Yule jamaa alinfurahisha kwa namna alivyojuw kulinda vitu, hasa vyakula na mahitaji mengine madogomadogo ambayo kimsingi ndio hugusa wengi (Ngoja nitumie mchele kama mfano).
Kitendo cha Mchele kuganda bei ya 1000-1200 kwa miaka miwili (2020-2021) bila kujali wakati wa mavuno au laah kilinifanya nimkubali sana kwenye food security, kibembe alipoingia tu huyu bibi ndani ya miezi 6 ukafikia 2000/= hapo ndo nilipoanza kushtuka kuwa tunakoelekea ni kubaya.
Ukitaka kutawala vizuri bila kelele hata kama ni mwizi basi hakikisha hauwabinyi watu watu kwenye mahitaji yao ya kila siku (hasa vyakula na viambata vyake) kwasababu hapo ndipo unapogusa hisia za wengi kwa wakati mmoja.
Utakuta mtu analipwa 500000Tsh, ila mtu huyohuyo akiwa na 10000 mkononi bado haitoshi hata kwa mahitaji ya siku moja, emagine ukinunua mchele 2Kg kwenye 5000 unabakiwa na 1000 ambayo haitoshi hata kununua mafuta nusu fanta, haya 10K imeisha hivyo[emoji23].
Sasahivi ni wakati wa mavuno ila gunia la mahindi utalinunu kwa 120k-130k, ikifika december au january tutalinunua kwa 200K, mafuta 5Ltrs 40K, daah[emoji23]. Halafu mtu anakuja kutetea eti mfumuko wa bei ni dunia nzima, nimetoka ZAMBIA mwezi uliopita wanaisha life zuri sana, hata Uganda tu hapa hakuna huo mfumuko wa kijinga kweye vyakula.
Haya maisha utayaona mazuri ukiwa mfanyaniashara (ingawa sera nazo ni mbaya), ila kwa watumishi wa umma mtavaa mno suruali moja kwa miezi[emoji23].