Kinacho ni uma mimi pamoja na tozo hizo hakuna miradi mipya ya kielezo....na ht walioachiwa inaenda mwendo wa kinyonga anaeumwa mdondo...
Dar ilikua ukikatiza unakuta huku Mibarabara inajengwa, huku wanafunga taa barabara za mitaaani, huku mi flyover watu wanachakarika, huku masoko huku hospitali, huku Dawasco wanavuta mabomba...
Asubuhi unapishana na Jaffo na watu wake wa Tamisemi wanaenda kukagua miradi, ukitatiza mbele unakutana na mkutano wa Lukuvi or Bashite wanatatua migogoro ya ardhi...
Ukifungulia TV unakutana na Waziri wa Maji ameliamsha huko mkoani, or waziri wa Nishati yupo Rusumo kwenye Bwawa la Umeme kukagua maendeleo...
Ndalichako na shule zake za Mfano..
Huku Bi Ummy anahangaika na vituo vyake vya Afya
Huku Mpango anapokea gawiwo...
kule Biteko anafungua soko la madini...
kule wakuu wa mkoa wanacheki km tofali za ujenzi ndo zenyewe or wanapokea madawati...
Ukiingia youtube ni video tu za miradi, kuanzia TRC, Tanrods, MeliTV mpaka Tamisemi.
huku JPM anapokea mindege
ili mradi kazi kazi, purukushani za kazi kila sehemu.
Nlikua kila week lazima nipitie website ya Tanraods kujishtua moyo na miradi mipya mipyaaa...now ht ule mradi wa mwendokasi wa kule kwetu g'mboto uliotanganzwa Aug 2020 mpaka leo hakuna jipya.
Now with all that money za mitozo na mikopo inchi bado imelala doro.
What happened to us?
I real miss the old days..