Uchaguzi 2020 Magufuli anaiona Tanzania nzuri miaka 30 ijayo, shida wengi tuna njaa

Uchaguzi 2020 Magufuli anaiona Tanzania nzuri miaka 30 ijayo, shida wengi tuna njaa

Hata Nyerere aliiona Tz yenye kujitegemea wakati anaanza kutawala kipindi hicho nchi bado bikra kabisa wazungu wakampa miaka michache baadae beberu yaan UK lilimuokoa asipinduliwe, miaka michache tena akafeli vibaya mnoooo kwenye utawala wake mpaka akakimbia madaraka (ila kumtunzia heshima tunasemaga mzee aling'atuka i.e. wajanja wanajua kung'atuka ni kwamba umeng'ang'ania ila imeshindikana so inabidi uachie tuna hamna namna) Magu hata angepewa miaka trillion kamwe usitegemee mapinduzi ya kiuchumi cha msingi pambana na hali yako Magu kutangazwa mshindi ipo wazi sasa basi tegemea ugumu wa maisha, ufukara, umaskini wa kupindukia utaongezeka mara dufu panapo majaliwa ya Mungu tukumbukushane huu uzi mwaka 2023 tarehe kama hii ya leo. Kumbuka ccm wamekaa madarakani miaka inakaribia 60 sasa kama wameshindwa miaka yote kuleta maboresho ya maana kwenye uchumi iweje leo uamini kuwa wamepata muarobaini wa matatizo ya waTz? Kila baada ya miaka 10 mgombea Uraisi wa ccm anapojinadi utadhan inchi ilikuwa chini ya upinzani, Magu kaingia na Tz ya viwanda leo hii hili limekufa hajui hata anasimamia nini kw sasa, kazi kusema tu anataka Sugu amsugue, anataka akistaaf aende zenj akaoe mke wa pili, anataka wagogo wampe mwali kigoli wa miaka 18!!
 
Ni kwa vile hujui South Korea ya leo ilitokana na kiongozi wa aina gani; unaweza kuwa unafurahia sana kutumia Samsung au Kia lakini hujui chimbuko lake.
Kasome tena historia ya uchumi wa South Korea. Park alikuwa dikteta yes lakini hakuwa mbomoaji nchi kama huyu. Park hakurudisha nyuma juhudi za Cheobels kujiimarisha. Park hakuuwa pivate sector ndio maana huo mfano uliotoa wa kampuni ya Samsung ni ya mtu binafsi, POSCo pia, KIA pia nk nk.
 
Mawazo haya ingekuwa umeyatoa kabla ya hii miaka mitano huenda kidogo kuna watu wangekuelewa ila si kwa sasa. Rangi ya huyu mtu ishajulikana hana uwezo wa kuivusha popote zaidi ya kuja kuiacha nchi pabaya kama alipoiacha Julius, na mbaya zaidi ikiwa vipande vipande tofauti na alivyoiacha Julius. Badala ya kuweka sera za kupanua vyanzo vya kodi yeye kaja kuongeza kodi kwa vyanzo hivyo hivyo. Take my word, miaka mitano ijayo ni migumu mnooo kwa JPM kiasi kwamba ccm itakosa ushawishi maradyfu ya ilivyo sasa. Hatakuwana majibu ya ajira kwa vijana, hatakuwa na vyanzo vipya vya kukusanya kodi, hatakuwa na "terms" nzuri za kukopa huko anakokopa nk nk. Wapambe wake mtasingizia vikwazo lakini ukweli ni kwamba misingi ya uchumi iliyochimbwa kwa miaka 30 iliyopita imetetemeshwa na kuvurugwa mnoo.
 
Huu ndio muda wa kuandaa katiba bora ya msingi itakayo liendesha taifa baada ya miaka zaidi ya 50 ya giza na kujitawala.

Magufuli hawezi kuleta hiyo
 
kuangalia mbele ni pamoja na kuwepo na haki za binadamu. Kama tungetaka hayo maendeleo wakoloni ndiyo walikuwa mbadal, tuliwakataa Kwa sababu tulitaka heshima yetu, haki zetu. Huwezi kumpiga mtu risasi 38 halafu iwe ndiyo sababu ya kujenga daraja.
to hell with your bridges!
 
