Magufuli alisema "nanyoosha nchi kwanza" Samia kasema "nisimamie uchumi kwanza"

Shida ipo kwenye muda huo, je ni miezi, mwaka au miaka?
 
[emoji3][emoji1][emoji2][emoji2]
 
Kwani Uchumi hauwezi kusimamiwa wakati demokrasia inafanyika? Tunataka uhuru wa kushiriki kwenye siasa za vyama vyetu
 
Kamanda tulia hapo hapo,piga kazi tujenge nchi
 
Nikweli [emoji2][emoji1][emoji3]
 
Wapinzani Wana hoja gani
Mkuu huwa husikilizi vyombo vya habari ama kusoma taarifa mbalimbali kutoka vyanzo tofauti vya habari hapa nchini?

Kweli hujawahi kusikia madai yatolewayo kuhusu katiba mpya, tume huru ya uchaguzi ama uhuru wa kikatiba na kisheria ulioanishwa katika kuendesha shughuli za kisiasa hapa nchini?
 
Hii nchi nadhani ikisimama inaweza kufika kwa Mungu
 
Wakuu,

Ifikie hatua watanzania mstuke sasa na mjue hawa jamaa hakuna wanachofanya tena wanahitaji mbadala ili wapumzike,
Toka 1961 bado jamaa wanadai wanajenga nchi huku wakitegemea misaada ya wahisani ukiangalia dhahabu kila kona, makaa ya mawe kila kona, Tanzanite, bahari, maziwa makubwa kama tanganyika na victoria, mafuta na gesi, hayo yote kwao ni bure bila aibu unakwenda kupandisha kodi kwenye mafuta, kosa ushushe maisha yawe nafuu wewe unapandisha na bila aibu unaenda kuchaji line za simu!

Mjue hawa akili zao zimechoka na haihitajiki tafiti kujua jamaa wamechoka, hawajengi tena wanazidi kubomoa wanatakiwa wapishe wengine wao wapumzike.
 
Kutoka kwenye huu mkwamo,Mama hana budi kukamilisha mchakato wa Katiba pendekezwa ukamilike ili Wananchi wafanye maamuzi kulingana na HAKI.

Tofauti na hapo hatuchomoki,ccm wanajichimbia kuongoza dola kiharamu huku wameshindwa kutuletea maendeleo ya kweli.
 
Hawa nguruwe wanatuona kama hatuna akili vile miaka nenda! Wanatuchezea tu akili. Itafikia wakati watakipata tu kile wanacho kitafuta kutoka kwetu.
 
Hivi 1961 mwenyekiti wenu alikuwa na uwezo kula bata Dubai?
kama sio CCM kukuza uchumi Mwentekiti wenu angeishia kuwa DJ tu
Swali la kipuuzi sana.Ukumbuke akina Mbowe ndiyo walitoa nauli ya mwalimu kwenda UNO.Wakati huo weye umejibanza kwenye punje ya karanga kuleee Nkuhungu!😝😝😝😝😝
 
Ukiwa MUONGO uwe unanyoosha maneno.

1961 ilikuwepo TANU.

CCM imeziwa mwaka 77.

Miaka 16 baadaye.

Kwani wewe HARAKATI ZA TANU ulizipinga/mlizipinga?!

Yes TANU ilijenga nchi kama ifuatavyo:

1) KUFUTA UKABILA

2) KUFUTA UDINI

3) KUFUTA UCHIFU WA KIMAMLAKA

4) KUWAUNGANISHA WATANZANIA waliokuwa na uchifu na mifumo ya kichifu KIUTAWALA

5) KUUSIMIKA UJAMAA

6) KULETA AZIMIO LA ARUSHA

7) KUUNGANISHA ZANZIBAR NA TANGANYIKA

***********************

Mwaka 1977 CCM haikuwa na majukumu hayo hapo juu kwa asilimia 100 Kama nilivyotaja......
 
Swali la kipuuzi sana.Ukumbuke akina Mbowe ndiyo walitoa nauli ya mwalimu kwenda UNO.Wakati huo weye umejibanza kwenye punje ya karanga kuleee Nkuhungu!😝😝😝😝😝
Nauli ilikuwa Sh ngapi?Achana na hizo story za kijiweni.
 
Nauli ilikuwa Sh ngapi?Achana na hizo story za kijiweni
Mbona babu yako hakutoa hiyo "senti" ngapi?Jibu ukiegemea swali lako la awali kabla ya hili.@jingalao the jingest.😝😝😝😝😝😝
 
CCM imezaliwa mwaka 1977.....

Mwaka mmoja tu baadae yaani 1978....nchi ikaingia VITANI kumuondoa IDD AMIN DADA aliyeivamia KAGERA na kutishia kuja mpaka Dodoma na Dar es salaam.....

Nchi iliyoasisiwa miaka 17 nyuma ikatumia DOLA MILIONI 500 kuilinda mipaka yake.......

*********************

Miaka 44 ya CCM si mingi katika KUIJENGA NCHI....hususani nchi za kiafrika ambazo TEKNOLOJIA HAZINA....ambazo maadui 3 UJINGA ,MARADHI NA UMASKINI bado ni CHANGAMOTO KUBWA kuliko nchi zilizoendelea Kama UJERUMANI (marafiki wakubwa wa CHADEMA).

#KaziIendelee
 

Wewe nae akili yako inashida, unaitofautishaje TAA , TANU na ASP na CCM au unaachaje generation ya CCM bila kuihisisha na hivyo vyama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…