Magufuli alisema "nanyoosha nchi kwanza" Samia kasema "nisimamie uchumi kwanza"

Magufuli alisema "nanyoosha nchi kwanza" Samia kasema "nisimamie uchumi kwanza"

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Ndugu zangu,

Mwaka 2016 Hayati Rais Dr.John Magufuli akiulizwa kuhusu mikutano ya vyama vya siasa na Katiba Mpya alisema "nataka niinyooshe nchi kwanza nipeni muda".

Leo Rais Samia Hassan akijibu hoja hizi za "Katiba mpya" na Mikutano ya vyama vya siasa" kasema "nipeni muda nisimamie uchumi wa nchi" ameendelea kusema "mbunge afanye Mkutano jimboni kwake".

Ni dhahiri tunahitaji kujenga nchi.
 
Ha ha ha kamanda bhana
Amesema anaomba muda aimarishe uchumi halafu ndipo atairekebisha KATIBA . Ameongeza kwa kusema anafanya hivi kwa kutambua kuwa economic power buys political power.

Amemaliza kwa kusema KATIBA Ni muhimu Sana kwasabb italeta utulivu wa nchi.
 
Amesema anaomba muda aimarishe uchumi halafu ndipo atairekebisha KATIBA . Ameongeza kwa kusema anafanya hivi kwa kutambua kuwa economic power buys political power.

Amemaliza kwa kusema KATIBA Ni muhimu Sana kwasabb italeta utulivu wa nchi.
Common sense is not common! Katiba ndiyo ingefanya nchi itulie kwani wawekezaji wangejua kabisa mwelekeo wa nchi. Sasa hivi anaweza kuja kuingia rais mwingine na kuja na mipango yake ya uharibifu kabisa. Jamani hatujajifunza kutokana na makosa ya nyuma tu? Kweli kile kiti cha urais kinalevya sana.
 
RAIS MAGUFULI ALIMWEKA "JELA" MAKAMU WAKE SAMIA SULUHU HASSAN

Na Bollen Ngetti

MWANAMUZIKI Ndanda Kosovo aliwahi kuimba, "Jela..jela ni mbaya, jela..jela ni mateso". Ndanda hakukosea. Aliimba uzoefu alioupata jela hapo Ukonga. Ninamuunga mkono Ndanda kwa uzoefu nilioupata nikiwa jela Keko na Segerea. Jela ni mbaya. Ukiwa jela umezungukwa kuta nene ndefu huwezi kuona nje kwa kifupi unakuwa umenyimwa uhuru wako.

Hata hivyo hakuna jela mbaya duniani kuliko hata Gwantanamo kama jela ya fikra. Yani jela ambapo huwezi kutoa mawazo yako hadharani. Hii ni jela mbaya inayojengwa na shetani tu.

Niliwahi kudokezwa huko nyuma lakini sikuandika maana nilikosa ushahidi kwamba kuna wakati Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alitaka kujiuzulu nafasi ya Umakamu kujiondoa kwenye gereza la fikra lakini wenye hekma na busara walimshauri asifanye hivyo.

Kwa namna Rais Samia Suluhu Hassan alivyoongoza nchi hii kwa siku 100 ni dhahiri alikuwa jela la fikra. Ni ukweli kwamba hakukubaliana na mambo mengi ya Rais Magufuli hata kama leo anasema "Mimi na Magufuli ni kitu kimoja" lakini matendo ni tofauti.

Mama Samia hakukubaliana na uendeshaji wa demokrasia nchini. Alikuwa jela na ilimtesa ndio maana amechukua njia tofauti kuendesha dhana nzima ya demokrasia. Hakuwa na jinsi wala namna. Bila shaka alilia kimya kimya gerezani.

Mama yetu Samia hakupenda uminyaji wa Uhuru wa Habari. Ilimtesa ndio maana "Fundi" alipomwondoa duniani Pombe naye kuchukua hatamu waandishi wa habari wakashangweka. Akaruhusu Uhuru wa Habari na dunia imeshuhudia maana enzi hizo za jela hata andiko hili lisingetoka maana ningekwenda jela la majengo.

Mama Samia hakufurahishwa na kesi za kubumba. Ilimtesa, ilikuwa ni jela kwake ndio maana alipoingia madarakani akafyatua kesi 147 zilizobumbwa na TAKUKURU. Hali hii ilimtesa. Lakini kuachiwa kwa viongozi wa dini wa Uamsho waliosota kwa miaka 9 jela nayo ilimweka jela kisaikolojia Samia. Hakupenda uonevu.

Huyu mama ni swala 5. Ni Muislamu Safi. Hapendi mali za dhulma iwe ni kwa mtu binafsi au Serikali. Hakupenda fedha za dhulma zilizotokana na kesi za kubumba za uhujumu uchumi na ML ndio maana tunaendelea kushuhudia watuhumiwa wakichomolewa magerezani kwa makundi. Lilimuumiza lakini hakuwa na lakufanya maana hakuwa Mkuu wa Maamuzi, Rais. Kitendo cha Mahakama Kuu kuamuru Serikali kurudisha fedha za dhulma kwa kina Mbowe ni ishara nyingine ya kuwa mama yetu aliumia sana kwa matendo hayo. Alikuwa jela.

Makamu wa Rais Samia (sasa Rais) hakupenda watu kuishi kwa hofu na woga. Alitamani watu wawe huru ndani ya nchi yao ila waheshimu Sheria za nchi. Ndio maana leo hata mama lishe, bodaboda nakadhalika wanakwambia, "nchi inafunguka". Wanahisi uhuru walioukosa miaka 5 tuliyoipa kisogo.

Kumbe hata mradi wa Bandari ya Bagamoyo (BEZ) iliyopigwa vita na Pombe ilimkera. Ilimweka jela la kifikra. Hakupenda lakini leo ameamua tufanye mazungumzo mradi ufanyike.

Ndugu zangu, tumuunge mkono Samia kuondokana na gereza la kifikra ili tulisongeshe mbele gurudumu la maendeleo ya nchi.

Binafsi nimejitoa sadaka kumlinda na kumtetea Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan. Mniunge mkono.

Bollen@2021
#MguseMamaNinuke
 
Back
Top Bottom