Kasome tena historia ya uchumi wa South Korea. Park alikuwa dikteta yes lakini hakuwa mbomoaji nchi kama huyu. Park hakurudisha nyuma juhudi za Cheobels kujiimarisha. Park hakuuwa pivate sector ndio maana huo mfano uliotoa wa kampuni ya Samsung ni ya mtu binafsi, POSCo pia, KIA pia nk nk.
Basi huijui historia ya uchumi wa Korea jinsi serikali ilivyowekeza kwenye miundombinu na viwanda; vile vile huenda pia hujui jinsi uchumi wa Japan ulivyokua kwa serikali kuwekeza kwenye miundombinu na viwanda.

Uchumi unakua kwa kuwa na infrastructure nzuri, jambo ambalo linafanywa na serikali pekee. Serikali yoyote duniani hujiendesha kwa kukusanya kodi. Unapochukia serikali kwa kukusanya kodi na kujenga miundo mbinu basi sijui wewe unataka serikali ya namna gani. Hii mediocrity ya kupenda kula bata bila kulipa kodi na kuendelea kuwa na miundo mbinu hovyohovyo isiyopotika wakati wa masika inabidi uindoe kichwani mwako. Shughuli za kiuchumi zinatakiwa ziwe zinafanyika all year round, siyo eti wakati wa masika watu wanajifungia ndani tu kwa sababu barabara hazipitiki. Kuna kauli za magufuli sikubaliani nazo, ila nakubaliana kabisa na jinsi anavyoendesha serikali kutekeleza wajibu wake. Normally serikali yoyote hufanya kazi kwa nguvu, siyo kwa kubembelezanana, ndiyo maana kuna sheria, anbazo ni instruments za matumizi ya nguvu.
 
First lady uko wapi mbina hatukusikii??!
Baba kashatamani huku ngambo ya maji akaongeze 2nd lady kazipenda baibui baada ya..
Njio okoa jahazi lisizame.
 
Kishajichokea huyo kwa kauli yake mwenyewe na Watanzania wengi wanaojitambua hawataki hata kumsikia achilia mbali kumpigia kura.

Nimejipa kazi kuwafatilia wagombea wawili wa uraisi wanaoonekana kupendwa na watu wengi, nimegundua kuwa Dr. Magufuri anawaza mambo ya miaka kama 30 ijayo ndo tule bata. Ili hali Ndg Lisu akiwaza mambo ya leo, kesho itajulikana ikifika.

Shida kwa watu wengi, bado huduma muhimu ( chakula, malazi na mavazi) ni shida njaa ni kubwa.

Cha kujiuliza ni,tufanye maendeleo atakayefika miaka hyo ale bata au tule leo wa miaka hiyo watajijua?

Maoni yangu ni kwamba Ndg Lisu aendelee kutupambania kama mwanaharakati, ili kumsutua Magufuri atoe vitu kama ajira ili hela irudi mtaani, na Dr. Magufuri aendelee na maono yake ya kujenga Tanzania ya miaka 30 ijayo.

Maoni yako ni yapi? Kumbuka maendeleo hayana chama.
 
Ameshindwa kutengeneza mifumo na Taasisi Imara.
Amekazana kuteka watu ,kuua ,kuwapoteza watu, kubana uhuru wa vyombo vya habari na mabaya ya kila namna .

"Hafai hata kuwa kiongozi wakijiji labda Nyapala wa bara bara.
RIP kingunge
unadai uhuru upi wa vyombo vya habali ?? na huku kesho wanatz wanahitaji vyombo vya usafiri vya kisasa vyenye speed ktk dunia mpya "mtu avundike ndizi akiwa MWANZA baada ya saa 6 ziwe DAR sokoni anauza na nauli nafuu kwa usafiri wa treni za kisasa...."NYAGHUKUNDO"
 
Hii kasumba ya kuamini katika mtu sijui itaisha lini, tunahitaji katiba imara, mifumo na taasisi imara ambazo zitamsimamia kila anayeingia. Aje TL atupe katiba nzuri naye tumbane nayo.

unadhani ikiwa hivyo nafasi ya rais itakuwa ni nini??

sio kweli kwamba katiba imara italeta maendeleo,kama akili za wengi zinavyoamini katika,mtu,katiba,mfumo au chama.ni kazi peke yake ndio inazalisha maendeleo jaman tuanche kuzidanganya akili zetu.
 
