Wakati unafuatilia kampeni hujisikiaje mwanzoni mwa kampeni unaambiwa "Maendeleo hayana chama" then baada ya nusu saa unasikia mtu yule yule anasema "Msipomchagua mbunge wa CCM hapa maji hamuwezipata" Then mtu yule yule wakati anamaliza kampeni siku hiyo hiyo tena ndani ya masaa tu anasema tena maendeleo hayana chama!!! Hiki ndicho ulichomaanisha kuwa na mawazo ya miaka 30 mbele!!Nimejipa kazi kuwafatilia wagombea wawili wa uraisi wanaoonekana kupendwa na watu wengi, nimegundua kuwa Dr. Magufuri anawaza mambo ya miaka kama 30 ijayo ndo tule bata. Ili hali Ndg Lisu akiwaza mambo ya leo, kesho itajulikana ikifika.
Shida kwa watu wengi, bado huduma muhimu ( chakula, malazi na mavazi) ni shida njaa ni kubwa.
Cha kujiuliza ni,tufanye maendeleo atakayefika miaka hyo ale bata au tule leo wa miaka hiyo watajijua?
Maoni yangu ni kwamba Ndg Lisu aendelee kutupambania kama mwanaharakati, ili kumsutua Magufuri atoe vitu kama ajira ili hela irudi mtaani, na Dr. Magufuri aendelee na maono yake ya kujenga Tanzania ya miaka 30 ijayo.
Maoni yako ni yapi? Kumbuka maendeleo hayana chama.
Kama ndani ya masaa 3 kumekuwa na disorganized ideas, messages, opinions, visions atakuwaje na mawazo ya 30 yrs ahead??? Watanzania tuseme ukweli na kumwogopa Mungu!