Magufuli: Tujikumbushe 'spana' za JF zilivyomsaidia Hayati Magufuli na Taifa. Je, Samia pia tumsaidie kwa 'spana' au tumkune tu tusimpare?

Pia nilishauri Tanzania tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!

Tuwakumbushe wasaidizi wake kutimiza wajibu wao kikamilifu Wasaidizi wa Magufuli walimuogopa hadi kushindwa kumsaidia, Je Wasaidizi wa Samia wanamsaidia kwa kumweleza ukweli au nao wanamuogopa? Tumsaidie au..?

Pia niliuliza Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?

Nimeendelea kusisitiza Rais Samia asaidiwe Kuna Kitu Rais Samia Amekisema Kuhusu Kurejea Kizimkazi “Post 2025”. Nashauri na Nasisitiza Wenye Uwezo Kusaidia, Tumsaidie Kumshauri Ukweli!

Na sio tuu, tunamsaidia Rais Samia kama rais wetu, bali pia tunawasaidia wale anaopaswa kufanyanao kazi ili wasipishane Tujikumbushe Kauli hii ya Rais Samia Atafanya Kazi na TLS ya Aina Gani? Hizi ni Salaam kwa Mwabu,. Swali ni is He A Bow Down Type or a Stand Firm?.

Mimi kwa upande wangu, nina maeneo mawili ya kusaidia, eneo la habari, na eneo la haki Kipindi cha TV, Kutoa Elimu ya Katiba, Sheria na Haki, Kuanza Jumapili Hii Kupita Channel Ten

View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=_KzrMbJ3JisbuXMeP
 
Nadhani watu wengi wangekuwa waumini wa Less is More ingewasaidia sana Wasomaji kuweza kuchambua Mengi kwa siku hususan in this day and age ambapo mambo ni mengi na muda ni mchache...

"Entities must not be multiplied beyond necessity", Hii mada yako huenda ina ujumbe murua sasa kama ungeweza kuuweka katika paragraph moja au mbili kwanini utumie kumi.... Kumbuka kizazi hiki cha Tik Tok kinahitaji mambo in summary...
 
Kuuelewa urais na changamoto zake pamoja na mema wanayoyatenda pia ni kwa kibali cha Mungu.

Kuelewa kwamba mwanasiasa anaweza kuteswa na wakati mwingine akauliwa vichakani ili tu awamu iliyopo wakati huo iweze kuchafuliwa pia inahitajika kibali maalum.

Mara nyingi wengi wetu tunakuja kuujua ukweli baada ya mwenye kupewa kibali kuwa keshaondoka ikulu na imeingia awamu nyingine yenye mtazamo tofauti na ule wa awali.
 
Kaka Paskali asante kwa ujumbe muruwaa! Kabla sijachangia naomba unisaidie kujibu swali langu!

JE! KUNA AWAMU AMBAYO DAMU HAZIKUMWAGIKA?

Pili! Je! Kama watu wanafanya mambo yao huko wanauana au Wanaua na Rais hahusiki kwanini hiyo dhambi aibebe?

Kumbuka Rais SAMIA alisema hajawahi Kuua mtu labda sisimizi! Maana yake inawezekana kabisa hata yale ya Mwembechai, Arusha, Zanzibar, Mbeya, Mwangosi, kina Ulimboka nk haya kuwa matakwa ya kiongozi husika!! Hivyo kwanini ahukumiwe???

Kumbuka laana isiyo haki haimpati mtu!!

Queen Esther
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…