Tanzania kama ni nguo miaka mitano mingine ya huyo anayejiita MWENDAWAZIMU basi nguo hiyo itakuwa HAITAZAMIKI na hakuna binadamu yeyote mwenye akili timamu atakayethubutu kuivaa.

Nimejipa kazi kuwafatilia wagombea wawili wa uraisi wanaoonekana kupendwa na watu wengi, nimegundua kuwa Dr. Magufuri anawaza mambo ya miaka kama 30 ijayo ndo tule bata. Ili hali Ndg Lisu akiwaza mambo ya leo, kesho itajulikana ikifika.

Shida kwa watu wengi, bado huduma muhimu ( chakula, malazi na mavazi) ni shida njaa ni kubwa.

Cha kujiuliza ni,tufanye maendeleo atakayefika miaka hyo ale bata au tule leo wa miaka hiyo watajijua?

Maoni yangu ni kwamba Ndg Lisu aendelee kutupambania kama mwanaharakati, ili kumsutua Magufuri atoe vitu kama ajira ili hela irudi mtaani, na Dr. Magufuri aendelee na maono yake ya kujenga Tanzania ya miaka 30 ijayo.

Maoni yako ni yapi? Kumbuka maendeleo hayana chama.
 
Kusema " maendeleo hayana chama" na hapo hapo unasema " msiponichagulia diwani, mbunge na raisi wa ccm, sitawaletea maendeleo" ni kutoa kauli mbili zinazopingana! Ni wagonjwa wa akili na wenye mtindio wa ubongo watakaoshindwa kuelewa ujinga huo wa kibaguzi dhahiri!
Hizo ni Kauli za Kisiasa tu. Wagombea huwa na kauli nyingi (propaganda, ahadi hewa etc.) ili tu kujaribu kushawishi wananchi wawapigie Kura.
"Maendeleo hayana Chama" huwa inamaanisha kwamba mfano Chama "A" kikishinda Uchaguzi na kuongoza Serikali, basi Maendeleo na Miundo Mbinu itakayojengwa na Chama "A" itatumika na Wananchi wote bila kujali itikadi zao za Kisiasa (chama), Haijalishi wananchi ni wanachama wa Chama "B", "C" au "D" Hivyo wote watanufaika kwa kutumia Maendeleo au Miundo Mbinu husika kujiletea maendeleo yao binafsi...
By the way, ila kwa AFRICA hapa kwa kipindi hiki yaani Rais utawale Muhula wa Kwanza halafu Muhula wa Pili ushindwe Uchaguzi daaah Hata wanao watakucheka kwa kweli.
Anyway, wacha tuone hiyo Octoba 28, Cha muhimu ni Tuhimizane Tarehe ikifika tukapige Kura, tusiishie tu kupiga soga Vijiweni na Online. Tupige Kura!
 
Kishajichokea huyo kwa kauli yake mwenyewe na Watanzania wengi wanaojitambua hawataki hata kumsikia achilia mbali kumpigia kura.
Mzee mzima kazi yako kuosha vibibi vya kizungu, mama yako mzazi anataabika huko kijijini, rudi nyumbani Bubu Ataka Kusema umwangalie mama yao. Aibu!
 
Magufuli hana uwezo wa kuona mbele hata kwa mwezi mmoja tu. Mfano wakati anakwiba mapesa kwenye hizi provident funds zetu hakujua kuwa kuna wataostaafu mwezi unaofuata
Hayo ni mawazo yako. Je wewe unaona mbali?
 
Umesema miaka 60 mpaka sasa hakuna Maendeleo yoyote...
Sikuwepo mwaka 1964 ila ni wazi kuwa Tanzania ya mwaka 1964 haiwezi kufanana na Tanzania ya mwaka 2020 kwa kuzilinganisha Kimaendeleo (Uchumi, Miundo Mbinu [umeme, barabara, Madaraja, Mawasiliano etc.], Afya, Elimu etc. )...
Mimi nakubaliana na Mtoa Mada kwa jinsi alivyowachambua Lissu na Magufuli.
Cha msingi ni tupige kura Tarehe 28 Octoba ikifika, Haya mengine tuwaachie Wanasiasa wenyewe.
Maana Mwanasiasa yeyote lengo kubwa ni Maslahi yake Binafsi kwanza, hata kama atatamka maneno matamu kiasi gani. Kutamka na Kutekeleza ni vitu viwili tofauti! Na hii kwa Wagombea wa Vyama Vyote.

Back
Top Bottom