Magufuli alisema "nanyoosha nchi kwanza" Samia kasema "nisimamie uchumi kwanza"

Magufuli alisema "nanyoosha nchi kwanza" Samia kasema "nisimamie uchumi kwanza"

Ndugu zangu,

Mwaka 2016 Hayati Rais Dr.John Magufuli akiulizwa kuhusu mikutano ya vyama vya siasa na Katiba Mpya alisema "nataka niinyooshe nchi kwanza nipeni muda".

Leo Rais Samia Hassan akijibu hoja hizi za "Katiba mpya" na Mikutano ya vyama vya siasa" kasema "nipeni muda nisimamie uchumi wa nchi" ameendelea kusema "mbunge afanye Mkutano jimboni kwake".

Ni dhahiri tunahitaji kujenga nchi.
Shida ipo kwenye muda huo, je ni miezi, mwaka au miaka?
 
Yani uende kule halafu acha kelele watu watasikia. Namaanisha kuwa uende kule ukawahi vyeo. Si unajua kuwa alikuwa anapiga kampeni kuwa akifika huko awe mkuu wa kina naniluu atakuwa keshapata ushindi huko. Wahi unaweza kuwa mkuu wa wilaya ya sayari ya Jupiter [emoji23]
[emoji3][emoji1][emoji2][emoji2]
 
Kwani Uchumi hauwezi kusimamiwa wakati demokrasia inafanyika? Tunataka uhuru wa kushiriki kwenye siasa za vyama vyetu
 
Kamanda tulia hapo hapo,piga kazi tujenge nchi
Ninyi watu hamuna hoja za kumpinga mama

Magufuli alivyosema hivyo kila kitu nchi hii kilisimama
Hakuajiri, kupandisha madaraja, annual increament na mengine mengi kwa sababu ya kunyoosha nchi

Mama anasimamisha nchi huku mambo mengine yanaenda kama kawaida
 
Mh. Samia S. S. si sawa na Magufuli.

Samia ni Mcha Mungu huku Magufuli akiwa mcha miungu.

Samia ni mpenda haki huku Magufuli ni mnyang'anya uhai.

Samia ni mkweli huku Magufuli akiwa baba wa uongo.

Kufananisha Mh. Samia na Magufuli ni kujitakia laana ya bure.
Nikweli [emoji2][emoji1][emoji3]
 
Wapinzani Wana hoja gani
Mkuu huwa husikilizi vyombo vya habari ama kusoma taarifa mbalimbali kutoka vyanzo tofauti vya habari hapa nchini?

Kweli hujawahi kusikia madai yatolewayo kuhusu katiba mpya, tume huru ya uchaguzi ama uhuru wa kikatiba na kisheria ulioanishwa katika kuendesha shughuli za kisiasa hapa nchini?
 
Hii nchi nadhani ikisimama inaweza kufika kwa Mungu
 
Wakuu,

Ifikie hatua watanzania mstuke sasa na mjue hawa jamaa hakuna wanachofanya tena wanahitaji mbadala ili wapumzike,
Toka 1961 bado jamaa wanadai wanajenga nchi huku wakitegemea misaada ya wahisani ukiangalia dhahabu kila kona, makaa ya mawe kila kona, Tanzanite, bahari, maziwa makubwa kama tanganyika na victoria, mafuta na gesi, hayo yote kwao ni bure bila aibu unakwenda kupandisha kodi kwenye mafuta, kosa ushushe maisha yawe nafuu wewe unapandisha na bila aibu unaenda kuchaji line za simu!

Mjue hawa akili zao zimechoka na haihitajiki tafiti kujua jamaa wamechoka, hawajengi tena wanazidi kubomoa wanatakiwa wapishe wengine wao wapumzike.
 
Kutoka kwenye huu mkwamo,Mama hana budi kukamilisha mchakato wa Katiba pendekezwa ukamilike ili Wananchi wafanye maamuzi kulingana na HAKI.

Tofauti na hapo hatuchomoki,ccm wanajichimbia kuongoza dola kiharamu huku wameshindwa kutuletea maendeleo ya kweli.
 
Hawa nguruwe wanatuona kama hatuna akili vile miaka nenda! Wanatuchezea tu akili. Itafikia wakati watakipata tu kile wanacho kitafuta kutoka kwetu.
 
Hivi 1961 mwenyekiti wenu alikuwa na uwezo kula bata Dubai?
kama sio CCM kukuza uchumi Mwentekiti wenu angeishia kuwa DJ tu
Swali la kipuuzi sana.Ukumbuke akina Mbowe ndiyo walitoa nauli ya mwalimu kwenda UNO.Wakati huo weye umejibanza kwenye punje ya karanga kuleee Nkuhungu!😝😝😝😝😝
 
Wakuu,

Ifikie hatua watanzania mstuke sasa na mjue hawa jamaa hakuna wanachofanya tena wanahitaji mbadala ili wapumzike,
Toka 1961 bado jamaa wanadai wanajenga nchi huku wakitegemea misaada ya wahisani ukiangalia dhahabu kila kona, makaa ya mawe kila kona, Tanzanite, bahari, maziwa makubwa kama tanganyika na victoria, mafuta na gesi, hayo yote kwao ni bure bila aibu unakwenda kupandisha kodi kwenye mafuta, kosa ushushe maisha yawe nafuu wewe unapandisha na bila aibu unaenda kuchaji line za simu!

Mjue hawa akili zao zimechoka na haihitajiki tafiti kujua jamaa wamechoka, hawajengi tena wanazidi kubomoa wanatakiwa wapishe wengine wao wapumzike.
Ukiwa MUONGO uwe unanyoosha maneno.

1961 ilikuwepo TANU.

CCM imeziwa mwaka 77.

Miaka 16 baadaye.

Kwani wewe HARAKATI ZA TANU ulizipinga/mlizipinga?!

Yes TANU ilijenga nchi kama ifuatavyo:

1) KUFUTA UKABILA

2) KUFUTA UDINI

3) KUFUTA UCHIFU WA KIMAMLAKA

4) KUWAUNGANISHA WATANZANIA waliokuwa na uchifu na mifumo ya kichifu KIUTAWALA

5) KUUSIMIKA UJAMAA

6) KULETA AZIMIO LA ARUSHA

7) KUUNGANISHA ZANZIBAR NA TANGANYIKA

***********************

Mwaka 1977 CCM haikuwa na majukumu hayo hapo juu kwa asilimia 100 Kama nilivyotaja......
 
CCM imezaliwa mwaka 1977.....

Mwaka mmoja tu baadae yaani 1978....nchi ikaingia VITANI kumuondoa IDD AMIN DADA aliyeivamia KAGERA na kutishia kuja mpaka Dodoma na Dar es salaam.....

Nchi iliyoasisiwa miaka 17 nyuma ikatumia DOLA MILIONI 500 kuilinda mipaka yake.......

*********************

Miaka 44 ya CCM si mingi katika KUIJENGA NCHI....hususani nchi za kiafrika ambazo TEKNOLOJIA HAZINA....ambazo maadui 3 UJINGA ,MARADHI NA UMASKINI bado ni CHANGAMOTO KUBWA kuliko nchi zilizoendelea Kama UJERUMANI (marafiki wakubwa wa CHADEMA).

#KaziIendelee
 
Wewe nae akili yako inashida, unaitofautishaje TAA , TANU na ASP na CCM au unaachaje generation ya CCM bila kuihisisha na hivyo vyama
 
Back
Top Bottom