Uchaguzi 2020 Magufuli anaiona Tanzania nzuri miaka 30 ijayo, shida wengi tuna njaa

Wakati unafuatilia kampeni hujisikiaje mwanzoni mwa kampeni unaambiwa "Maendeleo hayana chama" then baada ya nusu saa unasikia mtu yule yule anasema "Msipomchagua mbunge wa CCM hapa maji hamuwezipata" Then mtu yule yule wakati anamaliza kampeni siku hiyo hiyo tena ndani ya masaa tu anasema tena maendeleo hayana chama!!! Hiki ndicho ulichomaanisha kuwa na mawazo ya miaka 30 mbele!!

Kama ndani ya masaa 3 kumekuwa na disorganized ideas, messages, opinions, visions atakuwaje na mawazo ya 30 yrs ahead??? Watanzania tuseme ukweli na kumwogopa Mungu!
 
Una akili sana.
 
Urusi ilibadilika kutoka nchi ya kilimo na kuwa Industrialise country within 20 years.
Ukitaka kuwasikiliza wenye njaa maendeleo yatakuja baada ya sisi kufa.
 
Babuu wa kimeru kaniongezea siku ya kuishi kwa hoja za Magufuli awe Rais kwa miaka 20 !
Tazama video clip

 

Attachments

  • 1601892321538.mp4
    4 MB
  • 1601781206792.mp4
    8.9 MB
Kama naiona yeye sisi hatuioni basi sio mbaya akainee chato
 
Demokrasia ni watu kuchagua aina ya maendelo wanayoyataka wala siyo kuchaguliwa na mtu mwingine
Usijifanye hujaelewa ni hivi tunataka maendeleo ya watu vitu baadae
 
Kuna waliokuwa na umri wa wa kutosha wakati tunapata uhuru, eti nao wanasema hakuna kilichofanyika hadi leo. Sishangai vijana wakisema hivyo. Ila kwa hawa wazee, ni tatizo.
 
 
Mungu nasubiri baada ya tarehe 28 Lissu atakavyo futa hapa kazi tu kwenye ndege
 
hapa unapoteza tu mda, hawa jamaa hawaelewagi wanaongea nn! nakushauri kafanye tu shuhuli zingine za maendeleo hawa jamaa ni chama kizima ndo akili zao zpo ivo
Hawa hawa ndio watakuwa viongozi wetu chama chao kikichukua nchi.
 
Kama wameshindwa kwa miaka 30 wataweza kwa miaka 5? je hiyo miaka 30 utakuwepo?
 
Ye alitakiwa aitengeneze Tanzania aliyopewa kwa miaka 5,miaka 30 haimuhusu sasa miaka mitano imeisha hamna kitu au Ndo tusubiri mpaka 30?na je msoto tunaupitia wote?
 
Kwani Hawezi kuleta hayo mavitu yake bila kuteka, kupora, kuua, kupiga, watu risasi, kufunga watu bila hatia?
 
Usijifanye hujaelewa ni hivi tunataka maendeleo ya watu vitu baadae
Ndio point yangu, kwamba watu wachague aina ya maendelo wanayoyataka siyo mtu awachagulie.
Maendelo yanatokana na nguvu(Kodi) za wananchi, hivyo ni vizuri wananchi wakaamua ni kitu gani watakacho kwa nguvu zao wenyewe.
 
Mtu yeyote anayetaka kubadilisha jambo na kuona matokeo yake miaka 30 mbele hayuko serious au hajui anachofanya.

Uchumi ni jambo linalobadilika ndani ya week kadhaa tu, wenzetu hupima matokeo ya sera za uchumi katika quarters (robo mwaka).

Awaachie wanaoweza kuleta madhara katika miezi, sio miaka!!
 

Utakuwa kula kulala si bure.sera za jiwe ni za kizamani hazijawahi fanikiwa popote dunia,mtu ambae ajawahi soma hata development study atajua vipi kuhusu maendeleo ya watu.
Uliona wapi unaweza tengeneza future kwa kuuwa sekta binafsi,kuuwa diplomasia, kusomesha watu namba, kuminya demokrasia,kutunga Sheria Kandamizi, huwezi endelea kwa kuwa kisiwa Hali nchi tajiri zinaimarisha diplomasia.
 
Mfano pesa zilizowekezwa kwwenye hii miradi yote zingewekezwa kwenye kilimo ndani ya miaka 3 tu zingezaa mara tatu huku zikichochea ajira, pesa za kigeni, kuliko kutumia zaidi ya tilioni moja kununua ndege zinazoajiri watu 404 huku wanaomudu kupanda ndege awafiki hata milioni 1 nchi nzima.
Kwa mchumi hii miradi yote ilitakiwa ifanyike kwenye stage ya tatu ya ukuzaji uchumi.
Kiongozi mzuri utokana na fani ya sheria,diplomasia,uchumi au biashara, sayansi ya Jamii hizi fani zingine ni chenga tu maana zinahitaji claiming capacity na sio reasoning capacity, uongozi ni reasoning na sio claiming. Kuhesabu kilometers za barabara kumetuingiza chaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…